Ujenzi wa Shimo la kuhifadhia maji ya ujenzi

Nkondo 2

Senior Member
Joined
Oct 10, 2016
Posts
181
Reaction score
144
Salaam wakuu, nahitaji msaada wa kitaalamu, nahitaji kuchimba shimo ili niwe nahifadhi maji Kwa ajili ya ujenzi unaoendelea.

Nahitaji kuchimba shimo litakaloweza kubeba ujazo wa litre elf 7, naomba kufahamu Kwa ujazo huo je, inanipasa nichimbe shimo Kwa vipimo gani? (Yani nichimbe futi ngapi kwenda chini na upana uweje?)

Karibuni....
 
Salaam wakuu....
Nahitaji kujenga shimo la kuhifadhia maji kwaajili ya ujenzi. Naomba kufahamu Kwa shimo linaloweza kubeba litre elf 7 nichimbe Kwa vipimo gani? yaani urefu uwe ni futi ngapi na upana uweje?

Karibuni....
 
Chimba shimo walau urefu kwenda chini 5m(mita tano), kipenyo(diameter!?) 1.3m na utapata ujazo unaoutaka wa lita 7000
 
Salaam wakuu, nahitaji msaada wa kitaalamu, nahitaji kuchimba shimo ili niwe nahifadhi maji Kwa ajili ya ujenzi unaoendelea.

Nahitaji kuchimba shimo litakaloweza kubeba ujazo wa litre elf 7, naomba kufahamu Kwa ujazo huo je, inanipasa nichimbe shimo Kwa vipimo gani? (Yani nichimbe futi ngapi kwenda chini na upana uweje?)

Karibuni....
Volume (V)= 3.14 x Radius(R)² x Depth(H)
V=3.14×R²xH
V/(3.14xH)=R²
SQRT(V/3.14H)=R
R=SQRT(V/3.14H)
R=SQRT(7/3.14H)

Hapo kuna unknown mbili (Radius na Depth), kwa hivyo itabidi tuwe tunaplug unknown moja ili kupata unknown nyingine

Mfano ukitaka kuchimba shimo la futi 8 (ambayo ni sawa na mita 2.4)
R=SQRT(7/3.14x2.4)
Radius itakuwa 0.96m

Ukitaka kuchimba shimo la futi 10 (ambayo ni sawa na mita 3),
R=SQRT(7/3.14x3)
Radius itakuwa 0.86m

Ukitaka kuchimba shimo la futi 12 (ambayo ni sawa na mita 3.6)
R=SQRT(7/3.14x3.6)
Radius itakuwa 0.79m

Kiufupi kama utachimba shimo la futi 8 na kuendelea, radius ya mita 1 inatosha kabisa kupata huo ujazo

Kwa mahitaji ya Ramani, Makadirio au Ushauri kuhusu Ujenzi tuwasiliane +255(0)624068809
 
Shukrani Sana mkuu Kwa ufafanuzi huu mzuri japo umetumia lugha za kitaalamu na Mimi mwenzako ni wa D mbili hapo ndo nmepata taabu kuelewa.

Nieleze tu kwamba chini niende futi ngapi na upana uwe futi ngapi Kwa ngapi hapo ndo ntaelewa Kwa uzuri zaidi mkuu. Asante
 
Ok sawa, kama unataka kuchimba shimo la duara chimba shimo la upana wa mita 2 na kina cha futi 8

Kama unataka kuchimba shimo la mstatili, chimba shimo la urefu wa futi 8, upana wa futi 4 na kina cha futi 8 au kama ardhi yako ni ngumu kuchimba kwenda chini basi chimba shimo la urefu wa futi 10, upana wa futi 6 na kina cha futi 5 (ambapo hapa utakuwa na shimo la kuingiza lita 8000)
 
Barikiwa Sana mkuu Kwa maelezo mazuri namna hii.
 
Back
Top Bottom