mkiluvya
JF-Expert Member
- May 23, 2019
- 809
- 729
Ujerumani imekasirishwa na uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump wa kukata mahusiano na shirika la afya ulimwenguni WHO ikiielezea hatua hiyo kuwa na muvunja moyo na inayorudisha nyuma afya ya dunia.
"WHO inahitaji kufanyiwa mageuzi kama linataka kuleta maadiliko yoyote" aliandika Waziri wa afya wa Ujerumani Jens Spahn katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, huku akisema Umoja wa Ulaya unapaswa kuchukuwa jukumu kubwa la kulisaidia shirika hilo kifedha na kusema hilo, ndilo litakuwa moja ya vipaumbele vya Ujerumani wakati itakapochukua urais wa kupokezana wa umoja huo Julai Mosi mwaka huu.
Hapo jana Trump alisema anakata mahusiano ya Marekani na WHO anayoishutumu kwa kushindwa kuwajibika zaidi kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.