Ujumbe huu umeniliza bila kujua kuwa nalia nini!!

mtoa mada hii bangi uliovuta ni kiporo cha bangi nn? yaani mama yako akubebe miezi 9 tumboni aje akulele mwaka mzima tena aanzishe malezi ya miaka zaidi ya 18 alafu leo hii uje useme nimpende mwanamke ambae hata bikra sikutoa mm
 
Ngoja niywe chai ntakuja kusoma
 
Nasikitika maisha haya sijui nampenda nani daah. Baba? Mama? Dada? Kaka? Sina jibu kabisa maana sina feeling na mtu yeyote hadi huwa najishtukia.

Tatizo malezi niliyopitia, ndio madhara ya kukulia ghetto na wazazi kutoishi pamoja.
Pole sana jomba!!!
 
Mwenyezi Mungu kaumba moyo na kuujaza mapenzi ya aina tofauti kwa watu na vitu tofauti. Kuna mapenzi ya kupenda wazazi, kuna mapenzi ya kupenda ndugu, kuna mapenzi ya kupenda marafiki na hata kuna mapenzi ya kupenda vitu kama vile pesa, majumba, magari n.k, lakini yote hayo ni tofauti na mapenzi ya mke/mume au mchumba.

Mke huwezi kumgawa tofauti na pesa au mali pamoja na mapenzi yako kwa vitu hivyo, mama au baba mtampenda wengi yaani wewe na ndugu zako na pia utakua na uhakika kua na nyie wote kama watoto mnapendwa sana na wazazi awe baba au mama lakini kwa mke au mpenzi hutaki ampende mwingine mapenzi anayokupenda wewe.

Kwahiyo katika mioyo yetu kuna nafasi kwa mapenzi kuwapenda watu wengine tena mapenzi makubwa kwa kila mtu kutokana na nafasi yake, ni akili zako tu
 
Mama yangu ndiye tafsiri halisi ya upendo. Hata akifa, bado ataendelea kuishi ndani ya nafsi yangu. Nampenda sana mama yangu
 
Mama yangu ndiye tafsiri halisi ya upendo. Hata akifa, bado ataendelea kuishi ndani ya nafsi yangu. Nampenda sana mama yangu
Unampenda sana mama yako lakini tafadhali mkuu jiepushe na hiyo statement 'hata akifa ataendelea kuishi ndani ya nafsi yangu'....maana anaejua nani atatangulia mbele za haki kati yako na yeye ni Mola Mwenyewe
 
Elewa maana ya neno "hata"
 
Ni kweli kabisa ujumbe mzuri sana Mama ana nafasi yake sana lakini mke pia ana nafasi mtu unayelala naye kitanda kimoja mtu ambaye ukiumwa yeye ndio anajua ahangaike na wewe
 
Ni kweli kabisa ujumbe mzuri sana Mama ana nafasi yake sana lakini mke pia ana nafasi mtu unayelala naye kitanda kimoja mtu ambaye ukiumwa yeye ndio anajua ahangaike na wewe
Mapenzi ya mke ni unique kwakweli, Mungu Kaumba kamaliza pale
 
Mapenzi ya mke ni unique kwakweli, Mungu Kaumba kamaliza pale
Kweli kabisa mkuu ndio mana msiba wa mke au mume na wazazi wa mume na mke unauma sana mmezoeana sana sana kulala na mtu kesho hayupo lazima uchanganyikiwe mpaka uje kusahau sio leo
 
Kweli kabisa mkuu ndio mana msiba wa mke au mume na wazazi wa mume na mke unauma sana mmezoeana sana sana kulala na mtu kesho hayupo lazima uchanganyikiwe mpaka uje kusahau sio leo
Mara nyingi nashuhudia wanaume wanalia kama watoto wadogo wanapoondokewa na wake zao kitu ambacho ni nadra kuona wakati wamefiwa na mzazi, yaani kwa kifo ch amzazi anaweza akajikaza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…