Ujue utapeli uliojificha wa kutafuta sarafu za kizamani kwa dau nono | kaa chonjo

Mkuu biashara hii ina ukweli na utapeli pia. Especially kwa pesa ya rupiah Kuna uhitaji wa pesa hiyo na uhitaji huo umezaa matapeli. Binafsi nimewahi kuona watu wamepata pesa nyingi baada ya kuuza rupiah lakini pia nimewahi kuona watu wametapelia pesa nyingi kupitia pesa hiyo ya rupiah.

Hivyo usiseme 100% kuwa biashara hiyo ni ya kitapeli. Niliijalibu pia biashara hiyo ndiyo nikabaini ya kuwa kuna ugumu mkubwa sana ndani yake kwani nilikutana na mtu sahihi mwenye uhitani wa rupiah ambae alikuwa ni mjerumani na alikuwa ni padri baada ya kunielezea masharti ya rupiah zinazohitajika ilinibidi niweke daluga chini.

Lakini hadj kufikia hapo ni kweli nilikuwa nimepoteza pesa nyingi. Hadithi yenyewe ilikuwa hivi÷

Nilikuwa na kundi langu tunaitafuta rupiah hiyo ya mtu mwenye helmet na juu yake Kuna ndege. Tukampata msukuma m1 akasema amewahi kumuona mama yake anayo. Tukamshauri amuombe mama yake hiyo pesa tukatajilike. Jamaa alitumia mda mrefu sana kumshauri mama yake nae mama huyo akasema mwambie mwenzio m1 ambae ni mtu mzima aje nimpe masharti ya pesa hii na ndiye ntakaemkabidhi wewe ni mtoto mdogo hutayaweza masharti yake. Mimi ndiye nilikuwa mtu mzima zaidi ya wote hivyo nikateuliwa mimi kwenda kuonana na mama huyo.

Nikaonana na mama falagha akaniuliza ya kuwa nina uhakika wa kwamba mtu niliyenae ni mtu sahihi na siyo wezi wa pesa za rupiah? Mimi nilimwambia kuwa ni mtu sahihi Kisha nikamuunganisha na mhusika akaongea nae wakahojiana maswali kadha wa kadha wote wakaridhia kuwa biashara itafanyika. Mama huyo aliniambia kwamba pesa hiyo ni msaada mkubwa sana kwake ameamua kuitoa ili kumsaidia kijana wake lakini wenzake anaoshirikiana nao katika matumizi ya pesa hiyo watamlaumu sana. Mama nilimuuliza manufaa ya pesa hiyo kwake akasema haina maana kuniambia bali nielewe tu kwamba pesa hiyo ni ya msaada kwao.

Tukapanga siku ya safari mama akasema katika safari hiyo ni lazima na yeue awepo kwamba sisi hatuna uwezo wa kuibeba na kuisafirisha pesa hiyo. Tukakubaliana na tukaanza safari. Katika kundi letu mimi ndiye nilikuwa na uwezo qa kipesa hivyo ilinibidi nifadhli safari hiyo tukiwa jumla ya watu 7. Tumefika kwa mhusika mkoa wa kagera ikiwa sisi tumetokea dodoma na mmiliki wa mzigo timempitia nzega tabora. Mwenyeji wetu alitupokea vizuri sana akatulipia hotel na chakula kwa usiku huo. Kesho yake tulienda ofisini kwake akaomba tuingie ndani watu wa2 hivyo niliingia mimi na bibi. Akaomba mzigo akakabidhiwa akafanya uchunguzi wake Kisha akasema hataichukua rupiah hiyo kwa sababu imeua. Ilikuwa ni msamiati mgumu sana kwangu. Bibi huyo akasema ya kwamba ni kweli rupiah hiyo imeua. Mtaalam akasema ataongea na mhusika ambae yupo nje ya nchi ambae yeye ana uwezo wa kushughulima na rupiah zilizoua kisha atatupatia jibu. Alikuwa ni mtu mwema akaturudisha hotelini akatulipia chakula na hotel kwa siku hiyo na akatukatia nauli tukarudi makwetu

Baada ya miezi m4 akanipigia cm kuwa tuipeleke hiyo rupiah mhusika amekuja. Pa1 na utapeli hii biashara kuzungukana ni kugusa tu. Hivyo mimi sikuona sababu ya kuwajulisha wenzangu. Nikapanda gari mpaka mzega nikaonana na dogo nikamwelezea Kisha tukaenda kwa bibi. Bibi alivyoniona alibadilika sura akaonyesha sura ya kunikasilikia. Kijana wake akamwelezea kuhusu ujio wangu nae bibi akasemwambia kijana wake atoke tuongee sisi wawili. Nae kijana akatoka. Bubi akaniambia kwamba tulivyoondoka na pesa hiyo wenzie walijua na wamempa adhabu kali sana. Hivyo hayuko tayari kuitoa pesa hiyo. Na akaniamuru nitoke hapo kwake.

Nilimwambia kijana wake nae akamrudia mama yake kumuomba mama akasema tayari amenipa majibu hivyo hana la kuongea nae. Niliondoka na nikampigia mtaalam na kumwelezea scenario hiyo. Kisha nikataka kujua ni kwa nini mama huyo alinipa majibu hayo. Nae mtaalam alinipa majibu ambayo yalinipelekea niachane kabisa na biashara hiyo

Hivyo ni kweli kwamba biashara hiyo ina ukweli, utapeli na dhuluma ya kutosha
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji478][emoji478][emoji478][emoji478][emoji478][emoji478][emoji477][emoji477][emoji477][emoji477]
 
A
Afu watu hao hawashauriki kabisa, mpaka apigwe ndio akili inakuja
 
Yes,I do.
 
Tunashukuru kwa kutupanga, yaani ukisikia stelingi kakutana na jambazi kuu sasa kabla hawajagusana hata muvi ikaisha!
 
Mtu unaambiwa shilingi 20 ya mwaka 1993 je kuna ukweli wowote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…