Saudi Arabia yaonyesha mshikamano, na kulaani shambulio
Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia ilitoa taarifa mapema Jumamosi, "ikionyesha mshikamano wake na watu wa Ujerumani na familia za waathiriwa."
Wizara pia "ilithibitisha kukataa matumizi ya shambulio ."
Haiba ya Dr. Taleb al-Abdulmohsen daktari wa magonjwa ya akili aliyetekeleza shambulizi sokoni :
Saudi Arabia iliionya Ujerumani kuhusu mtu aliyeshikiliwa kwa shambulio la soko la Xmas mjini Magdeburg
Saudi Arabia awali mara kadhaa iliionya Ujerumani kuhusu mtu aliyekamatwa kufuatia shambulio la mjini Magdeburg Ujerumani Watu watano wameuawa na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa baada ya gari kutumika kama zana ya silaha ya kigaidi ktk shambulio kwa kuendeshwa kwenye soko la Krismasi lenye shughuli nyingi.
Watu waliweka maua na mishumaa kwenye kanisa huko Magdeburg siku moja baada ya shambulio hilo .
Mamlaka za Saudia ziliionya Ujerumani mara kwa mara kuhusu mtu anayedaiwa kutekeleza shambulizi la Ijumaa kwenye soko la Krismasi katika mji wa Magdeburg mashariki mwa Ujerumani na kusababisha vifo vya watu watano na makumi kadhaa kujeruhiwa, kulingana na maafisa wa usalama wa Ujerumani.
Maafisa hao walisema Riyadh ilizionya mamlaka za Ujerumani mshukiwa mshambulizi, Dr. Taleb al-Abdulmohsen, mpinzani wa Saudi ambaye alijieleza kuwa Muislamu aliyeachana na Uislamu, alijigamba kwenye mitandao ya kijamii kwamba "kitu kikubwa kitatokea nchini Ujerumani".
Haikuwa wazi kama polisi waliwahi kufanyia kazi onyo hilo.Machapisho mengi ya Al-Abdulmohsen kwenye mtandao wa kijamii wa X yanafichua kuwa alikuwa mkosoaji mkali wa Uislamu ambaye alikashifu Ujerumani kufungua milango kwa wahamiaji wa Kiislamu barani Ulaya na katika miezi ya hivi karibuni alionyesha kuongeza chuki na uadui kwa mamlaka ya Ujerumani, ambayo aliwashutumu kwa kujaribu kudhibiti watu kutoa maoni huru dhidi ya uislamu
.Watu watano waliuawa na zaidi ya 200 kujeruhiwa siku ya Ijumaa jioni wakati mwanamume mmoja alipovamia soko la Krismasi la Magdeburg.
Al-Abdulmohsen, mshukiwa wa shambulizi alikamatwa katika eneo la tukio. Mamlaka zilimtaja kama daktari mwenye umri wa miaka 50 kutoka Saudi Arabia ambaye alikuja Ujerumani mwaka 2006 na amekuwa akifanya kazi kama daktari wa magonjwa ya akili huko Bernburg, kusini mwa Magdeburg.
Shambulio hilo limetia giza hali ya hewa katika nchi ambayo tayari inakabiliwa na mdororo mkubwa wa kiuchumi na awamu ya kutokuwa na uhakika wa kisiasa kufuatia kusambaratika kwa serikali ya muungano ya vyama vitatu ya Kansela Olaf Scholz mwezi Novemba.
Shambulizi la ijumaa sokoni December 2024 limetokea karibu miaka minane baada ya mwanamgambo wa Islamic State kutumia lori kama silaha ya shambulizi kwenye soko la Krismasi mjini Berlin, na kuua 12, na kujeruhi 49 katika moja ya mashambulizi mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini Ujerumani.
Scholz alitembelea Magdeburg siku ya Jumamosi tarehe 21 December 2024, akiita tukio hilo kuwa "kitendo cha kutisha" na kuahidi kwamba "hakuna jiwe litakaloachwa" katika uchunguzi wa uhalifu.
Dr. Al-Abdulmohsen alikuwa mwanaharakati ambaye alikana Uislamu hadharani baada ya kuondoka Saudi Arabia na kuunda tovuti ya kuwasaidia wapinzani wa utawala wa Riyadh - hasa wanawake - kukimbia nchi na kuomba hifadhi Ulaya. Katika mahojiano na machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii yanafichua kuwa ni mkosoaji mpingaji wa Uislamu ambaye aliendeleza kuhusudu siasa za chama cha nchini Ujerumani cha Alternative for Germany (AfD), chama cha siasa kali za mrengo wa kulia kinachopinga vikali uhamiaji wa watu kutoka nchi za Kiislamu.
Katika miezi ya hivi majuzi Dr. Taleb al-Abdulmohsen alizidi kuwa na chuki dhidi ya Ujerumani, na kukosoa sheria zake kali dhidi ya matamshi ya chuki ambazo zinakataza uchochezi dhidi ya vikundi fulani vya kidini au kikabila.
Akiwa katika mahojiano ya kina na magazeti ya Ujerumani Dr. Taleb al-Abdulmohsen kuhusu uanaharakati wake mwaka 2019, akijieleza kwa gazeti tajwa kubwa la Frankfurter Allgemeine Zeitung kama "mkosoaji mkali zaidi dhidi ya Uislamu katika historia". "Ikiwa huniamini, waulize Waarabu," alisema.
"Baada ya miaka 25 katika fani yangu hii, unafikiri hakuna kitu kinachoweza kukushangaza zaidi," aliandika Peter Neumann, mtaalamu wa ugaidi katika Chuo cha King's College, London, kwenye X.
"Lakini Muislamu wa zamani wa Saudi mwenye umri wa miaka 50 ambaye anaishi Ujerumani Mashariki, kukipenda AfD chama cha mrengo mkali dhidi ya wahamiaji na sasa anataka kuiadhibu Ujerumani kwa uvumilivu wake kwa Waislam - hiyo haikuwa kwenye rada yangu anasema Peter Neumann, mtaalamu wa ugaidi katika Chuo cha King's College, London.
"Katika moja ya mahojiano ya 2019, alisema "amejitenga" na Uislamu mnamo 1997." Niliona maisha nchini Saudi Arabia kuwa ya taabu kwa kuwa lazima kuigiza kuwa wewe ni Mwislamu na kufuata mila zote," alisema.
"Nilijua singeweza tena kuishi kwa hofu na nilipogundua kwamba hata harakati zisizojulikana zingeweka maisha yangu hatarini kama Muislamu wa zamani wa Saudi, niliomba hifadhi Ujerumani. "Katika nyingine, alisema alikuwa ameandika machapisho ya kuukosoa Uislamu katika kongamano la mtandao linaloendeshwa na mwanaharakati aliyefungwa jela Raif Badawi na baadaye kupokea vitisho dhidi ya maisha yake."Walitaka 'kunichinja' ikiwa nitarudi Saudi Arabia," alisema.
"Haingekuwa na maana yoyote kujiweka kwenye hatari ya kurudi na kisha kuuawa."Katika miezi ya hivi karibuni, alionekana kujitenga na uanaharakati na kubadili matusi dhidi ya mamlaka ya Ujerumani, akiweka nadharia za njama mara nyingi zinazohusiana na haki ya utaifa.
Katika baadhi ya machapisho alidai kuwa alikuwa akizongwa pia akidhibitiwa na kuteswa kisaikolojia na mamlaka ya Ujerumani kwa kuandika mawazo huru au kujieleza kwa uhuru katika mahojiano na media za Ujerumani .
Katika chapisho la X mnamo Novemba akielezea "mahitaji ya upinzani wa kiliberali wa Saudi" alitoa wito kwa Ujerumani "kulinda mipaka yake dhidi ya uhamiaji haramu".
"Imedhihirika kuwa sera ya kuweka mipaka ya wazi ya Ujerumani kwa uhamiaji holela ilikuwa ni mpango wa [kansela wa zamani Angela] Merkel wa kuisilimisha Ulaya," aliandika.
Pia aliitaka Ujerumani kubatilisha sehemu za kanuni zake za adhabu ambazo anadai “kikomo . . . uhuru wa kujieleza” kwa “kufanya kuwa kosa [sic] kutusi au kudharau mafundisho au mazoea ya kidini”.
Wasifu wake wa X una bunduki na anadai "Ujerumani inawafukuza wanawake wanaotafuta hifadhi nchini Saudia, ndani na nje ya Ujerumani, ili kuharibu maisha yao".
Katika mahojiano mapema mwezi huu kwenye blogu inayopinga Uislamu aliishutumu mamlaka ya Ujerumani kwa kutekeleza operesheni ya siri ya kuwasaka waliokuwa Waislamu wa Saudia huku wakiwapa hifadhi wanajihadi wa Syria.
Katika miezi ya hivi karibuni jumbe zake zilichukua sauti inayozidi kutisha. "Ninawahakikishia: ikiwa Ujerumani inataka vita, tutakuwa na moja," aliandika kwenye X mnamo Agosti. "Ikiwa Ujerumani inataka kutuua, tutawaua, tutakufa au kwenda jela kwa kiburi
Source : Financial Times Ft.com