Ujenzi wamuomba JK amdhibiti Magufuli

Ujenzi wamuomba JK amdhibiti Magufuli

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Ujenzi wamuomba JK amdhibiti Magufuli



Na Mwandishi Wetu
Majira

HALI bado si shwari ndani ya Wizara ya Ujenzi licha ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi wa juu wa wizara hiyo mara baada ya uchaguzi
mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Wizara ya hiyo imekuwa katika mvutano na malumbano ya muda mrefu kiutendaji huku baadhi ya wafanyakazi wakilalamikia ukiukwaji taratibu unaofanywa na baadhi ya vigogo wa wizarani hapo.

Katika kile kinachoonekana kuwa ni mwendelezo wa mivutano hiyo, wafanyakazi wa wizara hiyo, wamemwomba Rais Jakaya Kikwete kutumia vyombo vyake kuzuia kile walichodai ubabe unaoendelezwa na waziri wa wizara hiyo, Dkt. John Magufuli anayedaiwa kuendelea kuipotosha serikali na umma kuhusu masuala mbalimbali ndani ya wizara hiyo.

Vyanzo vyetu kutoka ndani ya wizara hiyo vimeeleza kuwa kutokana na mwendelezo wa kile kinachoelezwa jeuri ya Dkt. Magufuli, baadhi ya wafanyakazi hao wamepoteza imani na serikali jambo linalochangia kushusha ufanisi wa wizara hiyo.

“Tunashangaa kuona rais wetu mpendwa anafanyiwa usanii hapa wizarani kwetu. Morali ya kazi imeshuka sana kutokana na migongano ya mambo mengi yanayoendelea. Inasikitisha wakuu wa wizara kuweka watu dhaifu kwenye nafasi nyeti za utendaji kwa maslahi binafsi, kwa mfano Mkurugenzi wa Wakala wa Umeme (TAMESA) ameteuliwa bila kushirikisha ngazi nyingine za wizara.

“Kikubwa na kushangaza zaidi, hadi leo wakurugenzi wa wizara wanakaimu nafasi zao huku wakifanya kazi kubwa za wizara, wengine wanashindwa kujibu hoja nzito wakihofia kuharibu nafasi wanazokaimu, sasa hapa tunawasaidia wananchi au tunacheza ?” Kilieleza na kuhoji chanzo chetu ndani ya wizara hiyo.

Ofisa mwingine wa ngazi ya juu wizarani hapo ameliambia Majira kwamba Rais Kikwete anapaswa kutupia macho Wizara ya Ujenzi kwa kutumia vyombo vyake kwani kinachoendelea ni kulindana bila kujali maslahi ya nchi.

“Mheshimiwa Rais kama anataka ahadi zake zitekelezeke zoezi la uteuzi wa wakurugenzi wa wizara na taasisi zake upitie kwake na si vinginevyo kwa maslahi ya nchi na umma,”alisema ofisa huyo na kueleza kuwa anaielewa vyema wizara hiyo kwani amefanya kazi kwa zaidi ya miaka kumi

Ofisa huyo ambaye kitaaluma ni mhandisi, alitoa mfano wa kusuasua kwa uteuzi wa nafasi ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS jambo alilosema linaathiri kwa kiasi kikubwa utendaji wa wizara hiyo.

“Kutokana na unyeti wa TANROADS, tunamuomba Rais kuingilia kati mchakato wa kumpata mtendaji mpya mwenye uwezo na sifa za kupambana na ufisadi badala ya kumuingiza mtu ambaye ataonekana kuja kulinda maslahi ya waliomtangulia na watuhumiwa wengine wa ufisadi,” alidai.

Ofisa huyo anasema kwa sasa kutokana na nguvu kubwa ya mafisadi ndani ya wizara, tayari watu wenye uwezo mkubwa wameenguliwa kupisha mtu atakayelinda maslahi ya Mtendaji aliyepita Bw. Mrema na wafanyabiashara watuhumiwa wa ufisadi.

“Patrick Mfugale ambaye Rais alitengua uteuzi wake kwenye nafasi ya ukurugenzi wa barabara sasa ndiye amepewa nafasi ya kukaimu taasisi nyeti kama TANROADS ambayo inahusika na barabara. Hii haiingii akilini, ndio maana sasa Waziri amekuwa akimdhalilisha Rais hadharani kupinga maamuzi yake. Tunamwomba Rais asafishe wizara yetu maana sasa wakubwa wanaangalia maslahi yao tu.”

Vyanzo hivyo vilidokeza kuwa Bw. Mfugale alishiriki katika mchakato uliomuingiza Bw. Mrema TANROADS mwaka 2007 akiwa miongoni mwa wajumbe watano wa Kamati iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo ikiitwa Wizara ya Miundombinu, Bw. Andrew Chenge.

Vyanzo hivyo vilieleza kuwa kabla ya Bw. Mrema kuondoka, alifanikiwa kumpa nafasi mjumbe mwingine wa kamati iliyomteua kwa kumteua kuwa Meneja wa Barabara zinazojengwa kwa fedha za serikali.

Wajumbe wengine walikuwa ni pamoja na Mwenyekiti Profesa Burton Mwamila, Bw. Steven Mlote na Bw. Joseph Haule.
 
Maelezo yana-logic, Je tatizo ni magufuli? Ni nani mwenye mamlaka ya kuteua watu hao? Kwanini mtu akaimu kwa muda mrefu? Wahusika wachukue hatua haraka kuhusu malalamiko haya.
 
Kwa Serikali hii ya kisanii sidhani kama wanaweza kuchukua hatua za haraka, kama wangekuwa wanaliweza hili basi kusingekuwa na malalamiko chungu nzima kuhusu utendaji wake
 
Ningesikia majungu haya yanatoka wizara ya wanawake watoto na nini sijui nisingeshangaa. Wizara ya Ujenzi tena ya wahandisi!!! Hivi kwa nini chokochoko za taarabu haziishi hiyo wizara!!?? Kulikoni!! Kwa nini nafasi ya chief wa Tanroads inaonekana kuwa ya maana kiasi cha kumwona Eng. Mfugale hafai!! Mawazo hayo ya kijinga ndiyo yanayoirudisha nyuma nchi hetu. Kuna watu wamekaa kwenye ofisi kwa ajili ya kupiga domo. Hawana kazi nyingine zaidi ya hiyo na mwisho wa mwezi wanalipwa mshahara.

Dr. Magufuli na Eng. Mfugale endeleeni kupiga mzigo. Achaneni na maneno ya kipuuzi.
 
hiyo wizar ilikuwa imeoza angalau Makufuli anajitahidi kuisafisha lkn hao wafanyakazi hata hawalioni hilo!! shida yetu kubwa watanzania ni wavivu wa kufanya kazi na kufikri pia, barabara kila siku zinajendwa chini ya viwango na hao maofisa sijui mainjinia wapo na hawasemi lolote, leo wamekaliwa kooni wanakasirika!? kwani mtu ukipewa kukaimu unashindwa nini kujibu hoja nzito kama ziko ndani ya mipaka yako, au nazo ni za kifisadi, afu eti "huyo rais wtu mpendwa anafanyiwa usanii" dah! hii si imekaa kujipendeka ili naye rais amuone!!!

bado watz tuna safari ndefu sana kujikomboa huku tuliko, huku maofisini yanaotekea hayana tofauti sana hayo yanaoelezewa hapo juu, esp ofic za serikali, anayefanya kazi vizuri na kwa haki na kwa maslahi ya serikali na umma( wafanyakazi wenzie) wanapigwa vita na hawatakiwi ila wale mazuzu ambao hawawezi kuquestion chochote ndio wanapewa vyeo ili watekeleze watakachoambiwa na wakubwa wao, si tunayaona!!??
 
Ukisoma btn the lines unagundua kuna mtu, watu na wapambe wana hamu na huo ukurugenzi na wanaona inakuwa ngumu with the current set up. Hv utendaji wa hiyo wizara kabla ya Magufuli si ndiyo ulituletea RITES hao wafanyakazi bora walikuwa wapi wakatik huo? Utendaji uliotukuku ni lini uliwahi kuonekana katika hiyo wizara toka 2005?
 
Hapo Mangufuli anaingia vipi? kwani yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Wakurugenzi! Acheni kupindisha mambo, hizi tuhuma inatakiwa ziwe za JK mwenyewe.
 
Magufuli anasingiziwa tu. Ni vigumu sana kwa watu dhaifu na wasioweza kufanya maamuzi mazito kwa masilahi ya Taifa kuweza kufanya kazi na Dr. Magufuli. Inasikitisha sana kuona Wizara hiyo tangu mwaka 2006 haijafanya chochote cha maana mbali na kuendekeza majungu na fitina. Suala la kuteua wakurugenzi sio jukumu la waziri. Tatizo kubwa liko kwa Kikwete mwenyewe na washauri wake na sio Magufuli. Wanaomtuhumu Magufuli wanaajenda zao binafsi ambazo kwa uwepo wa Magufuli wanaona itakuwa vigumu kuzitimiza.
 
Hapa Dkt. Magufuli anausika vipi? Kwani yeye ndiye anayeteua wakurugenzi? mbona sioni mantiki ya mchapakazi huyu kuwajibishwa kwa kupwaya Bosi wake kushindwa kuteua wakurugenzi. Hii si ajabu kwani mkuu huyu wa nchi ameshindwa hata kuteua wakuu wa mikoa, kwa kuofia kukosa mshahara wakuwalipa, ukizingatia kwa sasa hivi wizara ya fedha kwa sasa ni wizara ya madeni/kukopa. Kwa hiyo Magufuli hawekwe mbali na hili, labda kama mnataka kumletea fitina kwa sababu ya utendaji wake, kwa kuwa wizara ya ujenzi inajulikina kwa kula kodi za watanzania kisawa sawa kwa manufaa ya watu binafsi, matumbo yao na familia zao.
 
Tatizo si Magufuli kama wanavyotaka kudanganya watu. Ukisoma between lines inamaana hao Wakurugenzi wanaokaimu na hiyo nafasi ya TANROADS inawaumiza. Huu upuuzi wa kukimbilia vyombo vya habari kwa hoja za kitoto sijui utaisha lini? Hii iliwekwa hapa na ikapanguliwa maana haikuwa na nguvu.
Suala la vyeo ni TATA saana. Kuna haja ya kufumua na hao Wakurugenzi pia.
 
kutokana na utendaji makini wa magufuli,wafanyakazi wa wizara zote wanamuogopa asiwe bosi wao!jamaa hataki bla bla wala story.nakumbuka ali setup ardhi makao makuu mpaka paka pendeza!
 
Hahahaaaaa...wanajf mmenifurahisha mlivyopiga chini huu upuuzi.mie nimeuona nikaona moja kwa moja kuna watu wanataka hiyo post,ila wanatumia mbinu za kipuuzi.Kwani hata asipoteua rasmi aliyepewa kukaimu si kapewa kwa mujibu wa sheria,muacheni hata akaimu miaka kumi,cha msingi mumuheshimu kama mkubwa wenu.Huu upuuzi uko sana serikalini.magufuli anajulikana kwa uchapa kazi ila wale wanaofanya ofc za serikali kijiwe ndio wanapika majungu.mkiwajua muwapige chini tu.
 
Magufuli na Mfugale hawajakutana barabarani
Ningesikia majungu haya yanatoka wizara ya wanawake watoto na nini sijui nisingeshangaa. Wizara ya Ujenzi tena ya wahandisi!!! Hivi kwa nini chokochoko za taarabu haziishi hiyo wizara!!?? Kulikoni!! Kwa nini nafasi ya chief wa Tanroads inaonekana kuwa ya maana kiasi cha kumwona Eng. Mfugale hafai!! Mawazo hayo ya kijinga ndiyo yanayoirudisha nyuma nchi hetu. Kuna watu wamekaa kwenye ofisi kwa ajili ya kupiga domo. Hawana kazi nyingine zaidi ya hiyo na mwisho wa mwezi wanalipwa mshahara.

Dr. Magufuli na Eng. Mfugale endeleeni kupiga mzigo. Achaneni na maneno ya kipuuzi.
 
Back
Top Bottom