Ujenzi wa SLAB ya ghorofa

Marine plywood ina ukubwa wa 1.2*2.4 meters na unene wa 16mm. Mara ya mwisho nimeulizia(miezi mi3 iliyopita) minimum price ilikuwa 75,000
 
Last edited by a moderator:
Marine plywood ina ukubwa wa 1.2*2.4 meters na unene wa 16mm. Mara ya mwisho nimeulizia(miezi mi3 iliyopita) minimum price ilikuwa 75,000

Mkuu, unafahamu reliable supplier wa hizi boards...
 
Yapo material baadhi yanaweza kutumika zaidi ya mara moja hasa yenye asili ya plastic au chuma lakin lwa mbao kwenye kazi za zege ukizingatia ili zege iwe imara inahitaji maji na mbao na maji lazima iathirike. Haitatoa kitu kinachovutia kwa maana ya finishing surface. Kwa hiyo ni bora kugharamikia material kuliko kuja kuingia gharama ya kuremba baada ya ujenzi.
 
Dawa Ya Buguruni ni kwenda na futi yako we na msaidizi, mnapima wenyewe wao wanasimamia tu maana futi zao wanazikata katikati
Hivi wale jamaa Wakala wa vipimo (WMA) sio kazi yao hii? au ni mamlaka gani inayohusika kuangalia haki za wateja wanaodhulumiwa kwa vipimo kama hivyo? Maana malalamiko ya Buguruni yako muda mrefu sasa na sioni hatua zozote zikichukuliwa juu yao
 
Wakuu mimi nimejenga kigorofa cha square meter 144, Juu 3 bedroom (all masters ) sebule ndogo na Patio. Marine sheet peke yake zimekula million 6, ukiweka na mbao unaweza lia machozi. Mirunda nilinunua 800 hiyo ni 2 million, sasa mbao za 13000 ndio sikumbuki maana niliacha na kuhesabu kabisa. In short nyumba ya 144 sqrm andaa sio chini ya milion 27 kupiga slab tuu.

Msingi nadhani sio bei kali kama Slab.

Ukitaka kukodisha metal sheet za formwork kutoka kwa jamaa wa mtaani wale wanakupa kwa 4 weeks wanakucharge kama 30,000 kwa sqrm, hawakupi frame za beam, hivyo bado utaingia 2 au 3 million gharama, vilevile canopy yake sio kama ya mbao.

Misumari inayolika unaweza kulia machozi. Ujenzi wetu Tanzania bado ni wa karne ya 7.
 
Mkuu ZeMarcopolo tupe na maujanja ya kupunguza gharama za ujezi wa msingi wa ghorofa, hasa kwa hizi ghorofa moja tu za familia
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,

Kwenye msingi ujanja pekee ni kusimamia closely iili usiibiwe materials.

Zaidi ya hapo hakuna ujanja mwingine labda kwenye bei za ufundi.

Mkubwa ghorofa lako ushamaliza? Je msingi wa ghorofa wa sqm 64 kuweka starter 1.5m deep na slab ya sqm 64 inaweza cost kiasi gani? Kwa experience yako.
 
Mkubwa ghorofa lako ushamaliza? Je msingi wa ghorofa wa sqm 64 kuweka starter 1.5m deep na slab ya sqm 64 inaweza cost kiasi gani? Kwa experience yako.

Mkuu maisha ni kujikongoja,

Ingawakuna factors nyingi zinazoamua bei lakini on average it should be 7-9 mil. Kadiri sq. m. zinavyokuwa chache ndivyo jinsi unit price inavyoongezeka.

Kama nimekuelewa unataka kujenga nyumba ya chini lakini master bedroom iwe ghorofani.

Kama lengo lako ni kupunguza gharama mimi ningekushauri ujipige tu uweke kitu full. Mimi wakati fulani nilikuwa na idea hiyo, lakini nikafikiria dogo akikua atanimind, halafu family inakuwa detarched in some ways. Preferences ziko nyingi, I am just giving my perspective.
 

yap master iwe juu,okay thanx kwa ushauri ngoja nizichange change kuwe na hata vyumba vi2 juu,ukishazoea kukaa ghorofani kuishi nyumba za chini mtihani.
 

Tatizo upatikananji wake hizo mbao after ujenzi mkuu. Zinavunjwaga vujwaga hovyo ndo maana.
 
Kama unajipanga unaweza kujenga, lakini kujipanga ndio mambo yote. Usijenge gorofa kimasikini, litashuka kabla ya weekend.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…