Ujenzi wa SLAB ya ghorofa

Ujenzi wa SLAB ya ghorofa

ZeMarcopolo

Platinum Member
Joined
May 11, 2008
Posts
14,040
Reaction score
7,303
Wana JF,

Lengo la thread hii ni kupeana maarifa ya jinsi ya kupunguza gharama za ujenzi wa SLAB ya ghorofa.

Gharama ya ujenzi wa slab "inatia uchungu" kwa vile inahusisha mahitaji ambayo ni disposable lakini ni ya gharama kubwa. Mahitaji hayo ni support ya kubeba zege (mbao, plywood au iron sheet), mirunda, vyuma na misumali. Gharama hizi zinakadiriwa kuwa asilimia 20 ya materials za slab nzima. Hii si gharam ndogo. Kwa ghorofa moja yenye slab ya mita za mraba 140 inahitajika kama shilingi milioni 3.5 - 4.

Kuhusu Mbao, plywood, iron sheet na mirunda kuna haja ya kubuni mbinu mbalimbali za kupunguza gharama kama ifuatavyo:

1. Tafuta jirani aliye kwenye hatua inayofanana na wewe kwenye ujenzi na ukubaliane naye akuuzie materials zake akimaliza au wewe umuuzie ukimaliza.

2. Ulizia iwapo kuna wakodishaji wa vifaa hivyo. Hakikisha unakubaliana bei na jinsi ya kufidia mbao na mirunda itakayokatwa.

3. Nunua materials mpya na uanzishe biashara ya kuzikodisha baada ya kutumia.

4. Fanya urafiki na watu wenye makampuni ya ujenzi. You can even get these materials FOR FREE!!!

5. Anza kukusanya materials kidogokidogo toka kwa wajenzi wasiohitaji. Kama jirani yako anataka kutupa mrunda muombe akupe, akiweka mbao jalalani chukua. Kama kichaa vile lakini inaweza kusave you a great deal of money.

6. Kuwa mkali kwa fundi asitupe na kupoteza vipisi ambavyo vingeweza kufanya kazi na more importantly "asikosee mahesabu".

7. Nunua vifaa unavyohitaji kwa wingi kwa pamoja katika maduka ya jumla. Ukiamua kufanya hivyo hakikisha una utaratibu salama wa kuvihifadhi.

Njia hizi zinaweza kupunguza gharama za materials hizi "disposable" kwa asilimia 50-90!

Katika thread hii wale wenye biashara za kukodishe mbao, plywood, iron sheer, mirunda, vyumba etc tafadhali wekeni terms za biashara zenu ili kuwapa members picha halisi ya jinsi wanavyoweza kupunguza gharama za ujenzi wa slab.

Iwapo umejenga slab na una materials zilizobaki. Tumia thread hii kuingia deal na wadau ili uwauzie au kuwakodisha.

Kwenye ujenzi tunasema "every shilling is GOOD". Save shilling yako kwa kuuza mbao ambazo zingeliwa na mchwa.
 
Kwa hakika mahitaji ya formwork na falsework (hizo mbao, mirunda uliyotaja nk) ni moja ya gharama kubwa katika ujenzi wa nyumba za kawaida. Ingesaidia kiasi wakitokea wajasiriamali watakokusanya mbao used sehemu mbalimbali na kuwauzia wajenzi wapya kwa bei nafuu.
 
Idea nzuri sana umetoa. Hapa tunaona kuwa Bongo business opportunities bado ni nyingi sana.

Wadau changamkieni idea ya Mwasyoke hii, ameitoa bila patent kwa nia njema...
 
hayo magharama ya kwenye slab na msingi ndo pananikatishaga tamaa kabisa ninapofikiria kujenga kighorofa cha kishkaji cha kuishi na familia yangu
 
Idea nzuri sana umetoa. Hapa tunaona kuwa Bongo business opportunities bado ni nyingi sana.

Wadau changamkieni idea ya Mwasyoke hii, ameitoa bila patent kwa nia njema...

Ukitaka kujenga hakikisha unayo pesa sio kuleta ubangaizaji ndio mwishowe ni kuuwana; vifaa chakavu vya ujenzi haviwezi kuwa na strength ileile kama vikiwa vipya sasa unapovifanyia biashara ya kuvizungusha na kuvizungusha gorofa hadi gorofa mwishowe ni misiba na kuishia jela. Kama huna pesa kapange usilete biashara kichaa kwenye uhai wa wenzio
 
You never know ndugu yangu. Kesho unaweza kuamka na wewe unazo.

Follow this space closely.

Lakini hapa sio kwa wenye nazo, hapa ni kwa wale wanaotaka kusave. Wenye nazo wanaajiri kampuni liwafanyie kazi, wao wanaenda kuchukua funguo tu.

Mkuu, kama umeshajenga ya chini basi nenda mdogomdogo mpaka umalize ile kitu roho napenda. Hatua kwa hatua mpaka utafika. Hapa ndio tunabadilishana mawazo ya kufanikisha ndoto...
 
Ukitaka kujenga hakikisha unayo pesa sio kuleta ubangaizaji ndio mwishowe ni kuuwana; vifaa chakavu vya ujenzi haviwezi kuwa na strength ileile kama vikiwa vipya sasa unapovifanyia biashara ya kuvizungusha na kuvizungusha gorofa hadi gorofa mwishowe ni misiba na kuishia jela. Kama huna pesa kapange usilete biashara kichaa kwenye uhai wa wenzio

Mkuu, jaribu kusoma vizuri utaelewa tunachozungumza.
 
Jamani tukae tukijua kuwa mbao si re usable materia hasa kwenye ujenzi.....kwani uimara wa structure yako ni pamoja na uimara wa form works ulizotumia.......
 
Mkuu,
Naomba utuonyeshe uhusiano kati ya uimara wa structure na kutumia mbao zilizotumika in a scientific manner.
Asante.
 
MODs, naomba thread hii msiiunganishe na nyingine.

Lengo la thread hii ni kupeana maarifa ya jinsi ya kupunguza gharama za ujenzi wa SLAB ya ghorofa.

Gharama ya ujenzi wa slab "inatia uchungu" kwa vile inahusisha mahitaji ambayo ni disposable lakini ni ya gharama kubwa. Mahitaji hayo ni support ya kubeba zege (mbao, plywood au iron sheet), mirunda, vyuma na misumali. Gharama hizi zinakadiriwa kuwa asilimia 20 ya materials za slab nzima. Hii si gharam ndogo. Kwa ghorofa moja yenye slab ya mita za mraba 140 inahitajika kama shilingi milioni 3.5 - 4.

Kuhusu Mbao, plywood, iron sheet na mirunda kuna haja ya kubuni mbinu mbalimbali za kupunguza gharama kama ifuatavyo:

1. Tafuta jirani aliye kwenye hatua inayofanana na wewe kwenye ujenzi na ukubaliane naye akuuzie materials zake akimaliza au wewe umuuzie ukimaliza.

2. Ulizia iwapo kuna wakodishaji wa vifaa hivyo. Hakikisha unakubaliana bei na jinsi ya kufidia mbao na mirunda itakayokatwa.

3. Nunua materials mpya na uanzishe biashara ya kuzikodisha baada ya kutumia.

4. Fanya urafiki na watu wenye makampuni ya ujenzi. You can even get these materials FOR FREE!!!

5. Anza kukusanya materials kidogokidogo toka kwa wajenzi wasiohitaji. Kama jirani yako anataka kutupa mrunda muombe akupe, akiweka mbao jalalani chukua. Kama kichaa vile lakini inaweza kusave you a great deal of money.

6. Kuwa mkali kwa fundi asitupe na kupoteza vipisi ambavyo vingeweza kufanya kazi na more importantly "asikosee mahesabu".

7. Nunua vifaa unavyohitaji kwa wingi kwa pamoja katika maduka ya jumla. Ukiamua kufanya hivyo hakikisha una utaratibu salama wa kuvihifadhi.

Njia hizi zinaweza kupunguza gharama za materials hizi "disposable" kwa asilimia 50-90!

Katika thread hii wale wenye biashara za kukodishe mbao, plywood, iron sheer, mirunda, vyumba etc tafadhali wekeni terms za biashara zenu ili kuwapa members picha halisi ya jinsi wanavyoweza kupunguza gharama za ujenzi wa slab.

Iwapo umejenga slab na una materials zilizobaki. Tumia thread hii kuingia deal na wadau ili uwauzie au kuwakodisha. Kwenye ujenzi tunasema "every shilling is GOOD". Save shilling yako kwa kuuza mbao ambazo zingeliwa na mchwa.

Kabla sijaanzakijenga nyumba ninayo ishi sasa, nilitamanis ana kujenga kagorofa ka kishkaji lqkini ardhi niliyo nunua nikaona haitaweza kumudu gorofa. Nikaanza ujenzi wa kawaida, kama mnavyo jua msingi wa nyumba wa kawaida hauendi chini sana kama wa gorofa, baada ya kupauwa na finishing nyingine ndogo ndogo nikaamua kuchimba shimo la choo.
Siku wanaanza kuchimba sikuwa site jioni nikapigiwa simu kuwa kazi ngumu sana kutokana na mapatano yalivyokuwa, kesho yake nikaenda site nikakuta wamesha chimba kama futi tatu hivi lakini kando kulikuwa na na mawe makubwa wakasema wametoa ndani ya shimo. Ardhi ilikuwa ni nzuri yenye kuweza kubeba hata gorofa kumi. Nilijisikia vibaya na nilikuwa nishachelewa.
Baada ya miaka 6 nikanijia wazo la kubomia hii nyumba nijenge house of my dream lakini nikiangalia gharama nilizotumia mpaka sasa nashindwa nini cha kufanya.
 
Mara nyingi washauri wa masuala ya ujenzi nchini hawako scientific. Wanatumia zaidi hisia kuliko evidence.

Hao waliokwambia udongo hauwezi kubeba ghorofa ni obvious kuwa walikudanganya kwa sababu ghorofa moja la matumizi ya residential halina tofauti kubwa na nyumba ya chini. Kwahiyo kama eneo halifai kwa ghorofa moja residential basi hata nyumba ya chini lisingefaa kujenga.
Pole, lakini zipo njia za kubadilisha nyumba ya chini kuwa ghorofa. Njia hizo zinaweza kuhitaji mabadiliko ya paa tu na si kubomoa nyumba nzima.
 
Nimemaliza kumwaga zege. Nina mirunda 700 (bei @ 1,500) Marin Board 65 (bei @ 40,000) Mpya zimebaki 5 ambazo naziuza kwa (@ tshs 50,000) na Mbao za 4x2, 6x2 na 10x1 nyingi). zote zimetumika mara moja na ziko katika hali nzuri. kwa anayehitaji zitakuwa available baada ya wiki 2 kuanzia leo. unaweza anza fanya booking mapema na ukajiandaa kuzichukua. ni PM au piga 0713 60 28 00

Mkuu kibiashara

Je marine board moja ina size gani? Bei yake ya sokoni (zikiwa mpya) ni sh. ngapi?
Taarifa hizi zitawasaidia wadau kujua wanahitaji boards ngapi na kiasi cha pesa wanachoweza kusave kwa kununua toka kwako.

Kwa mirunda, sehemu nyingi za rejareja wanauza around sh. 2,500.

Je, iwapo mdau anataka kukodisha tu, unakubaliana na option hiyo?

Asante...
 
Last edited by a moderator:
Jamani tukae tukijua kuwa mbao si re usable materia hasa kwenye ujenzi.....kwani uimara wa structure yako ni pamoja na uimara wa form works ulizotumia.......

Iko hivi kaka mbao inapoteza strenth kila inapotumika so the more inatumika ndivyo strenth inavyoisha na kwenye structure ili ikae ni lazima kile kilichoshikilia kiwe na strenth ya kuweza kuhimili forces.zaidi kama ni slab itasag kama unatumia mbao zilizotumika mara nyingi kuna kitu kinaitwa bending moment. Inashauriwa mbao isitumike zaidi ya mara tatu kama sikosei. Mwisho mi sio eng ni architect so majibu sahihi ni yale atakayoshauri eng thanks
 
Kwahiyo tatizo sio mbao kutumika ila ni mbao kupoteza strength. Lets be careful with choice of words.

Mbao kutumia na mbao kupoteza strength ni vitu viwili tofauti. Unaweza usiitumie mbao lakini ukaiweka nje ikanyeshewa na mvua halafu ikawa haifai kwa kazi ya ujenzi, mwingine anaweza kuitumia mbao mara moja akaitunza vizuri na ikafaa kwa ujenzi baadae.

Hapo cha msingi ni fundi kuchagua mbao anazoona ziko katika hali inayofaa kwa kazi, lakini si sahihi kupiga mstari mwekundu kuwa mbao zilizotumika hazifai.
 
Iko hivi kaka mbao inapoteza strenth kila inapotumika so the more inatumika ndivyo strenth inavyoisha na kwenye structure ili ikae ni lazima kile kilichoshikilia kiwe na strenth ya kuweza kuhimili forces.zaidi kama ni slab itasag kama unatumia mbao zilizotumika mara nyingi kuna kitu kinaitwa bending moment. Inashauriwa mbao isitumike zaidi ya mara tatu kama sikosei. Mwisho mi sio eng ni architect so majibu sahihi ni yale atakayoshauri eng thanks

Heeee kiongozi ninavyoona ni kama kuna kitu unaelewa afu unataka kuona kama wengine wanajua. Kikubwa ni matumizi kwa sababu kwenye matunzo sitegemei utatumia mbao ya mwaka 2009 now labda treated.....vitu vingine tusifanye siasa na kuleta ujuaji....kimsingi materia zinazotakiwa site ni muhimu kuwa tested sema kwa.bongo ni kama matusi kumwambia mtu atest strengh za material....any way kwa ushauri wa bure mbao ikitumika mara tatu anza kuwa.makini nayo sana kwa sababu za kiusalama zaidi material yoyote hata kama haijatumika sehemu ni muhimu kuwa tested.
 
Back
Top Bottom