SoC02 Ujue ugonjwa wa UTI Kisha jikinge

SoC02 Ujue ugonjwa wa UTI Kisha jikinge

Stories of Change - 2022 Competition

Dr Yesaaya

Member
Joined
Jul 25, 2022
Posts
9
Reaction score
24
Jiepushe na Maambukizi katika njia ya mkojo kitaalamu – UTI (Urinary Tract Infections)

Anaandika Dr MSANGY. 0752591744/0682080069

UTI – Ni maambukizi ya vimelea vya magonjwa katika mfumo wa mkojo – kuanzia katika figo (kidneys) unapochujwa mkojo hadi katika sehemu ya kukojoa yaan urethra. UTI huwapata watu zaidi ya watu million 150 duniani kwa mwaka, na huwaathiri zaidi wanawake kuliko wanaume (sababu za kimaumbile).
zaidi ya asilimia 10 ya wanawake wote hupata UTI kwa mwaka.
Zaidi ya 50% ya wanawake wamewahi kupata ugonjwa huu katika maisha yao zaidi sana kati ya miaka 16-35. Ugonjwa huu uligundulika yapata miaka ya 1550 kabla ya kristo. (BC)

Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na
  • Maumivu wakati wa kukojoa - (mkojo kuunguza unapotoka – burning with urination).
  • Kukojoa mara kwa mara (kidogo kidogo).
  • Kujisikia haja ya kukojoa wakati kiuhalisia kibofu hakuna mkojo.
  • Homa, kutapika, kichwa kuuma huweza kuambatana na dalili hizo
  • Maumivu ya kiuno, Na mgongo wa chini – lower back pain
  • Mkojo wenye damu (mara chache hutokea), wakati mwingine usaha kwenye mkojo
Kwa wazee na watoto wachanga dalili za UTI huweza kutatiza kuzijua(vague symptoms)

Watoto – kushindwa kuzuia mkojo – kujikojolea huweza kuwa dalili y maambuki ya uti

Sababu ziletazo UTI
  • Maambukizi ya bakteria hasa e.coli, na wakati mwingine maambukizi ya fungus kama vile Candida albicans na bakteria wengine kama Staphylococcus saprophyticus huweza kusababisha ugonjwa huu.
  • Sababu zinazoweza kuchochea (risk factors) ni pamoja na maumbile ya kike (female anatomy), kujamiiana (sexual intercourse), unene uliopitiliza(obesity), historia katika familia.
  • Ikumbukwe – uti sio ugonjwa wa zinaa hivyo usije ukamlaumu mwenzi wako kwamba ana UTI hivyo amechepuka, la hasha! ugonjwa huu zamani ulijulikana kama honey moon cystitis – maana uliwapata zaidi wenzi waliotoka kufunga ndoa sababu ilihusishwa na hali ya kukutana kimwili hasa wanapokuwa fungate.
  • Wakati mwingine UTI husababishwa na maambukizi ndani ya damu (Blood borne) na husambaa hadi kwenye figo na kuleta UTI.
  • Vilevile kwa wagonjwa waliowekewa mpira wa mkojo – catheter huwa chanzo cha bakteria waletao UTI.
  • Kujamiiana – sexual intercourse – zaidi ya asilimia 75 – 90 ya wanawake wanaoshiriki sex hupatwa na UTI, na uwezekano wa kupata huongezeka zaidi kulingana na ufanywaji wa tendo mara kwa mara. (Kama nilivyoeleza juu ya honeymoon cystitis)
  • Jinsia ya kike wako katika hatari zaidi kupata maambukiz sababu mrija wa kutolea mkojo – urethra, ni mfupi kuliko wanaume
  • Tezi dume - large prostate pia husababisha maambuzi ya UTI kuzidi kujirudia.
JINSI YA KUGUNDUA – DIAGNOSIS

Daktari atakuomba ulete mkojo ili upimwe katika maabara – urinalysis pamoja na urine microscopy. Pia kuoteshwa mkojo – urine culture – ili kugundua aina wa bakteria walioshambulia mfumo wa mkojo.

KUJIKINGA/ kuepuka – PREVENTION
  • Kunywa maji ya kutosha na vimiminika vingine kama juisi za matunda, miwa, maji ya madafu – hii husaidia kuondoa vimelea vinavyoanza kuota na kutanda katika kuta za mfumo wa mkojo. Usipokunywa maji ya kutosha angalau lita 2 na nusu kwa siku kwa mtu mzima UTI itakusumbua.
  • Epuka matumizi ya vyoo vinavyotumika na watu wengi, au hakikisha usafi wake, kabla na baada ya kutumia. – vyoo vinapotumika na watu wengi na hasa vya kukaa au kuchuchumaa huweza kuwa chanzo cha UTI, maana katika watu wengi wamo walio na maambukizi katika mkojo huacha bakteria na kuenea kwa wengine watakaotumia choo hicho. Inapobidi kutumia hicho, safisha kwa maji mengi na sabuni ndipo utumie.
  • Kukojoa kwa haraka mara umalizapo tendo la kujamiiana – hii husaidia kusafisha njia ya mkojo na kuzuia wadudu kudanda katik kuta za mfumo wa mkojo na kuleta madhara. Kojoa haraka na kuwaondoa bakteria wale amabao kwa bahati mbaya waliingia wakati wa tendo la sex
  • Kubadilisha aina ya nguo za ndani – kama unapata UTI Zaid ya mara tano kwa mwaka, chunguza nguo za ndani na pata ushauri wa wataalamu ubadilishe kuepuka UTI Marakwa mara.
  • Usafi binafsi wakati wa kwenda haja ndogo na wakati wa haja kubwa
  • Usafi wa bafuni
  • Usichelewe kwenda kukojoa kwa kushukili mkojo muda mrefu
  • Wenye tezi dume kukojoa wakiwa wamekaa hupunguza maambukizi
  • Mipira ya mkojo – catheter kutumika kwa muda mfupi
  • Kutumia dawa kila wiki kwa wale ambayo uti imekuwa changamoto ya mara kwa mara, hasa wale wanaoshiriki tendo la ndoa mara kwa mara – mahusiano na ndoa.
Tiba
Zipo dawa mbalimbali za kuuwa bakteria zinazotibu UTI (sitaztaja hapa sababu wapo watakaochukuwa hatua kujinunulia bila kupima (over the counter medications haifai). Kama unazo dalili za UTI Nilizozitaja hapo juu tafadhari Fika kituo cha afya upate tiba sahihi.

Lakini kubwa ni kusisitiza unywaji wa maji ya kutosha, na kujikinga usipate maambukizi. Fuata kanuni za afya na kamwe usitumie dawa bila kupimwa na daktari kuthibitisha kwamba una maambukizi njia ya mkojo. Matumizi ya dawa bila kupimwa huleta usugu wa bakteria dhidi ya dawa – hivi sasa ni janga la dunia.

Elimu kwa umma – serikali na washika dau wadau wa sekta ya afya tuungane kwa pamoja kuelimisha jamii ya ugonjwa huu kwa mana kwa sasa ndio unaoongoza kwa watu kuhudhuria hospitali kupata tiba za ugonjwa huu na wengi hulalamika kujirudiarudia kwa maambukizi haya. Usafi na kuzingatia kanuni za afya ni nguzo ktika kukabiliana na taizo hili

Ni vema wenzi walio kwenye mahusiano au ndoa wakapima mkojo kwa pamoja, hasa inapotokea mwanamke ana UTI ni vizur mwanaume n yeye apimwe na kupatiwa matibabu kusaidia mwanamke asipate maambukizi kwa kujirudia.

Chukua hatua, mwambie na mwenzio

Asanteni.
 
Upvote 4

Asante sana mkuu
 
Back
Top Bottom