Dr. Zaganza
JF-Expert Member
- Jul 15, 2014
- 1,814
- 2,738
Kutokea uzoefu wa elimu ya mimea tiba na uhusiano wake na elimu ya viungo vya mwili vilipo(Anatomy) na elimu ya mwili unavofanya kazi (Physiology), Huu ni muunganiko wa maarifa mengi yaliyo katika taarifa za kisayansi. Kwa mfano leo tuelezee uwezo-tiba wa Mjafari (Zanthoxylum chalybeum), lakini kwa kemia-dawa kuna taarifa zifuatazo:
1. Histamine H-2 receptor antagonist (H2-blocker) = Inadhibiti uzalishaji wa Histamine H-2 ambayo ni kisababishi cha vidonda vya tumbo na changamoto katika Tiba ya vidonda vya tumbo
2. Cyclooxygenase 2 inhibitor = inazuia uzalishaji wa prostaglandins, leukotrienes na Thromboxanes (sawa na NSAIDS kama aspirin, paracetamol, ibuprofen n.k)
3. Inadhibiti na kuzuia kuzaliana baadhi ya bakteria, fangasi na virusi vya maradhi
4. Inadhibiti na kuzuia kuzaliana kwa parasites wa malaria, amoebas, giardia
5. Inarekebisha mfumo wa hormones za kike na kiume
6. Inaathiri ukuaji na kuongezeka chembehai zenye saratani.