Ujue ugonjwa wa Mba na tiba yake

Regency hospital Dr. Mgonda, huwa anakuwepo jumanne, KCMC pia kuna daktari specialist wa ngozi.
 
Salaam wanajamii.

Nina matitizo ya kichwa kuwasha kwa muda mrefu sana(miaka 5). Nywele zikiwa ndefu ndio kichwa kinavyozidi kuwasha. muwasho huambatana na maumivu makali. Nikinyoa nywele afadhali hupatikana kidogo. Je huu ni ugonjwa gani? nini tiba yake?
 
Hujatuambia wewe ni Mwanamke au Mwanamme? Huenda ukawa na Mba kichwani wakati unapokuwa na hizo nywele ndefu huo mba ndipo hujitokeza na kuwashwa washwa katika kichwa chako hebu jaribu kupaka Hina katika hizo Nywele zako huenda hayo matatizo yakaondoka. Uliwahi kwenda kumuona Daktari..............?
 
Mabaka:
Je, kuna dawa ya mabaka ya usoni, mgongoni, kifuani?

Mba:
Dawa ya mba please.(naomba isiwe cream ya kuchubua ngozi)

Je, kwa ugonjwa huu kuna dawa za mitishamba pia, ni zipi, zinatumikaje na dosage yake ikoje.
 
Achana na mitishamba ... nenda muhimbili kamuone dermatologist
 
mbona mnaamini sana dawa za miti shamba ambazo hazina vipimo sahihi nenda hosp
 
naungana na wenzangu kukushauri umuone daktari makini. usichoke katika kuhakikisha afya yako inakuwa imara. kwa Mba, ni mba wa wapi? ni kichwani?
 
Nenda pale Regency kuna Daktari wa ngozi kila jumatatu.
 
Matatizo mengi ya ngozi licha ya uambukizo yanatokana na ulaji usio na mpangilio. kutokula matunda na mboga za majani mchanganyiko husababisha matatizo mengi kwa ngozi na mfumo wa damu. Hivyo basi wakati unaelekea kupata vipimo kwa madaktari jitahidi sana kula mboga mchanganyiko (salad aka kachumbari) pia tengeneza na kunywa sharubati ya matunda mchanganyiko (raw fruit juice) pata aina za mboga tofauti si pungufu ya tano na aina za matunda zisizopungua sita. (hakikisha katika matunda unayopata kuna jamii ya tango, parachichi na limau, na pia usiweke matunda ya jamii moja katika mfumo huo wa juice. Pia katika mboga hakikisha kukosi koli japo kipande kidogo sana) Tumia (juice hiyo kila asubuhi mchana na jioni. na salad iwe katika kila mlo wako wa usiku)

Epuka kutumia dawa za mitaani au kununua bila maelekezo ya daktari, pia chunguza aina za loshen unazotumia inaweza kuwa sababu.
 
Wadau!

Kwa miezi mitatu sasa nasumbuliwa na mapele ya ndevu baada ya kunyoa kwa kutumia Magic, na nimeshatumia Dawa tofauti tofauti lakini bado sijapata solution.

Ni wapi kwa hapa Dar naweza kupata Dr Proffesional kwa ajili ya hili tatizo.

Nitashukuru!
 
mkuu nenda pale SH Amon kuna dawa moja inaitwa Bump patrol, hiyo ni fasta yanaisha. price yake ni arround 9000 sh. Mi ndo huwa natumia hiyo,iko bomba
 
Kuna hospitali inapatikana maeneo ya Tegeta, Kanisa katoliki wao ni wataalamu wa maswala ya ngozi tu wanaweza kukusaidia tatizo lako.
 
Kama shida ni Dk wa ngozi nenda Kairuki Hosp Mikocheni ulizia Dk Kishengere, ni mtaalamu sana wa ngozi. Ila huwa anakuwa na wagonjwa wengi sana. Waweza ongea nae akuelekeze hosp nyingine za private anazofanya, coz pale huwa anapatikana j.nne na jmosi jioni tu.
 
Asanteni wadau!
Nahitaji kuonana na Dr
Coz hizo Bump Patrol, Vaya, sabuni na mafuta yake nishatumia hali inaisha ndevu zikianza kuota na vipele vinaanza kujitokeza.
 
i. Mwarobaini Ndizi. *(tineakoporisi)

  • majani ya mwarobaini
  • ndizi moja iliyoiva sana
Chemsha mwarobini, pondandizi iliyoiva sana, kisha changanya maji ya mwarobini.
Matumizi:
Paka mwiliwote oga baada nusu saa mara 2 kila siku, kwa muda wa wiki 2.
ii. Kitunguu maji. *(tinea vesikola)

Kunywa juisiya kitunguu maji glasi 3 kila siku, pia paka kitunguu maji sehemu iliyoathirikamuda wa wiki 2.
iii. Hina na bizari *(funguskatikati ya vidole vya miguu)

Ponda majani ya hina na mizizi ya bizarikwa pamoja.
Matumizi:
Paka sehemu zilizoathirika asubuhi najioni muda wiki 2.
iv. Mdalasini asali. *(funguskatikati ya vidole vya miguu)

§ Kijiko 1 cha chakula cha mdalasini
§ kijiko 1 cha chakula cha asali.
changanya
Matumizi:
Paka sehemu iliyoathirika osha baada saa 1 fanya kabla ya kwenda kulalawiki 1.
v. Mshubiri (aloe vera) na mafutaya nazi.
Pondaponda jani la mshubirikisha kamua maji maji yake chemsha pamoja na mafuta ya nazi.
Matumizi:
Paka sehemu zilizoathirika na mba.
vi. Majaniya mwarubaini.
Kausha majani ya mwarubaini, kisha saga upate ungalaini uchanganye na mafuta mgando.
Matumizi:
Paka mafuta hayo mara 2.Kumbuka kufua nguo kwa maji ya moto ili kuua vimelea vya ugonjwa.
vii. Kitunguu maji na tambuu.
Changanya kiasi kinacholinganacha juisi ya kitunguu na juisi ya majani ya tambuu.
Matumizi:
Paka kwa muda wa siku10.
 
Salaam Wadau!

Hivi jamani wapi naweza kupata daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi hapa jijini Dsm? Nimezunguka Ocean Road na Hindu Mandal ila naona wote fix tu. kwanza hawajajaribu kufanya vipimo vyovyote juu ya ugonjwa wangu, wao wanapima kwa macho na kunipa madawa hayohayo kila siku ila kwa masharti tofauti. Wapi au hospitali gani wanaweza kunifanyia vipimo na kunipa tiba sahihi?

Nawasilisha!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…