Ujue mzimu wa Kempanju wa ukoo wa Abashambo wa Kiziba, Misenyi

Ujue mzimu wa Kempanju wa ukoo wa Abashambo wa Kiziba, Misenyi

ulimi waupanga

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2014
Posts
493
Reaction score
1,223
Miaka ya 1800's walikuwepo ndugu wawili kwa Majina ya KEMPANJU NA KASSA, huko mkoani Kagera wilaya ya Bukoba( Misenyi kwa sasa).

Imenichukua mwendo wa lisaa kutoka Bukoba mjini mpaka kata ya Buyango, kijiji Lwamachu kitongoji Nyakihanga ambapo ndiko haswa nyumbani kwa ayo majina mawili ambayo moja wapo( KEMPANJU) ndiyo chanzo cha safari yangu baada ya kusikia kuwa huyo mtu alikuwa na nguvu kubwa sana za kimizimu baada ya kifo chake.

Baada ya kufika apo kijijini lwamachu nikaelekezwa kwa Kempanju, kwa mwonekano ilionekana ni familia yenye heri kimaisha lakini ikiwa ina watu wachache. Baada ya kujitambulisha kwa mwenyeji wangu ambaye alikuwa ni mama wa makamo na kumwambia kuwa nahitaji kufahamu machache kuhusu huyu mtu KEMPANJU alionekana kusutuka na kunijibu " Mwanangu mimi apa ni mwolewaji tu wala hapa ulipo siyo Nyaruju( Ikuru) ya huyo Mzee" nikaendelea kumdadisi akanambia" Nitakuongoza mpaka kwa Mzee Marceli huyu ndiye atakupatia taarifa zote".

Baada ya mwendo kama Nusu kirometa katikati ya Mashamba ya Migomba tunafika Kwenye familia moja, anaishi Mzee mmoja na vijana watatu, kumbe huyu ndiye Mzee Marceli. Baada ya kujitambulisha kwingi na maswali Lukuki Mzee anakubali kunimegea historia ya huyu mtu KEMPANJU. Anasema:

KEMPENJU NA KASSA walikuwa ni ndugu wa damu wajukuu wa mtu mmoja aliyekuwa anaitwa KASHASHA Mwenye hasili ya Mpololo Uganda aliyehamia Bukoba kipindi cha mfalme mmoja wa Kiziba aliyeshindwa kupata mtoto akashauliwa kwamba Uganda kuna mganga anaweza kumsaidia. Hapo ndo KASHASHA NA Nduguye KALENGE walipopata nafasi ya kuvuka mto Kagera na kuingia Kiziba kwa ajili ya kumtibu mfalme. Baada ya kazi yao kufanikiwa ndipo mfalme akawakabidhi eneo la kuishi mmoja akapewa kata ya Kitobo uyo KALENGE, na KASHASHA akapewa Kantale kata ya Bwanjai.

Baada ya KASHASHA Kuongezeka sana na kusitawi, vizazi vyake vilianza kujitanua, ndipo mmoja kati ya watoto wake alihamia kijiji jirani cha Lwamachu kitongoji Nyakihanga apo ndo akazaa watoto wawili KEMPANJU NA KASSA. Huyu KEMPANJU akalithi mikoba ya Uganga ya Babu yake KASHASHA na kustawi sana katika fani ya Uganga na utabiri.

Mzee Marceli anaendelea kusimulia kwamba" Maisha yaliendelea vizuri apo kijijini kati ya hawa ndugu wawili huku wakiishi maisha ya kijamaa, kiasi kwamba KASSA akichinja Mbuzi au Ng'ombe lazima nusu ipelekwe kwa Kaka yake KEMPANJU na huyu naye hivyo hivyo. Anasema, KEMPANJU katika Uganga wake alikuwa na mwiko(ekihagale) mmoja ambao ni kutokula chakula kilichoguswa na mtu mwenye ( ebishoona) kwa tafsiri hisiyo rasmi sana huu ni ugonjwa kama Ukurutu.

Shida ilikuja ambapo siku moja KASSA alichinja mbuzi kama kawaida yao akamwagiza mwanae akate nyama kwa ajili ya kumpelekea KEMPANJU, huyu mwanaye KASSA alikuwa na mke ambaye kwa siku alikuwa ameugua huo ugonjwa wa Ebishoona lakini akawa amejificha maana kipindi hicho ilikuwa kama laana mtu kuonekana na ugonjwa huo. Kwahiyo huyo kijana wa KASSA naye akamwambie mke wake akate nyama kama alivyoagiza Mzee KASSA iende kwa KEMPANJU.

Huyu mama mwenye Ugonjwa akafanya kama alivyoagizwa na mumewe na mboga ikapelekwa kwa KEMPANJU, KEMPANJU bila kujua kama ile nyama imeguswa na mtu najisi akapikiwa na kula, alipokula ile nyama hapo hapo akafariki Dunia. Kuanzia hapo ndipo Mizimu( enchweke) ya KEMPANJU ilipoanza sarakasi zake.

Anaendelea kusimlia kuwa" Ile Siku wamemaliza kumzika Mzee KEMPANJU, siku iyo iyo wazee wote walipandisha roho vichwani na kuanza kunena kwa sauti ya Marehemu akilia na kusema kwa ukali" watata wakunyisile?" Yaani (ndugu yangu wewe ndiye ungeniua?), ikabidi KASSA adakie na kuuliza maana yeye alikuwa hajapandwa na roho ya Marehemu ( enchweke), watata nakwita ntai? Yaani ( ndugu yangu nimekuua vipi), Ile roho kwa vinywa vya wale wazee ikazidi kunena " watata nomanya okwo ntalya bihagalo, kyonkai wandetela ebihagalo byanyita" yaani( ndugu yangu unajua sili najisi lakini wewe umeniletea najisi nimekula na kufariki).

Hapo hapo ile roho kupitia vinywa vya wale wazee ikasema " kuanzia Leo naweka uhasama kati ya KEMPANJU na KASSA aliye wa KASSA akikanyaga aridhi ya KEMPANJU atakufa, hata mbuzi au kuku aliye wa KASSA hasikanyage kwa KEMPANJU...........!

Itaendelea....................!
 
ila bukoba kuna mizimu mingi na bado wana abudu tamaduni zao (nawaunga mkono 100%) pia dawa za mitishamba huuzwa sana hata mjini utakuta wanatembeza.

na waganga wao wengi ni wakweli sana tofauti na sehemu nyingine
 
Samahani wadau sikuweze kuleta mwendelezo wa historia yetu ya MZIMU WA KEMPANJU kwa wakati, lakini ngoja Leo tupate mwendelezo wake:

SEHEMU YA PILI YA SIMULIZI KUHUSU MZIMU WA KEMPANJU

Mzee Mariceli anaendelea kusimulia kuwa baada ya ile roho ya marehemu KEMPANJU kuwatoka wale wazee ilimbidi KASSA na walio wake waondoke pale msibani na kuelekea katika mashamba yao yaliyo upande wa mashariki mwa mashamba ya KEMPANJU.

Anaendelea kusema, KASSA aliendelea kutii yale maagizo ya roho( nchweke) ya kaka yake kwamba aliye wake(KASSA) hasiguse au kusogelea Eneo la KEMPANJU na hii ilikuwa ni laana ya milele. Bahati mbaya baada ya mda kidogo kupita kama unavyojua ni vigumu kuwazuia watoto wasicheze na wenzao, kila mtoto wa tumbo la KASSA aliyetambuka mipaka na kukanyaga aridhi ya KEMPANJU alipoteza maisha hapo hapo. Anasema ndani ya mwaka mmoja KASSA alipoteza jumla ya watu 12 na mifugo mingi sana maana ilikuwa hata mbuzi akikata kamba akikanyaga tu aridhi ya KEMPANJU anakauka hapo hapo.

Maisha yalizidi kuwa magumu kwa KASSA na watu wake maana kwa geografia ilivyo, ili mtu atoke kwa KASSA aende labda hospitali au kisimani kuchota maji hana budi kukatiza mashamba ya KEMPANJU, hivyo basi iliwabidi wazunguke kijiji upande wa kusini umbali wa kilometa kama 4 ili wapate kuingiliana na jamii ambapo kama wangepita kwa KEMPANJU ni chini ya mita 600.

Anasema, mwaka mmoja baadaye Mzee KASSA aliwaita vijana wake kuwapo wosia kwamba" wanangu kwa jinsi navyomjua kaka yangu bila kuchukua hatua mapema anakwenda kunifuta katika uso wa dunia maana yeye( alya akajunzile) kwa tafisiri hisiyo sahihj sana kwamba ni mtu wa visasi." Mzee KASSA aliamua kusafiri kwenda kijiji cha mbali cha Bukabuye kwa mganga mmoja rafiki yake wa karibu na KEMPANJU aliyeitwa KAIYURA MKUBA ( yaani Mtuma radi). Kisa cha kwenda kwa yule mganga ni vile aliamini hakuna mganga Duniani awezaye kutengua mitego ya KEMPANJU hisipokuwa huyu rafiki yake kwamba rabda anaweza jua madhaifu ya KEMPANJU.

Baada ya kufika kwa huyo Mganga, bwana Kaiyura Nkuba alisikitika sana na kumwambia, kwa kile alichokitega ndugu yake hakuna mwanadamu wa kukitegua hisipokuwa miungu ya Mpololo Uganda. Hivyo basi alimshauli asafiri kuelekea Uganda aende Kwenye Mizimu yao uko Mpololo ambako akifanya mitambiko inayofaa anaweza kuongea na KEMPANJU akamwomba msamaha.

Mzee KASSA alirejea nyumbani kwake na kufunga safari yeye na watu wake wote kuelekea Mpololo Uganda kwa ajili ya Tambiko la Msamaha. Ilikuwa safari ndefu ya wiki nzima kufika katika Eneo la tukio. Baada ya kufika na kufanya matambiko, Roho ya KEMPANJU ikajibu na kusema" Kwa vile ndugu yangu ulimwaga damu yangu na Mimi nahitaji Damu yako lakini hisiyo najisi na iwe safi na ya kike, akaendela kusema pamoja na iyo damu yako nataka utafute Mafahari matatu yaliyonona unitolee sadaka yachinjwe yakielekezwa kwako na nyama yake yote na maungo yake yote yasiliwe na mtu Bali yachomwe mishikaki kwa kuchomekwa Kwenye mipaka ya uwanja wa nyumba yangu pande zote mbili kwa muda wa siku tatu ili harufu yake itamaraki Eneo zima ili atakayepita kati ke mbwa au kagwantora ajue KEMPANJU nimerudi." Akamalizia kwa kusema ukiyafanya ayo yote katika usahihi wake ndipo nitakapo kusamehe wewe na walio wako na hata nisikumbuke hasira yangu juu yako.

Itandelea..............!
 
Historia nzuri sana japokuwa sikuwahi kuisikia kabla,na ninatokea kabisa kijiji cha Kantale kata ya Bwanjai na hata nikifa leo nitazikwa Kantale. Itabidi nimuulize babu yangu kuhusu huu mkasa.
 
Kempanju ana nongwa sana kwani ndugu yake alijua mkwelima wake ana ukoma? Makosa ya mtoto ambae aliambiwa kata nyama kamtuma mkewe
 
Aisee historia nzuri sana ntaifuatiria ila nilihitaji kujua chimbuko la Ikimba na mengine mengi
Hizi ndyo stori wajukuu wanahitaji kuzipata
IMG-20190914-WA0161.jpeg
 
Samahani wadau sikuweze kuleta mwendelezo wa historia yetu ya MZIMU WA KEMPANJU kwa wakati, lakini ngoja Leo tupate mwendelezo wake:

SEHEMU YA PILI YA SIMULIZI KUHUSU MZIMU WA KEMPANJU

Mzee Mariceli anaendelea kusimulia kuwa baada ya ile roho ya marehemu KEMPANJU kuwatoka wale wazee ilimbidi KASSA na walio wake waondoke pale msibani na kuelekea katika mashamba yao yaliyo upande wa mashariki mwa mashamba ya KEMPANJU.

Anaendelea kusema, KASSA aliendelea kutii yale maagizo ya roho( nchweke) ya kaka yake kwamba aliye wake(KASSA) hasiguse au kusogelea Eneo la KEMPANJU na hii ilikuwa ni laana ya milele. Bahati mbaya baada ya mda kidogo kupita kama unavyojua ni vigumu kuwazuia watoto wasicheze na wenzao, kila mtoto wa tumbo la KASSA aliyetambuka mipaka na kukanyaga aridhi ya KEMPANJU alipoteza maisha hapo hapo. Anasema ndani ya mwaka mmoja KASSA alipoteza jumla ya watu 12 na mifugo mingi sana maana ilikuwa hata mbuzi akikata kamba akikanyaga tu aridhi ya KEMPANJU anakauka hapo hapo.

Maisha yalizidi kuwa magumu kwa KASSA na watu wake maana kwa geografia ilivyo, ili mtu atoke kwa KASSA aende labda hospitali au kisimani kuchota maji hana budi kukatiza mashamba ya KEMPANJU, hivyo basi iliwabidi wazunguke kijiji upande wa kusini umbali wa kilometa kama 4 ili wapate kuingiliana na jamii ambapo kama wangepita kwa KEMPANJU ni chini ya mita 600.

Anasema, mwaka mmoja baadaye Mzee KASSA aliwaita vijana wake kuwapo wosia kwamba" wanangu kwa jinsi navyomjua kaka yangu bila kuchukua hatua mapema anakwenda kunifuta katika uso wa dunia maana yeye( alya akajunzile) kwa tafisiri hisiyo sahihj sana kwamba ni mtu wa visasi." Mzee KASSA aliamua kusafiri kwenda kijiji cha mbali cha Bukabuye kwa mganga mmoja rafiki yake wa karibu na KEMPANJU aliyeitwa KAIYURA MKUBA ( yaani Mtuma radi). Kisa cha kwenda kwa yule mganga ni vile aliamini hakuna mganga Duniani awezaye kutengua mitego ya KEMPANJU hisipokuwa huyu rafiki yake kwamba rabda anaweza jua madhaifu ya KEMPANJU.

Baada ya kufika kwa huyo Mganga, bwana Kaiyura Nkuba alisikitika sana na kumwambia, kwa kile alichokitega ndugu yake hakuna mwanadamu wa kukitegua hisipokuwa miungu ya Mpololo Uganda. Hivyo basi alimshauli asafiri kuelekea Uganda aende Kwenye Mizimu yao uko Mpololo ambako akifanya mitambiko inayofaa anaweza kuongea na KEMPANJU akamwomba msamaha.

Mzee KASSA alirejea nyumbani kwake na kufunga safari yeye na watu wake wote kuelekea Mpololo Uganda kwa ajili ya Tambiko la Msamaha. Ilikuwa safari ndefu ya wiki nzima kufika katika Eneo la tukio. Baada ya kufika na kufanya matambiko, Roho ya KEMPANJU ikajibu na kusema" Kwa vile ndugu yangu ulimwaga damu yangu na Mimi nahitaji Damu yako lakini hisiyo najisi na iwe safi na ya kike, akaendela kusema pamoja na iyo damu yako nataka utafute Mafahari matatu yaliyonona unitolee sadaka yachinjwe yakielekezwa kwako na nyama yake yote na maungo yake yote yasiliwe na mtu Bali yachomwe mishikaki kwa kuchomekwa Kwenye mipaka ya uwanja wa nyumba yangu pande zote mbili kwa muda wa siku tatu ili harufu yake itamaraki Eneo zima ili atakayepita kati ke mbwa au kagwantora ajue KEMPANJU nimerudi." Akamalizia kwa kusema ukiyafanya ayo yote katika usahihi wake ndipo nitakapo kusamehe wewe na walio wako na hata nisikumbuke hasira yangu juu yako.

Itandelea..............!
Mjukuu wa kempanju umetoka mbio
 
SEHEMU YA TATU

Mzee marceli anaendelea kusimulia kuwa: Baada ya Mzee KASSA na watu wake kupokea ayo maagizo ya Roho ya KEMPANJU walianza kufanya safari kuelekea kijijini Nyakihanga wakitokea uko Mpololo. Anasema walipofika waliandaa sherehe iyo ya matambiko iliyohusisha watu wote katika ukoo, uku ule uzao wa KASSA wakiingia kama uonavyo bibi harusi aingiavyo ukumbini akiwa na msururu wa watu akisindikizwa kwa nyimbo na tarumbeta nao uzao wa KASSA ndivyo walivyongia nyumbani kwa KEMPANJU.

Anasema baada ya Kufika kwa KEMPANJU hawakurusiwa kuingia ndani ya nyumba maana walikuwa najisi bado mbele ya KEMPANJU kwahiyo ilibidi waanze kufanya matambiko Mara moja ili kutuliza gadhabu ya Roho ya KEMPANJU maana kwa mda huo vijana wote wa tumbo la KEMPANJU walikuwa wamepandisha iyo roho ikifoka na ikitishia kwa kusema( nyite ente yange bugondo mbone?) Yaani Niue ng'ombe wangu bugondo msuhudie? Huku wazee wa ukoo wakiitikia kwa kusujudu mpaka chini ( waitu otaita otaita) yaani baba husiue husiue. Mzee Marceli anasema ile kusema ng'ombe wangu Bugondo alimaanisha ndugu yake KASSA ndiyo maana waliomba sanaaa mpaka kutoa machozi.

Waliaza kufanya Tambiko la upatanisho kwa kuwachinja mafahari watatu walionona uku shingo zao zikielekezwa mashariki mwa Eneo la KEMPANJU ambako ndiko nyumbani kwa KASSA kama KEMPANJU mwenyewe alivyoagiza. Anasema, kwa vile machinjio yalikuwa karibu na mpaka damu ilipovuka mpaka na kuingia katika aridhi ya KASSA ilikauka papo hapo jambo lilofanya watoa sadaka kuamini kuwa ilikuwa ikimezwa na KEMPANJU mwenyewe. Anasema nyama yote ilichomwa mishikaki kwa kusimikwa pande zote za( ekibuga) uwanja wa nyumba ya KEMPANJU kwa muda wa siku tatu usiku na mchana.

Baada ya kufanya ilo tambiko ilimbidi KASSA kumtolea kaka yake kempanju damu yake kama alivyoagiza mwenyewe, hivyo basi ndani ya Tumbo la KASSA hakuwepo binti aliyekuwa bikira na wala hasiye na ukurutu isipokuwa binti mdogo Wa miaka 15 aliyeitwa JEREME.

Hivyo basi Mzee KASSA alimchukua mjukuu wake uyo mchanga na kumpeleka juu ya kaburi la KEMPANJU na kusema( owatata nakuletela obwamba bwange obutole bukwogye omutima ongalule, nkule mmelele nkole uruganda.) Yaani ndugu yangu nimekuletea damu yangu, uipokee ikusafishe roho yako unisamehe, ili niongezeke na kutengeneza ukoo. Watu wote walijua uyo binti atakauka hapo hapo kwa vile alikuwa katolewa kama sadaka ya Malipizi.

Gafla sauti ya KEMPANJU ikasikika ikiwatoka wale vijana wote waliokuwa wamepandwa na roho yake tangu majuzi bila kula wala kunywa, ikisema: Ndugu yangu kwa vile sikubahatika kupata mtoto wa kike, kuanzia Leo Jereme ni mwanangu, hasikanyage kwako bila ruhusa yangu wala hasilale na mwanaume maisha yake yote Bali atakuwa ni muhudumu wa( ekirugu) madhabahu yangu siku zote za maisha yake yote. Anaendelea kusema, kwa sadaka hii nimekusamehe wewe na uzao wako wote lakini kila mtoto wa kiume kati ya tumbo langu na lako atakayezaliwa akiwa hana kasoro ya kimaumbile atavimba magoti( ebishona) iyo itakuwa ni ishara yangu kwako kwamba nimesamehe makosa yako juu yangu. Mzee marceli anasema mpaka Leo hii vijana wa ukoo huo wanasumbuliwa na ugonjwa huu ambao kwa uchunguzi wangu, wazungu wanauita Rhematoid athretis.

Anasema kuanzia siku iyo upatanisho baina ya ndugu hawa wawili ulipatikana na binti Jereme akahamia Kwenye hekaru( nyaruju) ya KEMPANJU akiendelea kuhudumu katika madhabahu ya KEMPANJU, ambako kila siku alikuwa akipeleka chakula hasubui na jioni na kila wakitengeneza pombe ya Kienyeji( orubisi) ilikuwa shariti pombe iwekwe Kwenye madhabau iyo.

Itaendelea...........!!!
 
SEHEMU YA NNE......!
Mzee marceli anaendelea kusimulia kwamba, maisha yaliendelea ambapo binti Jereme aliendelea kuhudumu katika madhabahu ya KEMPANJU iliyoko apo(Nyaruju) Ikulu ya ukoo. Miaka ilipita watu wakiishi kwa kutegemea mionhozo iliyokuwa ikitolewa na Mzimu wa KEMPANJU kwa kupitia vinywa vya wazawa wa kwanza. Anasema kipindi hicho mtu yeyote hasinheingiza dawa yoyote Kwenye ule ukoo maana ulikuwa ukilindwa vikali na huu mzimu, mpaka ilifika wakati kijana wa KEMPANJU akienda kuchumbia sehemu anapewa bure mke maana jamii iliamini binti yao anaenda Kwenye mikono salama.

Anasema kipindi hicho hata ndege wa angani hasingekatiza juu ya nyumba ya KEMPANJU, akijaribu tu anadondoka na ilikuwa ni kawaida kuokota ndege walioshushwa kwa mazindiko ya pale. Mwaka 1934 binti Jereme alkua na kuwa binti mkubwa tu, wazee walifanya ibada maalumu kumwomba KEMPANJU atoe ruhusu huyu binti aolewe maana alikuwa akilalamika kila siku. Baada ya maombi ya siku nyingi na sadaka za kutosha alikubali binti yake aolewe lakini kila siku hasubui arudi nyumbani kwa ajili ya kufagia kaburi lake. Alimchagulia mume wa kumuoa kwa Mzee jirani kidogo lakini wa ukoo tofauti akijulikana kama KAKUNGU.

Binti Jereme aliolewa hapo akabahatika kupata mtoto mmoja wa kiume, kama ilivyo kawaida ya wanadamu binti Jereme alipoolewa Kwenye ukoo mwingine aliambiwa hapa tuna tamaduni zetu hakuna ruhusa ya kuondoka kila siku kwenda kwenu hapa umeshaolewa tayari. Kwahiyo Jereme hakuweza kuendelea na utaratibu aliopewa na Mzimu wa KEMPANJU jambo lililomfanya KEMPANJU kuchukia na kupeleka ujumbe wa tahadhali kwa familia alikoolewa Jereme kwamba " mkiendelea kumzuia mwanangu nitakufanya wewe Kakungu wa kutanga tanga na nyumba yako itakuwa ni pori lisilokaliwa na mtu.

Kakungu alikaidi vitisho vya KEMPANJU akidai yeye ni familia huru haiwezi ingiliwa. Baada ya siku chache roho ya KEMPANJU ilipanda na kusema nimeweka uhasama kati yangu na Kakungu damu zetu hazitaingiliana, chochote chenye mchanganyiko wa hizi damu mbili hakitaishi, na Kakungu nimemfanya wakutanga tanga mpaka uzao wake wa Kumi. Kwa kusema vile radi kubwa ilipiga, bahati mbaya yule mtoto wa Jereme alipigwa na radi akiwa amebebwa mgongoni na mama yake uku aliyebeba mtoto hasiungue hata kidogo. Tangu siku hiyo familia ya Kakungu ilitaharuki na kisambaratika ikambidi binti Jereme arejee nyumbani kwa KEMPANJU anaendelea kuhudumu kama kawaida yake.

Anasema miaka iyo Mjukuu mkubwa wa KEMPANJU aliyeitwa Kahawa alio binti mmoja aliyeitwa Nana, anasema ile siku wameoana roho ya KEMPANJU ilipanda na kusema " Mwanangu huyu mwanamke uliyeoa atataka sana kushindana na Mimi maana ana mikono ya dawa sana lakini husimwache maana katika uzao wake atatoka Mwana atakayerithi mikoba yangu. Anasema baada ya miaka kupita huyu mama Nana alitaka kukabidhiwa mikoba ya uchawi na mama yake mzazi apa ndiko seke seke la ugomvi kati ya huyu mama na Mzimu wa KEMPANJU liliposhika hatamu. Nana na watu wake waliamini mtu aliyekufa tayari hawezi washinda walio hai, na KEMPANJU kwa upande wake akiweka msimamo kuwa dawa yoyote hisikanyage nyumbani kwake. Ili jambo lilimfanya Nana kuanzia kuzunguka kwa Waganga Tofauti akitafuta dawa za Kuzindika Mzimu wa KEMPANJU ili unyamaze na yeye apate Uhuru wa kufanya ushirikina wake bila bugudha.

Baada ya kuzunguka sana bila mafanikio maana waganga wengi walimwogopa KEMPANJU, aliamua kusafiri kuelekea Uganda kwa Mganga mmoja maarufu sana kipindi hicho kwa uchawi wa Vifaru na Mapembe( ekifaru na amaembe). Baada ya kufika yule mganga alimwambia huyu mtu alikufa akiwa amebugia hirizi ya mazindiko katika kinywa chake. Kwahiyo hawezi kufanywa lolote mpaka twende Kwenye kaburi lake tuchukue udongo wa upande kichwa kilipo. Nana akamwambia Mganga kwamba ilo ni gumu maana Kwenye kaburi la KEMPANJU hata lisipo limwa nyasi hazioti hata kuku akikatiza juu ya lile kaburi anakufa. Akamwambia ni mtu mmoja tu awezaye kulisogelea lile kaburi yule binti Jereme, na yeye haruhusiwi kulikanyaga au kuligusa maana aliapa kwamba kiumbe chochote chenye uhai kikikusa alikolala kitamfuata mda huo huo.
Mganga alimwambia yeye ndiye Docta atatumia majini yake mpaka achukue ule udongo. Walianza safari kuja nyumbani kwa KEMPANJU. Walipokuwa wakivuta mto Ngono walipigwa na upepo mkari sana na kwa maajabu Yule mganga akatembezwa Juu ya maji mpaka nje ya mto na kuambiwa, Leo nimekusamehe lakini siku ukiuvuka mto huu tena kuja upande wa pili utakuwa halali yangu. Baada ya siku 7 kupita kule nyumbani yule mama Nana akiwa hajulikani alipo mwanaye aliyeitwa Lukura alianza kumtafuta mama yake bila mafanikio. Ndipo KEMPANJU akapanda na kumwambia Nenda katika msitu Minziro katika mti mkubwa wa Mungu ndiko nilikomweka mama yako namlisha usiku na mchana ili asife njaa. Anaendelea kusimulia jinsi alivyotaka kumzindika ili hasiongee tena na jinsi alivyomtenda yeye na mganga wake na aliyekuwa akiwavusha Kwenye mtumbwi.

Anasema Roho iyo ya KEMPANJU iliendelea kulinda ule ukoo japo kwa ukari sana mpaka miaka ya 80 mwishoni. Lakini baada ya Mjukuu wa Yule mama mchawi Nana ambaye ndiye alitakiwa kurithi mikoba ya Uganga wa KEMPANJU kuchukiliwa na mapadri wa kanisa Katoriki kwa ajili ya kusoma upadri maana alikuwa na akiri sana na vipawa vingi sana walimpenda na kumchukua wakampeleka Seminary ya Rubya kusoma. Anasema KEMPANJU alipambana kijana arudi lakini ilishindikana mwisho wa siku aliamua kumtoa roho yule kijana akiwa shule. Na kusema kwa vile ukoo umeamua kuchagua Mungu mwingine anawaacha mpaka apo wakimkumbuka atawalinda tena.
Pamoja na matukio Mengi sana aliyosimulia Mzee Marceli anasema ni bora kipindi hicho wakati KEMPANJU akifanya kazi maana amani ilikuwepo kulikoni sasa hivi maana kila kitu kimevurugika.
 
Shukrani mkuu kwa simulizi nzuri. Umenikumbusha tulivyosimuliwa utotoni kuhusu mizimu ya kihaya ambayo huwa kwa alama ya mnyama kama simba au chui. Cha kushangaza ni wanaukoo walikuwa wanalindwa na hiyo mizimu kwa kuiona mfano usiku au sehemu hatarishi

Ila wanasema imepotea baada ya kuingia kwa dini na watu kuacha kuiabudu
 
Back
Top Bottom