Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 140
- 181
Eneo la mada
Miundombinu ya Usalama barabarani.
Mada:
UJENZI WA VITUO VYA DHARURA BARARANI ILI KUTOA HUDUMA KWA MAJERUHI WA AJALI ITASAIDIA KUPUNGUZA IDADI YA VIFO HAPA NCHINI.
Uwepo wa vituo vya dharura barabarani ni msaada mkubwa wa kuokoa maisha ya binadamu wenzetu pale inapotokea ajali za barabarani, Waathirika wengi wa ajali za barabarani upoteza maisha, ikiwa ni pamoja na kupatiwa huduma ya kwanza na mashuhuda wa ajali isiyo kidhi vigezo kutokana na ukosefu wa ujuzi wa kutosha, ikiwa ni sambamba na kuvuja damu nyingi kwa majeruhi, pamoja na maghari kuwaka moto na kubanwa na vyuma ndani ya gari.
Ukosefu wa huduma muhimu kwa majeruhi, uongeza tatizo kwa waliojeruhiwa na ajali, Mfano; Mtu aliyevunjika mkono au mguu kutokana na ajali ipo namna ya kumpa huduma ya kwanza, anapobebwa kienyeji basi tatizo uongezeka zaidi, Pia kutokuwepo na weledi katika kuwahudumia wahanga wa ajali upelekea kuenea kwa maambukizi mengine kama Ukimwi ( HIV), Homa ya ini (Hepatitis), Magonjwa ya ngozi, (Psoriasis), Ugonjwa wa macho (Conjuctivitis na Uveitis), n.k.
Dk. Ndugulile waliwai ksema, “Eneo la uokoaji bado tuna tatizo, tunawapoteza Watanzania wengi kipindi cha uokoaji kwa sababu ya uelewa duni, suala si kumkimbiza hospitali bali ni kum-stabilize palepale kwenye eneo la tukio kabla hajapelekwa hospital” Kwa mantiki hiyo uokoaji na usaidizi wa majeruhi wa ajali za barabarani hapa nchini ni tatizo sugu, ambalo sasa linahitaji ufumbuzi wa haraka sana iwezekanavyo.
Mathalani mwaka 2018 mwezi wa kumi eneo la Manyoni, nilishuhudia ajali ambayo watu sita walipoteza maisha baada ya kukosa huduma muhimu kutoka kwa wataalam hii ni baada ya kuvuja damu nyingi baada ya kutokea ajali, laiti ukanda huo ungekuwa na kituo cha dharura barabarani nina amini maisha ya wenzetu yangeweza kuokolewa.
Ipo wazi kitakwimu kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayoandamwa na wimbi la ajali za barabarani hapa barani Afrika, hivyo ajali za barabarani kwa Tanzania ni janga la kitaifa, Mbali na kuwa janga lakini bado ajali uchangia katika kuzalisha umaskini ndani ya nchi yetu.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ajali za barabarani hapa nchini ni sababu kuu ya vifo vya Watoto wenye umri kati ya miaka 5 hadi 14, sambamba na vijana wa miaka 15-29, hii ni nguvu kazi ya taifa na tegemeo kwa uchumi wa nchi inayoishia kwenye ajali za barabarani.
Serikali na taasisi zake kwa maana ya jeshi la polisi, baraza la taifa la usalama barabarani, Bunge na Wizara ya Afya, mambo ya ndani, na kamati za usalama barani mkoa na wadau wengine bado wapo nyuma kwenye uwekezaji muhimu ndani ya eneo hili, Je mamlaka hawaoni kuwa hili ni tatizo ambalo pengine linahitaji kupewa kipaumbele kama vipaumbe vingine?
Wakati ni huu sasa mamlaka husika kuwekeza kwenye vituo vya dharura barabarani ili kunusuru uhai wetu maana hatujui nani anaweza kuwa muhanga wa ajali, si kiongozi wala raia wa kawaida, anayeweza kujua ni lini atakumbwa na tatizo hili la ajali.
Ushauri wa andiko hili kwa serikali ni kutenga bajeti ya kutosha kwa kipindi cha miaka 15 hadi 25 ijayo kuhakikisha nchi nzima inakuwa na mtandao wa vituo vya kutoa huduma ya dharura kwa majeruhi wa ajali za barabarani ili kupunguza vifo vitokanavyo na ajali ambazo kwa mazingira ya Kitanzania ni ngumu kukwepa ajali hizo.
Pengine kwa nini ni ngumu, sababu ni pamoja na uwepo wa rushwa, sheria mbovu za usalama barabarani, miundombinu ya barabara isiyo rafiki, nidhamu mbovu kwa madereva, ulevi na matumizi ya simu wakati wa uendeshaji wa chombo cha moto.
Serikali itambue sasa ajali za barabarani kama janga la kitaifa ambalo linapoteza nguvu kazi na kuleta umaskini kwa Watanzania, aidha serikali inatumia gharama kubwa kuwahudumia majeruhi wa ajali za barabarani.
Hivyo Ushauri wa andiko hili ni serikali itenge bajeti maalumu kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya dharura ambavyo vitakuwa na huduma za kisasa katika kuhudumia majeruhi baada ya kutokea ajali ili kuweza kunusuru maisha yao, ni jambo la utashi ambalo lipo ndani ya uwezo wa serikali kibajeti.
Aidha Ushauri wa andiko hili kwa mamlaka ni kujenga vituo kwenye maeneo maalumu ndani ya mipaka ya Barabara kuu vituo vikiwa na magari, wahudumu na vifaa vya kisasa ili kuweza kukabiliana na tatizo pale inapotokea ajali ya barabarani.
Uwepo wa vituo ndani ya eneo la Barabara kuu ni njia muhimu ya kusaidia majeruhi na kuokoa wahanga wa ajali, kuwa na magari ya zimamoto yenye kuweza kutoa huduma ya kwanza pindi ajali itokeapo ni jambo moja na muhimu, lakini kuwa na vituo maalum ni jambo jingine muhimu zaidi kusaidia kufika kwa wakati na kutoa huduma kadri inavyohitajika.
Serikali imeweza kujenga vituo vingi vya ukaguzi “barriers” kwenye maeneo mengi hapa nchini, pia inaweza kufanikisha ili la ujenzi wa vituo vya dharura kwa kila ilipo “barriers” ili kuweza kukabiliana na tatizo kwa haraka sana.
Kwa mantiki hiyo serikali itoe kipaumbele kwenye eneo hili, itambue umuhimu wake na hivyo itenge bajeti mara moja ya ujenzi wa vituo vya dharura ili kusaidia pale tatizo linapotokea kwa ukaribu zaidi, kuliko kusubiri huduma ambayo inaweza kufika baada ya masaa sita hadi saba bila kuwa na tija yoyote kwa majeruhi wa ajali.

Upvote
4