Wana JF,
Lengo la thread hii ni kupeana maarifa ya jinsi ya kupunguza gharama za ujenzi wa SLAB ya ghorofa.
Gharama ya ujenzi wa slab "inatia uchungu" kwa vile inahusisha mahitaji ambayo ni disposable lakini ni ya gharama kubwa. Mahitaji hayo ni support ya kubeba zege (mbao, plywood au iron sheet), mirunda, vyuma na misumali. Gharama hizi zinakadiriwa kuwa asilimia 20 ya materials za slab nzima. Hii si gharam ndogo. Kwa ghorofa moja yenye slab ya mita za mraba 140 inahitajika kama shilingi milioni 3.5 - 4.
Kuhusu Mbao, plywood, iron sheet na mirunda kuna haja ya kubuni mbinu mbalimbali za kupunguza gharama kama ifuatavyo:
1. Tafuta jirani aliye kwenye hatua inayofanana na wewe kwenye ujenzi na ukubaliane naye akuuzie materials zake akimaliza au wewe umuuzie ukimaliza.
2. Ulizia iwapo kuna wakodishaji wa vifaa hivyo. Hakikisha unakubaliana bei na jinsi ya kufidia mbao na mirunda itakayokatwa.
3. Nunua materials mpya na uanzishe biashara ya kuzikodisha baada ya kutumia.
4. Fanya urafiki na watu wenye makampuni ya ujenzi. You can even get these materials FOR FREE!!!
5. Anza kukusanya materials kidogokidogo toka kwa wajenzi wasiohitaji. Kama jirani yako anataka kutupa mrunda muombe akupe, akiweka mbao jalalani chukua. Kama kichaa vile lakini inaweza kusave you a great deal of money.
6. Kuwa mkali kwa fundi asitupe na kupoteza vipisi ambavyo vingeweza kufanya kazi na more importantly "asikosee mahesabu".
7. Nunua vifaa unavyohitaji kwa wingi kwa pamoja katika maduka ya jumla. Ukiamua kufanya hivyo hakikisha una utaratibu salama wa kuvihifadhi.
Njia hizi zinaweza kupunguza gharama za materials hizi "disposable" kwa asilimia 50-90!
Katika thread hii wale wenye biashara za kukodishe mbao, plywood, iron sheer, mirunda, vyumba etc tafadhali wekeni terms za biashara zenu ili kuwapa members picha halisi ya jinsi wanavyoweza kupunguza gharama za ujenzi wa slab.
Iwapo umejenga slab na una materials zilizobaki. Tumia thread hii kuingia deal na wadau ili uwauzie au kuwakodisha.
Kwenye ujenzi tunasema "every shilling is GOOD". Save shilling yako kwa kuuza mbao ambazo zingeliwa na mchwa.