kolelosi
JF-Expert Member
- Jun 16, 2015
- 814
- 1,940
Respect mkuu naona umeichambua copper belt sawa sawa, ukweli huu ukanda ni wenye kipato cha uhakika ukilinganisha na njia ya kati... lakini tukifanya hivi malori yetu yataendelea kupata mizigo???Mradi wa sgr umetutia madeni. Halafu mradi ukikamilika utatutia madeni zaidi. Pia ramani ya mradi imekosewa. Reli ya sgr inatakiwa iende sehemu ya mizigo mingi. Na mizigo mingi ni shaba ya Zambia, na madini ya cobalt na shaba yaliyopo Lubumbashi/kolwezi/katanga DR Congo.
Sasa hii reli naona imepotea uelekeo wa mizigo mingi mno kwa hiyo haitarudisha hela. Kwa hiyo ni madeni juu ya madeni halafu riba. Mizigo mingi ipo kusini kwa Congo na Zambia. Halafu reli inaelekea mashariki mwa Congo
Hao Rwanda na Burundi hawana mzigo wa maana kuzidi Zambia na Cobalt na Copper ya Drc congo. Ilitakiwa SGR iende kwenye mizigo ya maana huko kwenye migodi ya zambia na Congo.
Hii sgr inayojengwa imekosewa kabisa. SGR ilitakiwa iwe Dar-Kapirimposhi-Lubumbashi(ikiwezekana ipite kwenye migodi ya Copper na Cobalt iliyopo Kolwezi, Mutanda huko Drc ndanindani)