Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Wanasayansi hivi sasa wanakiri kwamba, huwa inatokea mpenzi akamshika mpenzi wake kwenye akili, yaani akili yako inaweza kushikwa na mpenzi wako na ukasumbuka sana. Kwenye lugha za mitaani hali hiyo inaitwa kushikwa au wengine huita Limbwata.
Kwenye kitabu kiitwacho, Why we Love: The nature and Chemistry of Romantic Love, mtafiti Helen Fisher anasema, kuna usugu ambao hujengwa kwenye akili ya mpenzi, sawa na usugu unaojengwa na sigara kwenye akili ya mvutaji kiasi kwamba, ni vigumu sana kukubali kuachwa au kuachana naye, hata kama anakutesa na kukuuwa.Eneo la ubongo ambalo linakuwa na mabadiliko pale mtu anapomwona na kumfikiria mpenzi wake, ni eneo hilo hilo linalokuwa na mabadiliko wakati mtu anapotumia madawa ya kulevywa.
Hii ina maana kwamba, kama inavyotokea mtu akashindwa kutoka kwenye ulevi hadi anakuwa sugu, ndivyo inavyotokea kwa baadhi ya watu wanapopenda.Hivi sasa tafiti zinathibitisha kwamba, mtu anapoingia kwenye hali ya kupenda kusiko na kizuizi, yaani kushikwa, sehemu inayohusika kwenye ubongo huonesha dalili zote ambazo hujionesha mtu anapobwia dawa ya kulevywa aina ya Cocaine, kama vile kukosa usingizi, kushindwa kujua hata muda au kutojali kuhusu muda na kuweka nguvu kwenye penzi, kiasi cha kutojali maumivu yake au ya wengine wanaomzunguka.
Inaelezwa kwamba, mtu anapoathiriwa kwenye eneo hilo la ubongo na mapenzi, anakuwa hawezi kupambanua mambo, kwani eneo la mantiki ubongoni linakuwa limezuiwa kufanya kazi. Ndio maana mtu anaposhikwa kwenye mapenzi anaonekana wazi hatumii akili, kwani hushindwa kuona ukweli hata ule mdogo kabisa.