Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Wizara ya Mambo ya kigeni ya Ujerumani leo imemwita balozi wa Urusi kujadili uwezekano wa kuiwekea Moscow vikwazo kufuatia madai ya udukuzi ya mwaka 2015 dhidi ya bunge la Ujerumani, Bundestag.
Taarifa ya wizara hiyo imesema balozi wa Urusi amearifiwa kuwaUjerumani inalenga kuuomba Umoja wa Ulaya kuiwekea vikwazo Urusi pamoja na raia wa nchi hiyo Dmitry Badin anayeshukiwa kuongoza udukuzi huo.
Mapema mwezi huu Kansela Angela Merkel aliliambia bunge kuwa ana ushahidi wa Urusi kumlenga mara kadhaa kwenye mashambulizi ya udukuzi na kuongeza uwezekano wa kuiwekea vikwazo nchi hiyo.
Inaaminika kati ya mwaka 2012 na 2015 wadukuzi wa mtandaoni walifanikiwa kukusanya data za wabunge kadhaa wa Ujerumani pamoja na kupakua baruapepe mbili kutoka akaunti ya Kansela Merkel.