MUWHWELA
Senior Member
- Oct 26, 2013
- 167
- 238
Twime tubite!!
Dunia yetu imejaa taarifa ambazo siyo sahihi japo ni za kweli, kwa kuwa siyo za kweli basi zimewekwa kwenye mifumo ya Elimu na Media Ili lengo lao Liwe timilifu.
Binafsi nikiwa Katika lindi la mawazo huru nakuja kugundua kwamba UJINGA ni bidhaa inayouzwa kwa bei kubwa bila wajinga wenyewe kujua kwamba wananunu ujinga.
Elimu yetu imeundwa na mkoloni, Ili ipewee kibali Cha kukubalika duniani lazima ifuate utaratibu wao, unajiuliza kwani kufundisha watu wetu utamaduni wetu na mawazo yetu kama Babu zetu haiwezekani? Jibu (inawezekana)
Tuna vyuo vikuu vya kiafrika vilivyopo Afrika Lakini mifumo Yao yote ni ya Ulaya,Amerika au Asia, hapa ndipo msingi wa kuzalisha wajinga unaporutubishwa..
Ukishindikana huko kwenye Elimu basi utaangamia kwenye Media, wanatangaza na kusemea agenda zao za Siri, kwa kuwa ubinadamu wetu una-addict Fulani basi vile tunavyoona mara kwa mara kwenye tv zetu na mitandaoni huo tunaona ndiyo ukweli na jambo sahihi kumbe ni kampeni za kupumbaza wengi zaidi.
Mawazo yetu Yako wapi, Fikra zetu zimefia wapi, maulizo murua yamepotelea wapi..vyote vimeondoka na dhana hizi Tatu...Dini,Media , Elimu .
Wengi hatutumii mawazo yetu, Kila ukisema una wazo lako, ama ulifundishwa shule, kwenye nyumba ya Ibada au uliona Katika tv Yako...Lakini huwezi kukuta MTU mwenye misuli ya kujisemea na kusimamia mawazo yake, nje ya alichofundishwa.
Turuhusu mawazo yetu yafanye kazi na kizazi hiki, hayo yote yaliyoandikwa na yanayosemwa tunayoyaamini ni Mawazo ya watu...Tena watu kama sisi tu siyo malaika.
IPE AKILI KAZI