Kesho kutakuwa na msafara wa viongozi wa TCU na Wizara ya Elimu(MOEVT) utakaotembelea ofisi za DAAD, mjini Bonn nchini Ujerumani. Msafara huu utaongozwa na Katibu mkuu Wizara ya Elimu pamoja na kiongozi mkubwa wa TCU. swala hasa ni kuhusiana na ufadhili unaotolewa na wizara ya elimu pamoja na DAAD kwa masomo ya PhD, kwa wahadhiri wa kitanzania nchini Ujerumani.
ufadhili huu umegubikwa na tatizo kubwa la ucheleweshaji wa fedha toka Tanzania, kila mara likihahidiwa kutatolewa. Kwa mara nyingine tena hili tatizo limejirudia tena kipindi hiki ambapo mwaka wa kwanza ambao walitakiwa walipwe hela za miezi mitatu tangu Septemba mwishoni, mpaka leo hawajalipwa. Mbaya zaidi kulikuwa hakuna taarifa zilizotolewa toka Tanzania kwa wanafunzi hao walioko Ujerumani lini hela zitatumwa au kwanini zimechelewa.
swali kwa viongozi hao wanaokuja, wanakuja kufanya nini Ujerumani wakati tatizo kuu halitajatatuliwa? Je kuna tatizo gani linalofanya mara nyingi hela zichelewe? Je wanajua huo uchelewashaji unavyoathiri wanafunzi hao , ukizingatia wako nchi ya Ugenini?