Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kila leo Ukraine inazidi kukandamizwa na marafiki zake.Ujerumani hapo mwanzoni mwa vita tarehe 24 Februari ilisema itaisaidia Ukraine kisilaha kwa kuipa vifaru vyake aina ya Gepard .
Vifaru hivyo baada ya kusubiriwa muda mrefu bila kuwasili Kyiv hatimae imedhihirika kuwa vifaru hivyo havikuwa na makombora yake na kampuni iliyokuwa ikitengeneza imesema ikipata pesa itatengeneza makombora hayo ili yawe tayari mwezi Julai.
Kauli hiyo imemuudhi sana mbunge wa Ukraine, Anastasia Radina na kusema maneno hayo ya Ujerumani ni kama kumwambia mama aliyejifungua mtoto na hana maziwa asubiri mpaka miezi mitatu ndipo amnyonyeshe mwanawe.