Ujenzi wa nyumba: Budget ya milioni 25

Ujenzi wa nyumba: Budget ya milioni 25

Financial Analyst

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
1,849
Reaction score
3,506
Hello quick thinkers na valuators wa JF, nina budget ya Tsh 25 millions. Kiwanja kipo tayari na eneo la ujenzi ni mkoa wa Mara.

Je hiyo budget inaweza kufinance ujenzi wa awali, kupaua na finishing katika nyumba yenye sifa zifuatazo:

1: Ukubwa wa mita 12 × 13
2: Master room moja
3: Single rooms tatu
4: Public toilet ya ndani moja
5: Average sized sitting room
6: Small dining room
7: Kitchen ya ndani ndogo
8: Fence
9: Isiyo ndefu kwenda juu (Bati chache)
 
Subiri wataalam wanakuja ila mambo mazuri na ya hakika yanahitaji gharama. Wataalam nao wanalipwa maana mkono mtupu haulambwi
 
Hiyo nyumba mbona kubwa sana? Vyumba vinne vya kulala vya nini vyote hivyo?

Hiyo hela inatosha nyumba ya vyumba viwili, sitting cum dinning, jiko na choo cha kushare. Hapo unamaliza kabisa.

Jambo la kuzingatia kama una hiyo fedha cash, nunua materials zote kwa jumla na fanya utafiti wa bei hasa mfano kuagiza vitu kama vifaa vya maji, umeme, bati, tires etc. Mfano unaagiza vyote DSM na bei ya usafirishaji kama 500k kwa pamoja utasave sana.

Usinunue materials mikoani kwa rejareja, hiki ndio kinakula fedha za finishing.
 
Kweli kabisa
 
Haitatosha.
Mimi siyo fundi ila nimeshiriki ujenzi kwa muda, milioni 25 kwa nyumba unayoifikiria haitoshi.
Ila utajenga mpaka kufikia kiwango cha kuweza kuhamia na kuishi.
Huu ni ushauri halisi japo kwako inaweza usiwe nzuri kulingana na matarajio yako. Nimefanya ujenzi wenye kufanana na specifications sawa na zako.

Kingine ninavyofahamu mtu kukujibu hapa si vizuri, slope ya kiwanja na nature ya udongo pia huchangia kupandisha cost za ujenzi.
 
Hello quick thinkers na valuators wa JF, nina budget ya Tsh 25 millions. Kiwanja kipo tayari na eneo la ujenzi ni mkoa wa Mara.

Je hiyo budget inaweza kufinance ujenzi wa awali, kupaua na finishing katika nyumba yenye sifa zifuatazo:

1: Ukubwa wa mita 12 × 13
2: Master room moja
3: Single rooms tatu
4: Public toilet ya ndani moja
5: Average sized sitting room
6: Small dining room
7: Kitchen ya ndani ndogo
8: Fence
9: Isiyo ndefu kwenda juu (Bati chache)
Ongeza 5M. Maana kwa nyumba unayotaka kama uko Dar. Msingi na Boma itakula 11M. Mbao na bati itakula 10M. Zilizobaki 4 Ni madirisha na milango. Lazima uwe na 5M ya sakafu ukuta na chini. Hapo nyumba bado finishing haijapendeza kabisa ila utahamia.

ili utie na rangi, umeme na plumbing, gypsum na tiles it tale another 10M
 
35 million sio mbaya eti
 
Inaweza ikatosha au isitoshe, tafuta fundi akupe makadirio yake kwanza, ikiwa fundi ni mtu wako wa karibu itakuwa poa zaidi bei itapoa, ukiwa na muda uwepo site, material jitahidi kununua kwa jumla au lah km una idea ya ufundi usipattane na fundi boma zima, waje mafumdi wajenge uwalipe kwa tofali.

Kuna kibanda cha vyumba vi4, kimoja master na ukumbi wake, choo cha public, sebule, jiko, stoo na dinning, nimetumia kama milioni 20 hv bado finishing kidoogo hapo nishaipaua, madirisha, chini niliweka zzege, plasta, mabomba ya umeme tayari gypsum board.

Kilichonisaidia mimi ni kujuana na watu, kasoro boma tu ndio nilikubaliana na fundi akataka 1.8 huyu ni fundi wa huko huko ninakojengea(nimejenga kijijini, hivyo kuweka ukaribu na watu nikaona si vema kuchukua mafundi mbali, huyu aliwahi nitengenezea kisima) alipomaliza boma, kupaua akaleta michongo ya tamaa akataka milioni 2, nikapiiga chini, kuna shemeji yangu ni mtaalam wa kupaua nikamfata nikampa mikabala, akaniambiia ninunue vifaa vyoote aje apige kazi siku 2 tu nimuandalie laki 6, wiring nikamchek broo wangu mmoja akaniambia ninunue vifaa vyote aje apige kazi kwa siku mbili yeye hakutaka tsh 10 zaidi nikawapoza vibarua tu.
Plasta, zege la chini, shimo la choo na kukiset choo cha public, na gypsum nikampata mwanangu akanifanyia kazi kwa bei chee tu.
Madirisha nikanunua vifaa kuna kijana tunafanya nae mazoezi ya mpira sehemu akaja kunifanyia home, kila dirisha nilimpa elfu 15 kama sijakosea.

Hapo unaweza kupata picha kamili.
 
Back
Top Bottom