Ujio mpya wa muimbaji wa Rose Muhando umefufua matumaini mapya kwa washabiki wake

Ujio mpya wa muimbaji wa Rose Muhando umefufua matumaini mapya kwa washabiki wake

Benaya-

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2019
Posts
4,415
Reaction score
7,631
Ujio mpya wa muimbaji wa Rose Muhando umefufua matumaini mapya kwa washabiki wake ambao walikosa matumaini baada ya muimbaji huyu kupitia misukosuko mingi ya kimaisha na kijamii.

Akiwa katika studio za Wasafitv, dada Rose ameimba kwa hisia na mguso wa hali ya juu, jambo ambalo limewagusa wengi pamoja na watangazaji wa kipindi hiki cha dini yaani Lilian Mwasha na Emanuel Mgaya a.k.a Masanja mkandamizaji.

Jambo hili limenigusa mimi binafsi, hivyo namtakia mafanikio katika safari yake mpya ya huduma hii ya uimbaji.

Shukrani ziwaendee Watumishi wa Kenya waliomwinua kutoka matopeni, wakamfuta na wakamtia moyo kuwa ##anaweza kusimama tena##

Kwetu Watanzania hatunaga muda wa kutengeneza bali kula vilivyo tayari na KUBOMOA.

Mungu atusaidie, Mungu amsimamie Rose...Amen

 
Pitia link hapo juu ujionee mwenyewe
 
Ni mwimbaji mzuri na aliyevutia wengi sana kuingia kwenye huduma hiyo. Kuteleza si kuanguka. Ajifunze kutokana na makosa yaliyompoteza katika huduma yake. Nakuombea Mungu akusaidie asimame imara.
Kuna jambo wengi wetu huwa tuna kosea mapema.

Alipoanza huduma, kuna watu walijifanya wadhamini kumbe ni wachumia tumbo, alijiingiza mzima mzima na jamaa alimtumia kadiri apendavyo.

Rose aliona akijitoa kwake angeshindwa kusonga mbele, ulifika wakati alitamani kujitoa lkn alishindwa kwani alijikuta kwenye kina kirefu.

Ilimpa msongo wa mawazo akajikuta snachukua maamuzi magumu hadi kutumia yale MAKITU a.k.a chid benz.
Asgukuriwe Mungu aliyemkumbuka tena.
 
Alikuwa na tatizo gani mbona kawa hivyo jamani
 
Back
Top Bottom