Ujio wa Masihi katika Soka la Tanzania

Ujio wa Masihi katika Soka la Tanzania

Nimeiangalia Yanga ya msimu jana iliyotolewa na Rivers United, nimeiangalia Yanga ya msimu huu iliyotolewa na Al Hilal, naweza kusema timu haikua mbovu isipokua ilikosa imani.

Nilishawahi kusema linapokuja suala la mechi za kimataifa Yanga siyo mbovu, isipokuwa inakosa ile 'breakthrough moment' ya kuwafunulia wachezaji na kuamini kwamba inawezekana. Sioni tena ni kwa namna gani wapinzani wataweza kuizuia Yanga huko mbeleni

Amini nakwambia, historia italikumbuka goli la Aziz Ki kama 'turning point' ya wananchi katika michuano ya kimataifa. Nakuakikishia Yanga ndiyo itakua timu ya kwanza kuleta Kombe la CAF Championship/Confederation katika ardhi ya nchi hii.

Watanzania tembeeni kifua mbele kwa maana Masihi amerudi, mkombozi wa soka letu amekuja kuleta makombe ya kimataifa na kuondoa ule utamaduni wa jirani kushangilia kufika robo fainali.
Hapo kwenye breakthrough nakukubalia
 
Back
Top Bottom