Ujenzi wa mjeredi mgongoni

Ujenzi wa mjeredi mgongoni

TCSPM

Member
Joined
Dec 3, 2020
Posts
52
Reaction score
78
Wadau kichwa tajwa hapo juu

Niko na 26 Years Jijin Dar income 200k per month na 30k allowance per week ktk harakati za maisha Mungu amenisaidia kuwa na nidhamu kubwa sana ya kutimiza malengo yangu ya Kila mwezi nayojipangia
Toka 2021 mpaka Leo nikiwa ktk shauku ileile.

Hakika ujenzi wa kipato duni ni Fimbo yenye maumivu makubwa sana hasa unapowashwa zaidi na malengo yako yaan unayapa malengo nafasi kubwa sana kuliko chochote kile.

Wadau ujenzi wa aina hii unanifanya naishi maisha duni sana mpaka nawaza kwani wenzangu wa kipato hiki wanakidhi vip mambo mengine bila kuathili ndoto zao?

Ujenzi wangu umefika hatua ya boma vyumba vitatu vya kulala , jiko na sebre ndani vyumba 3 kimoja ni master.

Style yangu ya kutimiza malengo ni kuwekeza fedha mojakwamoja ktk vitu naitaji kama matofali nalipia nondo nalipia siment kadhalika baada ya hapo hupita kuvikusanya siku ya ujenzi nimefanikiwa kiasi kikubwa ila Kwa maumivu sana.

Kinacho niacha hoi ni hizi gharama ambazo zinazaliwa mara TU ukifika site hii ndio panga linaloniacha mfukoni mtupu wadau hii inakuwaje?

IMG_20220731_180108.jpg
 
Naomba picha ya hilo boma lilipofikia na eneo ulilojenga hizo room hadi na sebule. 200,000 per month ukiitumia kujenga hapa Dar si unafariki kabisa?
 
Hongera kwa kujinyima hakika yahitaji moyo kwa mshahara wa 200k, mkuu menu yako ipoje Hadi unatoboa kusave
 
Back
Top Bottom