Ujumbe huu umeniliza bila kujua kuwa nalia nini!!

Snipperkilungu

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
253
Reaction score
424
Babu mmoja aling’ng’ania kwenda mjini kwenye harusi ya mjukuu wake, pamoja na hali yake ya kiafya kuwa mbaya lakini alitaka hivyo. Alihudhuria na siku ya harusi baada ya sherehe alimuomba mjukuu wake aongee naye kabla hawajaenda honeymoon.

Watu walitaka asubiri kwanza lakini aliwaambia hapana, mjukuu aliitwa na alianza kuongea naye. “Mjukuu wangu najua sina muda sana ila kuna kitu nataka kukuambia, leo umeoa sitaki ufanye kosa kama nililofanya mimi na alilofanya Baba yako. Baba yako nilimfundisha kua wanawake si watu wa kuaminiwa na unapaswa kuamini familia kwanza.

Nilikosea na ndiyo maana leo pamoja na kuwa Bibi yako bado yupo lakini nakufa mpweke. Ukweli nikua mjukuu wangu mkeo ndiyo anapaswa kuwa namba moja kwako kwa kila kitu kwani huyo ndiyo mtu pekee ambaye utazeeka naye na utakufa pembeni yake.

Mimi nilimpenda Mama yangu kuliko Bibi yako, lakini leo hayupo, nikawapenda Dada zangu lakini leo wanakufa na waume zao, nikawapenda Kaka zangu lakini leo wanakufa na wake zao. Mtu pekee ambaye nilimdharau na kumnyanyasa ni Bibi yako na ndiye ambaye tumetelekezwa naye Kijijini.

Angalia Baba yako, walikua wakipendana sana na Baba zako wadogo lakini leo wako wapi, kila mmoja anakufa na wake. Hivyo mjukuu wangu kama ukimpenda mkeo sasa basi wakati mkiwa wazee hutakua ukijuta hasa ukikumbuka kuwa ulimtesa zamani kama mimi ninavyojuta sasa.

Mjukuu wangu mtu hazeeki na Mama yake, mwanaume ambaye huzeeka akiwa anaishi kwa Mama yake huyo si mwanaume ni Dung’uthi, mwanaume ambaye huzeekea akiwa anaishi kwa Dada yake huyo ni Zezeta na mwanaume ambaye huzeeka akiwa anaishi kwa Kaka yake huyo ni Kapuku ila ambaye huzeeka na mkewe huyo ndiyo Mwanaume.”

Babu alimaliza kuongea na kuwaruhusu wajukuu zake kwenda kusherehekea harusi yao. Siku tatu baadaye babu alifariki akiwa pembeni ya mkewe “Bibi”, mwanamke ambaye alitumia ujana wake wote kumnyanyasa. Maneno ya Babu yalitimia, alikufa pemeni ya mwanamke aliyekua akimnyanyasa na kumuona kama takataka.
 
For compliment nitamwita mwanamke Mama.

Ila ukweli nihuu ,Hamna mwanamke chini ya jua atakayekuja kukata uzi wa Upendo wa Agape ulopo kati yangu na Mama yangu ..

hizi mambo zakufa namuachia Mungu .
 
The way nimehustle na Mama yangu leo uniambie nitapata ule upendo kwa mwanamke mwingine?..BIG NO!!.. I will love her in her own fashion and way!.
Sijui kama unaamini katika dini.

Biblia inasema 'Mwanamke atamuacha baba na mama yake ataungana na mume wake na mwanaume atamuacha baba na mama yake ataungana na mke wake nao hawa watakua mwili mmoja'
Kosa ni unapoamua kumvuta mama ako ukaungane naye kwenye ndoa yako, utajuta.

Hiyo ni biblia. Mtaani tunasema wewe ni mama's boy.

Njaa inauma sana usinichukulie serious.
 
Sikiliza hekima utaishi., fadhila huja bila kuumba acha Mama yako apambane na baba yako.
 
Hahahahh!!... na kuna msemo wanasema "don't trust a woman, apart from your mama" usiusahau na huu!. Anyway what i mean is mama yangu ana nafasi kubwa sana kunitengeneza leo hii zaidi ya mwanamke yeyote nilowahi kuwa nae, na wao wana waona wazazi wao ni bora sema inawezekana yupo nawe sababu ya natural law au biblical quote kama ulionipa while ukipata ile shida soo intense atarudi kwao tu or them family member watamshawishi arudi!.
 
Nasikitika maisha haya sijui nampenda nani daah. Baba? Mama? Dada? Kaka? Sina jibu kabisa maana sina feeling na mtu yeyote hadi huwa najishtukia.

Tatizo malezi niliyopitia, ndio madhara ya kukulia ghetto na wazazi kutoishi pamoja.
 
Mimi kwakweli huwa najipenda mwenyew kwanza maradufu..kisha nafasi finyu itakayobaki ndio nawapatia na hao wengine....mwambie huyo babu apambane tu na hali Yke aisee""

alamsiki mtoa mada
 
Nasikitika maisha haya sijui nampenda nani daah. Baba? Mama? Dada? Kaka? Sina jibu kabisa maana sina feeling na mtu yeyote hadi huwa najishtukia.

Tatizo malezi niliyopitia, ndio madhara ya kukulia ghetto na wazazi kutoishi pamoja.
pole sana" mimi nawapnda wote ...ila mapenzi yangu yamezdi kidogo kwa Dada zangu"" but hawajafikia hata nusu ya upendo nilionao dhidi yangu mimi mwenyew
 
Msingi wa upendo unatakiwa uwe kuaminiana, mnaaminiana halafu mapenzi ndiyo yafuate.

Mama ameujenga huo msingi over years kuanzia kukutunza tumboni mpaka kukulisha na asikulishe sumu, ukimpa chansi mtu baki ya kuuweka huo msingi am sure hatokudisappoint.

Kama mlikua na msingi imara, shida intense siyo kitu. Kuna id ilileta malalamiko humu kua mumewe ameteguka kiuno lakini amekua mkali etc etc etc, lakini hakuondoka last time alipost kuonyesha kua bado wapo wote.
 
Mimi kwakweli huwa najipenda mwenyew kwanza maradufu..kisha nafasi finyu itakayobaki ndio nawapatia na hao wengine....mwambie huyo babu apambane tu na hali Yke aisee""

alamsiki mtoa mada
Unaonekana ukiumwa hua unalegea sana.
 
Kila mtu ana nafasi yake. Mambo ya ndoa ni ya wanandoa wenyewe. Wazazi, ndugu na jamaa wasipewe fursa ya kukuongozea ndoa yako. Itavunjika au itakuwa si ya furaha kwenu wanandoa.
 
Aint no woman to alive that can take my mamas place....2pac Shakur
 
HUWEZI KUSEMA HUYU NITAMPENDA ZAIDI KULIKO YULE, KILA MTU (MAMA, BABA, MKE AU MUME ) WOTE KILA MMOJA WAO ANA NAFASI YAKE YA UPENDO KWAKO, AMBAO HAUWEZI KULINGANISHWA. KWASABABU KILA MTU ANA NAFASI, UMUHIMU, USHAWISHI NA MCHANGO FULANI KWAKO WEWE. HAKUNA ALIYE BORA KULIKO MWINGINE NI SUALA LA MCHANGO WA KILA MMOJA KATIKA MAISHA YAKO. LABDA KAMA ULIPATA UZOEFU MBAYA KUTOKA KWA MMOJA WAO LAKINI HUWEZI KUWAPENDA KWA KUWALINGANISHA KWANI MICHANGO NA NAFASI ZAO NI TOFAUTI.

KUMPENDA MKEO KWA KIWANGO CHOCHOTE HAIMAANISHI KWAMBA HUMPENDI MAMA YAKO AU KUMPENDA MAMA YAKO HAINA MAANA KWAMBA HUNA MAPENZI NA MKEO.

MPENDE KILA MMOJA KWA NAFASI YAKE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…