Ujue mzimu wa Kempanju wa ukoo wa Abashambo wa Kiziba, Misenyi

hadithi tamu.
siku nyingine tuletee migration ya wa sudan kusini, kuingia uganda, tanzania, kupitia bukoba, kuvuka maji, kupitia kerebe, goziba, ukerewe hadi ku-settle musoma.
 
Upande huu waziba.....upande mwingine wahangiro
 
Mkuu twendelee bc inabidi wafanyaje waliobaki ili kurudisha ulinzi wa kbanjuu
 
Mbona kuna padri alikua anaitwa kempanju ila baadae aliasi upadri na kuoa au uyo ni mwingine
 
Weekend moja nikiwa na wazee fulani kijiweni mitaa ya Bukoba, walianza kusimulia kuhusu ndugu wawili waliofarakana baada ya ndugu mmoja kuvunja masharti.

Inasemekana miaka ya 1880 kuna ndugu wawili waliojulikana kwa Majina ya Kempanju na Kassa. Hawa walikuwa ni wajukuu wa Mzee mmoja mganga fundi aliyetoka Uganda kuja Kiziba kumtibu Mfalme mmoja ambaye hakubahatika kupata mtoto.

Mzee huyo Kashasha baada ya kufanikiwa kumtibu mtawala huyo wa Kiziba, alifanikiwa kupewa eneo huko Kiziba ili aweze kuanzisha makazi yake. Alijistawisha sana na hatimaye ukoo kukua. Hivyo mmoja wa wajukuu wake aliyejulikana kama Kempanju alirithishwa Uganga.

Inadaiwa Kempanju alikuwa mganga hatari aliyeogopwa sana. Sasa laana ya Kempanju kwa ndugu yake Kassa ilikuja baada ya Kassa kuvunja masharti yaliyowekwa na Kempanju na kupelekea Kempanju kufariki dunia.

Inadaiwa Kempanju kupitia mizimu yake alinuia kumaliza uzao mzima wa nduguye Kassa. Wazee wale wanasema kuwa ilikuwa patashika nguo kuchanika mpaka kuja kuvunja ile laana.

Upi ukweli kuhusu mkasa huu?
 
Eduche Edwin
 
Hii ndiyo JF tuliyokua tunapenda ....nk
Kuna vitu kwenye simurizi umekosea kuandika ila umeweza kueleweka. Ukweli tumeacha tamaduni zetu....nakumbuka enchweke,mugasha,emizimu pamoja na embandwa.Hivi vitu vilikuwepo na kufanya kazi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…