Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI KIKONGO, KIBAHA VIJIJINI-PWANI
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Mhe. Hawa Mchafu akikagua Miundombinu ya Shule ya Sekondari Kikongo iliyopo Wilaya ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani ili kujiridhisha na Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2020-2025
"Nimejionea hali ya Ujenzi na nimefurahishwa sana kuona fedha alizotoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Kikongo, Kibaha Vijijini-Pwani zimefanya kazi vizuri" - Amesema Mhe. Hawa Mchafu (Mb)
Mhe. Hawa Mchafu
Mbunge Viti Maalum CCM-Pwani
Tarehe 13 Januari 2023
HAKUNA KITAKACHOSIMAMA NDANI YA MKOA WA PWANI