Ujumbe huu unamhusu Rais Samia juu ya waliovunjiwa vibanda vya biashara

Ujumbe huu unamhusu Rais Samia juu ya waliovunjiwa vibanda vya biashara

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Salama wandugu,

Wikiend hii nikiwa nimeamka mapema nikiwa nacheki TBC kufuatiria ziara ya Rais wa nchi Mara kidogo nasikia hodi wife akatoka kidogo akaingia na mwanamke akiwa analia kisa mama huyo alikuwa akiuza mihogo huko kariakoo eneo ambalo hawakujua Kama wanatakiwa kaondoka

Mgambo wa jiji wamemkamata na ili asifungwe amelipa 170,000 la sivyo angeenda kufungwa na wenzake mama anadiriki kusema kuwa alifikia kutaka kunywa sumu na watoto wake sababu yeye ana watoto mume kamuacha na watoto ataIshi vipi na watoto fedha alizolipa ndio mtaji wake nakamuuliza rais wako siyo huyu anaonyeshwa kwenye TV hapa akasema baba ndio huyuhuyu huku akitokwa na machozi hapa anahitaji msaada wa mtaji.

Swali: Kwanini wakikamatwa wanatozwa pesa zinaenda wapi wametumwa na nani?
 
Hili lipo maeneo karibu yote tanzania, mwanza unakamatwa unapelekwa na inatakiwa ulipe 500,00 ili wakuachie
 
Hii nchi inahitaji Rais mfuatiliaji km JPM, Rais anayeshauriwa na kupangiwa kila kitu na wasaidizi wake bila kuhoji na kutafakari yeye mwenyewe lazima nchi imshinde.
 
Hi nikweli kabisa, juzi kuna sehemu nimesikia pia Kuna watu walikamatwa huko tegeta, kila mmoja ametoa laki moja
 
Two Wrongs don't make it Right

1) Huyo mama hakupaswa kuweka Biashara sehemu isiyoruhusiwa

2) Mgambo hawakupaswa kuchukua Rushwa au yeye kutoa Rushwa. Ila Je hata angepelekwa huko inapobidi apelekwe kutokana na hili kosa ingemsaidia ? Au yeye kapita na kuona alternative ni afadhali?

3) Serikali / Mamlaka pia ina makosa kutokuwa na shughuli alternative za watu kujipatia kipato hadi kupelekea watu kuhangaika kutafuta mkate wa kila siku kwenye mazingira hatarishi (Bila kuwapa watu alternative bora zaidi hizi vurugu hazitaisha)
 
Ni kosa kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi kibiashara.

Kama ilivyo mtu akiiba mali za umma akibainika anashitakiwa kwakuwa amevunja sheria, hata huyo mama amevunja sheria.

Ukibaka unashitakiwa kwakuwa ni kosa

Ukitukana unashitakiwa kwakuwa ni kosa

Ukisambaza picha za uchi unashitakiwa kwakuwa ni kosa.

Basi wafute kipengele kinachowazuia watu kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi. Hilo ndilo jambo la maana.

Sheria inatungwa ikifuatwa mnalalamika
 
Huyu mama anawavuruga sana Watanzania hapa nakunywa dodoma wine badala ya chai namuangalia tu yupo bandarini hata simuelewi anasema awamu iliyopita ndio ilikuwa na mafisadi so tuache kuchukua lawama awamu iliyopita na kutupia awamu ya sita
 
Hii nchi inahitaji Rais mfuatiliaji km JPM, Rais anayeshauriwa na kupangiwa kila kitu na wasaidizi wake bila kuhoji na kutafakari yeye mwenyewe lazima nchi imshinde.
Unaelewa maana ya uongozi? Kwani huyo mama kaonewa? Aliambiwa hapa haparusiwi kajipeleka. Kumbuka kutokujua sheria sio kisingizio.

Magufuli alivunja nyumba za watu kimara bila huruma. Akaunda task force kuua wapinzania n. K unapata wapi ujasiri wa kumtetea muuaji?
 
Wangemuacha akanywa sumu ili akifa ajifunze kua mamlaka zimekataza kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi.
 
Back
Top Bottom