Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,926
- 15,634
EU+NATO washindwa tena ktk kutekeleza vikwazo walivyokubaliana na kuviweka wao wenyewe juu ya kuminya matumizi ya gesi ya Urusi ili kuipunguzia Urusi pesa ipatazo toka kwenye biashara hiyo.
Mabeberu waliweka vikwazo ktk vipuri vya miundombinu ya gesi. Ujerumani ilipeleka injini fulani Canada ikafanyiwe matengenezo. Injini hiyo inahusika na mitambo ya gesi ya Urusi kwenye miundombinu iliyopo Ujerumani. Injini ikazuiwa Canada kwa kuwa ipo kwenye list ya vifaa vinavyofanyiwa vikwazo.
Urusi haikusema neno. Yenyewe ikafanya vitendo tu. Ikapunguza gesi iliyokuwa ikiipeleka Ujerumani kwa asilimia 60, yaani ikawa inapeleka gesi ailimia 40 tu. Ujerumani wamechezea mkong'oto mkali ambao umeathiri sekta mbalimbali ikiwemo viwanda na uchumi. Ujerumani yenyewe sasa ndio ikapiga magoti kwa Canada kuwa jamani tunaomba hiyo injini irejeshwe nchini Ujerumani ili tupate gesi kwa asilimia zote (100%), hali ni tete sisi Wajerumani ndio twateseka, na sio Putin...Uchumi waanguka na isitoshe winter yaja.
Wakati Ujerumani yalalamika hivyo, Zelensky anaiambia Canada isiachie injini ile, kwa maneno mengine Zelensky anafurahia Wajerumani kuendelea kuteseka kwa faida yake yeye Zelensky na Ukraine. Mwisho wa siku Zelensky kapuuzwa na injini inarejeshwa Ujerumani.
=======