Ujio wa simu wa smartphone, imefanya baadhi ya mambo kukosa ushabiki

Ujio wa simu wa smartphone, imefanya baadhi ya mambo kukosa ushabiki

Uhuru24

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
4,112
Reaction score
4,361
Ukweli mchungu, ila tokea utambulisho wa simu janja(smart phone) kwakweli kuna baadhi ya mambo/vitu vimeanza kukosa ushabiki kwa kasi ya hatari sana.

Ni ukweli usiopinginga vitu kama kuasikiliza muziki, kuangalia movie, kuangalia TV naona kila UCHWAO ushawishi unazidi kushuka kwa kasi sana. Sasa hivi hata wasanii (wanamuziki) hawafuatiliwi kabisa pindi wanapotoa nyimbo zao tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Tuje kwenye television ndio kabisa I nafika hatua watu hata kulipia king'amuzi wanaona ni kupoteza hela tu na nguvu kuziwekeza kwenye simu janja (smartphone).

Huko kwenye upande wa redio ndio kabisa, yaan sasa hivi watu wanachosikiliza ni kipindi cha michezo tu, na kikubwa kinachowapeleka huko sio kuasikiliza uchambuzi bali ni umbea wa SIMBA na Yanga, kikiisha basi kila mtu anageuza kitako na kuachana na redio na kuendelea na simu yake.

Sijagusia kwenye magazeti, majarida, Internet cafe na N.K.

NAITAZAMA MIAKA 10 IJAYO YA SMARTPHONE, SIJUI TUTAKUWA WAPI. "" maendeleo hayana chama ""
tapatalk_1603779152690.jpg
 
Kuna wamama wa sinema zetu na tamthilia gani sijui....usilipie kingamuzi uone moto wake
 
Tutakua kama huyo ndege hapo juu kila kitu tutamaliza wenyewe.
 
Maofisini kule kuna tv, maduka makubwa kuna tv, vijiwe vya kahawa kuna tv wote wanafuatlia habari.
Kuna kaya ndiyo zimevuta umeme television kwao ni ugeni, kuna madogo wamemaliza shule na vyuo hawana michongo wanakesha kutizama tv(muvi, siwema zetu, huna, bongo star search, sultan,).
Raia kila kukicha wanasafiri humo kwenye mabasi ni muziki na muvi, idadi ya waliopo kijijini ambao hakuna umeme wanasikiliza redio na nyimbo zilizo kwenye simu, kwa kifupi mambo yako vilevile, au labda nitakuwa sijaelewa point yako.
 
Back
Top Bottom