Ujenzi wa nyumba: Budget ya milioni 25

Basi inabidi atafute wataalam zaidi kama vile akina Kingo Properties Ltd ambao wamejenga na wanauza nyumba ya vyumba viwili, choo, bafu na sebule kwa Milioni TANO NA NUSU huko Mwasonga, Kigamboni!
 
Makadirio hayo anayaweza Financial Analyst, lakini mimi kwa uzoefu wangu nasema inaweza kujenga nyumba; sasa ni mbwembwe kiasi gani utaweka ndani na nje ya hiyo nyumba, inaweza isitoshe! Halafu kwenye septic system siku hizi zipo za aina nyingi na cheap, sijui kuna za aina ya Urusi na nyingine ambazo ukiweka hakuna suala la kunyonya nyoka hayo maji taka! Hivyo gharama kwa kweli ni very subjective inapokuja kwenye ujenzi wa nyumba.
 
Sure kabisa
 
Kwa sababu ulivyosema inatosha, labda ulishawahi kujenga nyumba ya aina hiyo?
Ndio maana nikauliza kama wewe unakumbuka ulitumia kiasi gani?
 
Kwa sababu ulivyosema inatosha, labda ulishawahi kujenga nyumba ya aina hiyo?
Ndio maana nikauliza kama wewe unakumbuka ulitumia kiasi gani?
Nilishawi kujenga lakini kukumbuka gharama leo siyo rahisi, lakini kwa kuona namna ujenzi unavyo kwenda na bei za vifaa na gharama za mafundi, bado naamini hiyo pesa inatosha, labda kama nilivyo sema mtu aweke mbwembwe za ziada!
 
25m haitoshi hio nyumba ni kubwa,na kwa hizo points tisa ulizoweka Sio nyumba simple. Nyumba ya sqm156 sio ndogo.
 
Unajua ana familia ya watu wangapi?!?!!!!!
 
Naomba msaada wakujua japo maduka machache yanayouza vifaa bei rahis vya jumla hasa mabomba ya maji, umeme na tiles kwa Dar. Npo hatua ya kupauwa.
 
kwa bei hizi nondo mm 12 wanauza 24,000
cement 15,000 kwa Dar vijijini 22,000 hiyo pesa yako itaishia kupandisha boma tu. tafuta fundi kwanza jengea chini nyumba yako kabla hujaanza kununua material. hiyo pesa haitoshi, labda kama utaamua kuhamia site[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…