Ujenzi wa nyumba ya matofali ya kuchoma Buyuni

Ujenzi wa nyumba ya matofali ya kuchoma Buyuni

Damp-Proof-Membrane.jpg
Mimi naomba kufahamu kati ya matofali ya kuchoma na block yapi hayavuti maji? nimeona nyumba nyingi karibu na msingi zinakuwa na fungi hivi kutokana na maji yaliyo ardhini

Zote tu zinavuta maji kama msingi ni mfupi yaani msingi unaishia karibu sana na level ya ardhi au umejenga sehemu yenye unyevunyevu, tatizo huwa tuna-ignore kanuni za ujenzi kutokana na kwamba kuna nyumba zinajengwa unakuta ule ukuta haunyonyi maji hivyo huwa tunahalalisha kwamba ndio inapaswa kuwa hivyo.

Nyumba yoyote tunatakiwa tunapomaliza msingi au uwe umepiga jamvi, kabla ya kunyanyua ukuta huwa wanaweka mpira (damp proof membrane) ambao ni size ya tofari pale chini kisha wanaweka morta (mchanganyiko wa mchanga na cement) na kuanza kujenga ili kuzuia maji yaliyo chini yasipande kwenye ukuta juu. Ushauri wangu, ile nyumba yako ya pili unayojenga weka mpira (damp proof membrane) kabla ya kujenga kozi ya kwanza ya matofali

Hiyo picha juu ndo huo mpira niliosema (damp proof membrane)
 
Back
Top Bottom