Ujinga wa mtanzania (?)

Ujinga wa mtanzania (?)

Mbu

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2007
Posts
12,752
Reaction score
7,861
...mambo mengine tukisema ni ujinga wa mwafrika, tunakosea. Huu wizi wa vifaa vya hospitali, mfano huu wa kuiba mashine ya saratani, ni ujinga wa mtanzania.

hii ni Inside job, inayowahusisha wafanyakazi wote... walinzi, watumiaji (lab technician), wabebaji, dereva aliyehusika, middleman 'aliyechonga huo mchongo', pamoja na huyo mnunuzi!... WAFUNGWE WOTE wakipatikana!!!

Mashine tiba ya kansa yaibwa Ocean Road

2009-01-31 10:50:32
Na Tamara Manyata

Zaidi ya wagonjwa 170 hawatapata matibabu ya saratani (kansa) katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es salaam baada ya mtambo wa kuendeshea mashine za kuchoma mionzi kuibwa hospitalini hapo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka taasisi hiyo, kuibiwa kwa kifaa hicho kunafanya shughuli nzima ya uchomaji wa mionzi na tiba ya saratani kusimama.

Akielezea tukio hilo, Mkurugenzi wa Ttaasisi hiyo, Dk Twalib Ngoma, alisema kuwa mtambo huo uliibiwa usiku wa kuamkia jana huku kukiwa na takribani wagonjwa 170 wanaohitaji tiba inayotolewa na mitambo hiyo.

Kwa mujibu wa Dk. Ngoma, mtambo huo hapa nchini upo Ocean Road tu.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Alisema kuwa Jeshi la Polisi linawashikilia watumishi sita kutoka Taasisi hiyo kwa ajili mahojiano zaidi.

Aidha, huduma za tiba ya saratani zitaendelea baada ya kifaa hicho kupatikana au kununuliwa kingine.
Kifaa hicho pamoja na mashine ya mionzi kinagharimu kiasi cha Sh bilioni moja.
 
Ni kweli, mara kadhaa nimesema hapa JF, umasikini wetu wa kwanza kabisa waTz ni AKILI.

Kwa kweli sijui ni lini tutajikomboa..
 
jamani naomba niulize, hiyo mashine inaukubwa gani. kama punje ya mchele au ni kubwa kama zile za X-ray, haiwezi kuingia akilini kabisa, kuna wagonjwa wamelazwa pale na kuna walinzi na wahudumu wa hospitalini, iweje mashine itoke nje,
mimi siamini kama huo ni wizi, huo ni ufisadi mtupu, hiyo mashine itapatikan lakini itakuwa sio yenyewe kwani wameenda kuiswap tu
 
...Ujinga huu si kwamba umeanza kwa hiyo mashine tu, ...hata Hospitali kuu kama Muhimbili utashangaa kusikia vifaa vikubwa na adimu nchini eti vinaibiwa, halafu huduma matibabu kwa kutumia vifaa hivyo yanasimamishwa!

Mbaya zaidi, baada ya siku kadhaa unasikia hospitali binafsi imeanzisha huduma ya matibabu kwa kutumia kifaa hicho hicho... kwa malipo maradufu ya yale yanayotolewa kwenye hospitali za rufaa...

Inasikitisha sana sana sana.

mfani; ni aibu kubwa kwa Dialysis Machine (mashine ya kusaidia figo kusafisha damu) inapatikana (kwa ufahamu wangu mpaka sasa) pale Regency Hospital pekee, labda na Aga Khan au Hindu Mandal, wakati naamini Serikali ilipokea msaada wa Dialysis Machine hospitali ya Muhimbili, lakini miaka na miaka sasa imeharibiwa kwa makusudi, na spare zake zinayeyukia mikononi kwa 'wajinga' kama hao wanaoiba mashine ya matibabu ya saratani.

Haki ya Mungu serikali ya Tanzania hii inahitaji mtu kama Mrema, siku saba mashine ingekuwa isharudishwa hiyo!!!
 
Hahahahahahaaa...Miafrika Ndivyo Tulivyo! Kwa kiasi kikubwa, mambo ya kipumbavu yatokeayo Tanzania hutokea pia katika nchi zingine za Kiafrika. Sisi ni Ndivyo Tulivyo, period.
 
Ni kweli, mara kadhaa nimesema hapa JF, umasikini wetu wa kwanza kabisa waTz ni AKILI.

Kwa kweli sijui ni lini tutajikomboa..

...mambo kama haya ndiyo yanayomfanyisha NYERERE aonekane nabii kwa wafuasi wengine, au RAIS aliyekuwa na muono wa mbali kuliko kiongozi mwingine yeyote aliyepata kuiongoza Tanzania

...alisema ili tuendelee tunahitaji kupiga vita UJINGA, MARADHI na NJAA... na hayo yanawezekana tu iwapo tutakuwa na WATU SAFI, ARDHI, SIASA SAFI na UONGOZI BORA katika nyanja zote...

Swali zuri sana hilo, LINI TUTAJIKOMBOA?

...mambo mengine kama hayo ya kuiba yanatia aibu kusema yanatokea TANZANIA hii ya mwaka 2009. Unaiba kifaa cha kuendesha mtambo kama huu...
...ili iweje kwa wagonjwa? ndio kama wale wanaoiba vyuma vya reli wakati ndugu na jamaa zao wenyewe wengine walio mahututi wanatumia usafiri wa reli!

Sabotage nyingine ziangukie kwenye makosa ya Uuaji! wahusika kama hawa wahukumiwe kama wenye makosa ya kuua...! Adhabu yao iwe kunyongwa hadharani! ...Na experience binafsi ya kumuuguza mgonjwa wa saratani, na mateso yanayoambatana na ugonjwa huo,... nikifikiria delayed treatment kwa wagonjwa wote hao, haki ya mungu Inauma sana!
 
Mosi, Hiyo ni sawa na kuiba ndani ya nyumba yako.

Pili, tunatakiwa kubadilika kifaa hicho ni nyeti tulitakiwa kuweka ulinzi na usalama wa kutosha. Dunia yote kwa ujumla imebadilika...mimi nasema Binadamu ndio walivyo kumbuka binadamu ni kama mnyama yoyote ambaye anaweza kurudi katika ualisia wake ambao huwezi kumtofautisha na wanyama wengine( naongelea erosion of moral standards duniani).

Suluhisho: Serikali na taasisi zake zinatakiwa kuakikisha kuwa zinafunga kamera za usalama katika maeneo yote nyeti kama hapo taasisi ya kansa - Ocean Road. Tubadilike jamani.

Shadow.
 
Sasa huyu mwizi tukimpata tumfanye nini? Hali niliyo iona pale ocean Road hospital siku moja inatisha sana. Inakuwaje mtu ktk mazingira yale magumu ya ndugu zetu wagonjwa unapanga dili la hivyo? Asilimia kubwa sana ya wagonjwa pale hutokea mikoani na wengi ni walalahoi wenzetu.

Hapa naungana na Waziri Mkuu Pinda, tukimshika tumchome moto mchana kweupe.
 
Mosi, Hiyo ni sawa na kuiba ndani ya nyumba yako.

Pili, tunatakiwa kubadilika kifaa hicho ni nyeti tulitakiwa kuweka ulinzi na usalama wa kutosha. Dunia yote kwa ujumla imebadilika...mimi nasema Binadamu ndio walivyo kumbuka binadamu ni kama mnyama yoyote ambaye anaweza kurudi katika ualisia wake ambao huwezi kumtofautisha na wanyama wengine( naongelea erosion of moral standards duniani).

Suluhisho: Serikali na taasisi zake zinatakiwa kuakikisha kuwa zinafunga kamera za usalama katika maeneo yote nyeti kama hapo taasisi ya kansa - Ocean Road. Tubadilike jamani.

Shadow.

...Shadow, deal ya kuiba huenda ilimhusisha hata huyo mlinzi ambaya hata ingefungwa cctv, huenda yeye ndiye ange pause/kubadilisha tape kupoteza evidence...

Mungu samehe lakini mijizi kama hiyo naiombea ife kidogo kidoooogo kwa saratani!!!
 
Mbu, Kuna siku shemeji yangu kasahau simu yake tawi la benki ya CRDB pale mwenge kwenye ATM na aliporudi kuomba uongozi uonyeshe mkanda wa mida hiyo ili waweze kumpata mtu alikwapua hiyo simu. Uongozi ulisema kamera mbovu kwa hiyo habri ndo ikawa imeishia hapo.

Tunatakiwa kubadilika kweli kweli. Ulinzi kama wa Ocean Road unatakiwa si tu kwenye CCTV bali hata hao walinzi wa getini ambao wako bize kutumwa na wagonjwa kununua matunda nje ya lango badala ya kulinda usalama.

Hapo pia kunatakiwa kuwajibika kwa uongozi wa hiyo hospitali. Utasikia wameunda tume yenye kuchukua gharama mara mbili ya kifaa kilichoibwa...Binadamu isee, kileo cha mwingine yeye anageuza mradi...I am pissed off..

God Bless Tanzania...
 
Kwa mujibu wa Dk. Ngoma, mtambo huo hapa nchini upo Ocean Road tu.

Kama huo mtambo umeibiwa kwa ajili ya kutumika hapa nchini ni rahisi kupatikana, kwa mujibu wa Dk. Ngoma kuwa upo Ocean Road tu. Lakini kama utapelekwa nje ya nchi, hapo ndio itakuwa kazi. Sasa wagonjwa wote wa Kansa iliyoshindikana hupelekwa OR, kweli wengi watapata shida kwa muda huu. Ufisadi kila kona...
 
Mbu, Kuna siku shemeji yangu kasahau simu yake tawi la benki ya CRDB pale mwenge kwenye ATM na aliporudi kuomba uongozi uonyeshe mkanda wa mida hiyo ili waweze kumpata mtu alikwapua hiyo simu. Uongozi ulisema kamera mbovu kwa hiyo habri ndo ikawa imeishia hapo. Tunatakiwa kubadilika kweli kweli. Ulinzi kama wa Ocean Road unatakiwa si tu kwenye CCTV bali hata hao walinzi wa getini ambao wako bize kutumwa na wagonjwa kununua matunda nje ya lango badala ya kulinda usalama. Hapo pia kunatakiwa kuwajibika kwa uongozi wa hiyo hospitali. Utasikia wameunda tume yenye kuchukua gharama mara mbili ya kifaa kilichoibwa...Binadamu isee, kileo cha mwingine yeye anageuza mradi...I am pissed off..
God Bless Tanzania...

Shadow, unajua TZ vitu huwa vinafanywa kimchezo mchezo, unaweza kuta huo mkanda ulikuwepo, ila kuanza kumuonesha wanaona ni usumbufu manake katika huo upotevu hawaathiriki kitu.

Umenikumbusha, nilienda hospitali moja Mwanza kujaziwa "Medical Examination Form". Sasa nilikuwa na bahasha, yule daktari aliyenifanyia uchunguzi nilipokuwa naongea naye nikasahau bahasha yangu juu ya meza yake, ambayo nilikuwa niitume nikitoka pale hospitali. Nilipotoka baada ya dk kama 15 nikakumbuka nimesahau bahasha kwa daktari. Nikarudi, nilipogonga na kuingia si nikamkuta keshaifungua anaangalia kuna nini, alishtuka aliponiona. Nikamwambia nipe bahasha yangu, nikaangalia kila kitu kipo, sikumwambia kitu nikaondoka. Uaminifu umepungua sana.
 
Ocen Rd ni karibu na Ikulu na kuna mageti milango yote..je wezi walipita wapi?

Hii ni deal from inside?
 
Hahahahahahaaa...Miafrika Ndivyo Tulivyo! Kwa kiasi kikubwa, mambo ya kipumbavu yatokeayo Tanzania hutokea pia katika nchi zingine za Kiafrika. Sisi ni Ndivyo Tulivyo, period.
Hii ni aina mojawapo ya Ufisadi
 
Shadow, unajua TZ vitu huwa vinafanywa kimchezo mchezo, unaweza kuta huo mkanda ulikuwepo, ila kuanza kumuonesha wanaona ni usumbufu manake katika huo upotevu hawaathiriki kitu...

...na wala si ajabu cctv cameras zao wamezielekeza kwenye vyoo vya kina mama 'kupiga bodi' na mikanda imechukuliwa na bosi kurekodia harusi ya mwanae.. 🙁 wanaudhi kweli!!!
 
... Huu wizi wa vifaa vya hospitali, mfano huu wa kuiba mashine ya saratani, ni ujinga wa mtanzania.

MBU,
Mtazamo wako si sahihi.
Kwani ocean road ni watanzania pekee wanafanya kazi hapo?
Waza sawa sawa MBU.
 
MBU,
Mtazamo wako si sahihi.
Kwani ocean road ni watanzania pekee wanafanya kazi hapo?
Waza sawa sawa MBU.

...😱 EJM, hebu nihabarishe hao ma foreigners wanaoweza kuiba kifaa hicho hapo! nipe mwanga, nipo kizani!!!
 
Mambo haya ya kuiba vifaa vinavyosaidia jamii, kama inatokea kule China, Hukumu yao ni risasi mpaka wafe...!

Wizi huu ni sawa na kuwahukumu kifo wagonjwa wote waliokuwa wanatarajia matibabu pale Hospitalini. Haya ni mauwaji ya kukusudia.
 
Ocean Road yanunua vifaa vingine

na Deogratius Temba

TAASISI ya kutibu magonjwa ya saratani ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam, juzi ilituma fedha nchini Canada kwa ajili ya kununua vifaa vya kompyuta za kuongozea mashine za kutibu wagonjwa vilivyoibwa.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya dola 14,000 (sh milioni 18), viliibwa mwishoni mwa wiki iliyopita hospitalini hapo na kusababisha huduma za kuwatibu wagonjwa wapatao 200 wa saratani kukwama.

Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dk. Twalib Ngoma, alisema walituma pesa hizo juzi na zilitarajiwa kufika nchini Canada siku hiyo mchana.

Dk. Ngoma, alisema vifaa hivyo vinatarajiwa kuwasili muda wowote kutegemea na uharaka wa kuvipakia huko na muda vitakapochukua.

Alisema walichofanya ni kuchukua fedha na kuambatanisha na maelezo kama yaliyokuwa yametumwa na kampuni hiyo pekee inayotengeneza vifaa vya mashine za saratani, ya Best Theratronic ya Canada.

Vifaa hivyo vya kompyuta mbili zinazoongoza mashine za kutibu wagonjwa wa saratani viliibwa katika chumba maalumu cha kutibu wagonjwa hao, usiku wa kuamkia Januari 30 mwaka huu.

Tayari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, amekiri kuwa wafanyakazi wanne wa taasisi hiyo walikuwa wakishikiliwa na polisi kwa mahojiano.

Source: Ocean Road yanunua vifaa vingine
 
Back
Top Bottom