Ujenzi wa SLAB ya ghorofa


Marine board nyingi ni around 8*4 in size.bei zake zinarange from 50,000 to 65,000 kutokana na unene.Namfahamu jamaa anayefanya biashara ya kukodisha Scaffolds(metal) kwa ajili ya ujenzi wa magorofa.am sure these can be reused more efficiently for those looking to venture into this type of business as they are much more flexible than wood.
 

Mkuu,
Asante kwa taarifa.
Je, jamaa anayekodisha bei zake zikoje?
 
Mkuu,
Asante kwa taarifa.
Je, jamaa anayekodisha bei zake zikoje?

Mimi niliwasiliana na jamaa mmoja anaitwa Mushi yupo mitaa ya Mbweni, lakini sasa huyu jamaa price yake ni 30,000 kwa Sqrm lakini kumbuka lazima utengeneze Beam zako mwenyewe na hapo lazima Marine kama 20 zilike. Kisha yeye atakupa hizo sheet metal ambazo utakaa nazo only for 4 weeks. 30,000 sqrm ni pamoja na labor. Hii nyumba ya 144 sqrm ilikuja 5 million ukijumlisha na marine nikaona bora ninunue marine zote nifanye foarmwork mwenyewe. It was expensive.
 

Huyo jamaa bei yake ni kubwa mno. Elfu 30 kwa square metre ni TOO MUCH. This is more expensive than kununua mbao au marine boards!!!
 
Huyo jamaa bei yake ni kubwa mno. Elfu 30 kwa square metre ni TOO MUCH. This is more expensive than kununua mbao au marine boards!!!

ndio maana nikanunua Marine mwenyewe. Formwork ilinigharimu kama million 8 hivi. Hapa kuna Marine kama 120, Mirunda nilinunua 800, misumari niliacha kuhesabu maana. Mbao zililika za kutosha zababu ya kutengeneza canopy sijui ngazi ya kumwaga jamvi na nyingine za kushikilia canopy nje. Plus 800,000 labor ya formwork.
 

Ila mkuu kwa nyuma ya sq. m 144 mirunda 800 huyo fundi wako aliiweka wapi?

Mimi nakushauri kama bado unajenga na huyo fundi kuwa karibu sana na materials anavyotumia. Usimpe pesa akanunue au kumuwekea materials ukaondoka. Nyumba ya sq. m 144 haitakiwi kuzidi mirunda 400.
 

Mkuu kweli milunda mingi ilibaki, nilikwenda shamba nikanunua lori moja na hiyo ilikuwa quote ya fundi. Kweli kabisa mafundi ni wezi. Kilio changu kilikuwa kwenye mbao hapo nimenunua nyingi mpaka basi. Ikafika muda nikataka liishe nipumzike.
 
ZeMarcopolo,

Nataka fundi mkali wa kunipaulia kaka. Nataka kuchukua likizo kabisa kama una contact zozote please share kaka.
 

Kama hujui kinachoongelewa bora unyamaze tu!
 
ZeMarcopolo,

Nataka fundi mkali wa kunipaulia kaka. Nataka kuchukua likizo kabisa kama una contact zozote please share kaka.

Ee bwana kuna fundi mmoja yuko fresh ila sijawahi kufanya nae kazi. Naweza kukuconnect naye. Ila kuna paa moja nimeiona kitaa ni kali sana kwanza kwa sababu ya materials alizotumia, lakini pili kwa ufundi wa aliyepaua. Kama uko Dar naweza kukuelekea ukaione nyumba yenyewe ninayosema iko sehemu rahisi kufika.
Yule fundi ndio nitamtafuta in my next project.
Unaweza kupeleleza ukapata contact zake, kama uko interested naweza kukupa njia za "kipelelezi" za kumpata.
 
Kama upo Dar naweza kukuunganisha na fundi wa kupaua mkali sanaa, ukitaka wa gypsum na fundi rangi mzuri pia

Mkuu, kama vipi weka jina na contacts ya huyo fundi hapa. Utamsaidia fundi kupata wateja pamoja na wadau kupata fundi.
 
Dr ZeMarcopolo leo ninakupigia salute. Hakika tuweke SIHASA pembeni pia wakati mwingine tuje na issu critical kama hizi. Umenifundisha kitu hapa. Asante sana.
 
Dr ZeMarcopolo leo ninakupigia salute. Hakika tuweke SIHASA pembeni pia wakati mwingine tuje na issu critical kama hizi. Umenifundisha kitu hapa. Asante sana.

Wakuu nani amepiga canopy ya juu? hii kitu ni balaa lakini inapendezesha sana nyumba.
 
Hello wakuu, kuna rafiki yangu ameezua slab yake ya ghorofa, kwa hiyo ana mirunda 500 na kila mmoja anauza 1300, marin boards 18mm 35 @ 30000 na mbao 4X2 zipo 100 kwa 3500, zote zimetumika mara moja, na site ipo tegeta salasala kwa anayependa ni PM nikuunganishe kama wataka kuziona na kununua
 
Marine plywood ina ukubwa wa 1.2*2.4 meters na unene wa 16mm. Mara ya mwisho nimeulizia(miezi mi3 iliyopita) minimum price ilikuwa 75,000

Sawa mkuu hiyo ndo bei ila ukitka zaidi ya 50pcs pale kwa warusi Tabata mpaka kwa 60,000 unapata. Mimi nimenunua hapo one month ago 70pcs kwa bei hiyo.
 

Mkuu hapo umesema kweli mimi nimejenga ya ukubwa kama wa kwako hiyo slab mkuunilifikiri nimeibiwa lakini sasa naamini ni kweli mbao mpaka nilianganyikiwa Nondo ndio balaa tena engineer wangu akaniambia anataka nondo za nje du ilikuwa si mchezo. So ni vizuri kama kuna namna ya kupunguza gharama hizi ingekuwa vizuri
 

Nyumba yakawaida ibadlishe kuwa ghorofa kwa kubdilisha paa?? are you serious? msingi wa ghorofa unaujua kweli mkuu wangu..
 
Natafuta marine boards za kukodisha lakini ziwe zimetumika sio zaidi mara moja.

Mtafute beaf tanzania , anazo za chuma anakodisha....

Otherwise kwanini usijengee structural insulated panels kwa upande wa ghorofa uliobaki uokoe gharama za ujenzi ?
No concrete slab, no conrete columns and no formwork,.
 
Last edited by a moderator:
Acha kuingilia kazi za watu. Kwenye Civil Engineering, kuna somo topic inafundishwa isemayo "Structure/Jengo ni lazima iwe Imara, Ipendeze, Ifanye kazi inayotakiwa ifanye, Idumu na Iwe Economical"

Tunaposema Economical (sijui kwa Kiswahili tusemaje?) tunamaanisha hadi kwenye ujenzi pia. Siku zote tunasema unapojenga basi tumia materials ya ujenzi yaliyo karibu. Kwa nini kutoa Cement Mbeya hadi Bukoba na wakati huohuo, Mwanza kunaweza kupatikana matofali ya kuchoma au mawe? Wewe unang'ang'ania matofali ya Cement?

Wakati mwingine ni kweli kabisa ukiagiza kampuni ya ujenzi wakufanyie kazi, inaweza kuwa bei rahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…