"Ujinai" wa Lulu katika "mauaji" ya Kanumba (R.I.P)

Labda sijakusoma vizuri.....ila Lulu ana miaka 18 na miezi kadhaa sasa hivi....
Sio kwamba alitoka nje kusikiliza simu.....kwa mujibu wa kaka wa marehemu steve.....lulu na kanumba walitoka ndani wakifukuzana mpaka nje marehamu akitaka kujua nani anaongea na lulu....sio kwamba alitoka mwenyewe na kusikiliza simu.....
tena....kanumba hakumfungia Lulu ndani...ila aliingia chumbani na lulu na haijajulikana kama alifunga mlango au la..na hata kama alifunga mlango ieleweke hakumfungia ila alifunga mlango na yeye akiwa ndani....kuna utofauti hapo WoS....Pia mdogo wa marehemu alisikia mifarakano ya marehemu na lulu na chanzo kilikuwa simu....hakujaribu kugonga kuuliza mpaka alipoitwa na lulu....

hapa ninatoa kama alivyosema mdogo wa marehemu ambae alikuwa kwenye scene.....ni kwamba baadae alifuatwa na lulu na kuambiwa kakake kaanguka..alipokwenda alimkuta anatoka na mapovu kinywani....alipokuwa anatafuta means na kumpigia dr wake...muda woote huo lulu alikuwa akizunguka zunguka ndani....na mara akatoweka bila kuaga.....kama angekuwepo basi mtu wa kwanza kufika pale muigizaji mwenzake angemkuta lulu muda huo usiku wa manane.....je alikwenda wapi?????

Sasa ndugu zanguni, kwanini Lulu anaonekana alifanya mauaji ya kukusudia? Ikiwa Kanumba alianguka katika purukushani na kuponda kichwa na kufa, Lulu kaua vipi?
 
Last edited by a moderator:

Kama Ditopile alipata dhamana katika kesi yake ya kuua kwa kukusudia (japo ilibadilishwa na kuwa kuua bila ya kukusudia).. Kwa nini Lulu nae acipewe dhamana kwa shauri hili ambalo kisheria si kubwa kama lile la Mh marehemu Ditopile..? Double standard..?
 

Kitendo cha daktari wa kanumba kwanza kutotoa maelezo kwa simu juu ya huduma mpaka kuja mwenyewe nyumbani kwake ni uthibitisho wa kuwa kulikuwa na ugonjwa aliokua ana mtibu specifically,then kuruhusu mwli ubebwe kupeleka muhimbili bila kuhusisha polisi kuja kuchunguza ni uthibitisho wa pili kwamba alijiridhisha kanumba alikufa natural death tokana na ugonjwa uliokuwa una msumbua pengine from mixing medication na hizo jd zake
 
Utata mtupu.Mbona kuna maelezo mengine kuwa alilegea na kuanguka mwenyewe?Inapingana na suala la kupigana

“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.

“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”

“Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”


Source: Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza
 
lulu kakua yakhe
 
nimependa ulivyochambua hili tukio.
katika eneo ulilolipa (2) umeeleza kuwa marehemu ndiye aliyekuwa mshari,lakini msingi wako mkuu kwa kusema hivyo ni kwa sababu alimfuata nje na kumrudisha ndani kwa ajili ya mahojiano. sidhani kama kumfuata mtu unaemtilia shaka juu ya jambo fulani na kutaka kujua nini kinaendelea utakuwa wewe ndio mshari, hapana. nasema hivyo kwa sababu zifuatazo.moja, aliyetiliwa mashaka akitoa majibu yasiotia shaka hakuna tatizo hapo.lakini akitoa majibu yanayotia shaka na yakapelekea ugomvi naye ana sehemu yake ya lawama.pili,endapo naye anayehoji akipewa majibu lakini akayakataa na kutaka iwe anavyofikiri yeye atakuwa ndiche chanzo. lakini tatu, wote walitakiwa kupima cosequences ya ubishi waliokuwa wameuanzisha, nakunukuu,kwanini Lulu anaonekana alifanya mauaji ya kukusudia,

hapa,WoS, umenichanganya sana, hivi hukumu imekwishatoka au huu ni mtizamo wako? nakunukuu tena," Ikiwa Kanumba alianguka katika purukushani na kuponda kichwa na kufa, Lulu kaua vipi?" haya ukumbuke ni maneno ya mtuhumiwa lakini sio matokeo ya uchunguzi. na sitegemei mtuhumiwa aseme nimeua. ni mara chache sana. lakini kwa mtazamo wangu wa haraka sana naona kuwa kweli alianguka kwa sababu tangu mwanzo wa hizi taarifa hakuna aliyesema mambo yafuatayo,

  • tulipoingia chumbani kwa marehemu tulikuta vitu vimetawanyika na stuli au chupa au kitu chochote kilikutwa na alama za damu kuonyesha kuwa kilitumika kama silaha.
  • Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi, uchunguzi wa madaktari unaonyesha kuwa, ubongo wa marehemu (sehemu ya Nyuma) ulishtuka na kushindwa kufanya kazi na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji. madaktari hapa nao wamekaa kimya kuhusu majeraha katika mwili (kichwa) cha marehemu.lakini sehemu ya nyuma ya kichwa ina maana ya kisogo. ukitizama kwa haraka haraka, huwezi kugombana na mtu ukampa kisogo. ina maana walikuwa face to face. sasa mtuhumiwa anampigaje marehemu kisogoni wakati wanatazamana? ina maana aidha alianguka kwa kuteleza au kusukumwa.
unajua kuna wakati unakosa namna ya kupata majibu na kulazimika kukubaliana na maelezo ya mtuhumiwa kwani ndiye pekee aliyekuwepo kwenye eno la tukio. lakini utafanya hivi in absence of other evidences. ngoja tuwaachie wataalamu. mtu aliyekuzidi nguvu anapokufungia ndani ya chumba kwa nia mbaya, 'you have to use the first available apportunity to save your life and don't go back unless you are sure it's safe.'
 


Nimejaribu ku-google kuhusu brain concussion na kusoma maelezo yake.. Bado ninashindwa kuyaelewa haya maelezo ya madaktari wetu.. Unaweza kupata brain concussion and yet usiwe na alama au uvimbe maeneo ya kichwani..? Pitia tovuti hizi mbili hapa chini..

Brain Concussion Causes, Types, Symptoms, Diagnosis, Treatment, and Prevention Information on MedicineNet.com#
Concussions & Brain Injuries Pictures Slideshow: Symptoms, Test & Treatment on MedicineNet#
 
Ukifuatilia hii thread https://www.jamiiforums.com/celebri...lu-ajishushia-hadhi-kwa-kuendekeza-pombe.html aiseee ina maana haka katoto kalianza kwenda night club kakiwa na 15?? cus hiyo ilikuwa 2010....
kuna haja hizi club zetu kuingia na ID........unaonyesha mlangoni.....

kwa hali hii hata mie nikikuta shoree tena kama huyu alivyovaa uchi tena club.....kumtongoza then nikamrukia sitakuwa na kosa.....


hata kanumba tusimlaumu maana nimeanza kusikia eti alimbaka kwa umri wake.....
 
kweli huyu dokta nae ana siri kubwa kuna kitu hapo katikati.
 
Of course Lulu hajaua ila anavuna alichopanda. Angekuwa binti aliyetulia hili vagi lisingemkuta. Atatoka ila yaliyompata kajitakia.
 
He!!! Makubwa haya!!! Mambo ya Lulu ndio haya!!!!
 
the weight of the event now it is on LULU's shoulders , at her age..it is too heavy for her..kibaya zaidi ni jinsia yake na lifestyle yake..huko polisi ndugu zanguni..hakufai..namuonea huruma sana..pole yake..
 
mkuu unachotakiwa kuelewa ni kwamba, katika kesi yeyote ukiona kuna mazingira ya kupigana, basi hiyo huenda moja kwa moja kwenye manslaughter. Hapa sisi sote hatuna facts, facts zipo kule polisi,bado wanafanya utafiti. tunachoongelea hapa, ni kutokana na yale tu yaliyoongelewa juu juu.

Kuhusiana na hiyo principle of causation, usiumize sana kichwa, nimeandika opinion nyingi sana nikiwa state attorney, katika kesi hizi hizi za murder. zipo Court of Appeal case law zinazosema death resulting as a result of a fight will always endup to a lesser offence of manslaughter, na sio murder. hapa tunachoongelea kwa huyu dada ni murder or manslaughter tu, kwani kosa gani lingine unafikiri atashitakiwa katika homicide kama hii? only either of the two, na ndizo tunazozijadili. .................., pamoja na ile whisky na soda, so vikienda kwa mkemia mkuu watatoa jibu zuri kama alilishwa sumu, etc, hapo ndo labda uyu mtoto anaweza kuwa kwenye mazingira ya kwenda kwenye murder, lakini kama walikuwa katika ugomvi akamuua, moja kwa moja ni manslaughter.
 
my friend, hakuna mtu hata mmoja anayeweza kupata dhamana katika kosa la kuua kwa kukusudia, yaani murder. Ditopile ile kesi ilianza kwa kuua kwa kukusudia, lakini baadaye ilibadilika kuwa kuua bila kukusudia. unachotakiwa kuelewa ni kwamba, katika kesi za murder, upelelezi ukikamilika jalada huwa linapelekwa kwa mawakili wa serikali wakaandika opinion kama iwe murder or manslaughter, hapo ndo kosa linabadilika, ikidondokea kwenye manslaughter tu unaweza kuomba dhamana high court. kama ikibakia murder basi subiri tu jaji. hakuna murder yenye dhamana.
 
Hata kama kukiwa na ushahidi kuwa mtuhumiwa alipanga kuuwa na ili kutimiza lengo lake alianzisha 'ugomvi' makusudi ili kuwepo na kupigana na hatimaye atimize lengo lake?
 
Hata kama kukiwa na ushahidi kuwa mtuhumiwa alipanga kuuwa na ili kutimiza lengo lake alianzisha 'ugomvi' makusudi ili kuwepo na kupigana na hatimaye atimize lengo lake?
kila kesi huwa inaamuliwa kulingana na facts zake. hapa naongelea watu kugombana tu kwa kawaida kwa kutumia ngumi tu na sio silaha. kama hiyo premeditated malice aforethought (intention to cause death)kweli ilikuwepo, na ukathibitisha kwamba ilikuwepo, basi inaweza kuwa murder, ila kila kesi huamuliwa kwa facts zake. vilevile katika kesi za murder, aina ya silaha iliyotumika, eneo ambalo mtu ame attack, na mazingira mbalimbali ya kabla na baada ya kufanya tukio vyote hivi huwasaidia majaji kutathimini kama ni murder au manslaughter au kuachiwa kabisa.muunganiko wa vitu hivi pia vyaweza kufanya mnyororo wa ushahidi unaoweza kueleza kama mshitakiwa alikuwa na nia ya kuua au la. kwahiyo kwa sali lako, naweza sema not always, ila kila kesi huamuliwa kwa facts zake.

however, kumbuka hapa tunaongelea wapenzi hawa wawili kanumba na lulu. kwa hiyo unataka kusema lulu alikuwa na nia ya kumpiga kanumba hadi amuue, kwahiyo alianzisha ugomvi kama chambo? is that what you wanted to say, kwasababu hapa tunaongelea topic ya lulu ujue.
 
Reactions: SMU
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…