Mujib Abdullah
Member
- Sep 18, 2019
- 6
- 2
Enyi watoto wa Kambarage ndimi ni mgeni wenu kutoka katika mamlaka ya ufahamu na utimamu wa kifikra, kwa hekima na uluwa nimetumwa kwenu niwaeleze kuwa kama mnataka mabadiliko ya kweli ndani ya miaka 25 ijayo basi mzingatie sana kuitibu changamoto ya afya ya akili ili muwe na kizazi chenye fikara timamu zitakazojenga maendeleo ya nchi katika kila nyanja.
Kwa undani wake afya ya akili hujumuisha ustawi wetu wa kihisia, kisaikolojia, na kijamii. Kwa kiasi kikubwa ndiyo inayoathiri jinsi tunavyofikiria, kuhisi, na kutenda, ndio msingi mkuu wa namna gani tunavyokabiliana na msongo wa mawazo, kuhusiana na wengine na kufanya maamuzi pia.
Kielelezo 1. Picha kwa hisani ya google
Utimamu wa afya ya akili ni suala mtambuka lenye kuhusisha kila nyanja kwasababu pasi na akili timamu hakuna sekta inayoweza kufanya maamuzi sahihi, kwa bahati mbaya suala hili halipewi uzito stahiki sio nchini kwetu tu bali duniani kwa ujumla, inasadikika kuwa watu hutumia chini ya asilimia moja (1%) ya bajeti zao za mwaka mzima kwa ajili ya kukabiliana na changamoto yoyote ya afya zao za akili.
Upande mwingine takwimu zinasema kuwa zaidi ya asilimia themanini na tano (85%) za watu wanagundulika kuwa wana matatizo ya afya ya akili huwa hawapati matibabu sahihi hali inayopelekea usugu na kuongeza idadi ya waathirika katika jamii.
Nadiriki kusema kuwa katika nchi hii kuna mamilioni ya watu waishio na matatizo ya afya ya akili pasi na kujijua kwasababu hatujajijengea utaratibu wa kuchunguza afya zetu za akili kitalaamu aidha kwa kukosa elimu au kwa kupuuzia.
Mengi yaripotiwayo na vyombo vya habari kutoka katika vungu mbalimbali za nchi yetu husabishwa na kukosekana kwa utimamu wa afya ya akili.
View: https://youtu.be/-wbzCsYk948?si=BxjiV5jaB2PbZY3r
Kielelezo 2. kwa hisani ya YouTube
Matukio kama ya Baba kumlawiti mtoto wake wa kumzaa, Mama kumchoma moto mwanae kwasababu amedokoa mboga jikoni, Marafiki wameuana kwasababu ya wivu wa kimapenzi na mwingine amejinyonga baada ya kusalitiwa na mpenziwe, matukio ya kuwauwa Albino, wazee na watu wenye macho mekundu ni kiashiria tosha cha namna gani tatizo la afya ya akili lilivyokuwa kidutu kwenye jamii yetu.
Mbolea ya hayo yote ni malezi na mifumo ya maisha yetu ya kila siku, tumezaliwa kwenye jamii ambazo mtoto wa mfugaji analazimishwa kumchukia mkulima, aliyefeli darasani atasimangwa na kukatishwa tamaa kama vile amefikia ukomo wa kuishi, na bado tunaaminishwa kuwa waliofanikiwa wengi wamepata walivyonavyo kwa nguvu za giza na sio jitihada za mikono yao.
Hata yule mtoto anaelelewa na mama peke yake atalishwa sumu ili amchukie baba yake bila ya kujali huduma na upendo wa baba huyo kwa mwanae, hapo ndipo uzaliwa Sonona na visasi visivyoisha vinavyoharibu utendaji wa moyo wa mtu na utimamu wake wa kufikiri.
Hata katika ngazi za juu za kimamlaka nao wanawajibika katika hili, kwasababu kwenye nchi hii wale wasemao ukweli ndio hupingwa, uhasama baina ya vyama vya siasa hufanya chuki itafune mioyo yetu na kufikia hatua ya kuuana, aukosoae uongozi kwa nia njema hutambulika kama adui wa maendeleo, haya ndio yaliyozalisha kizazi chenye uoga wa kukemea maovu na chenye hofu ya kutosikilizwa hali iliyopelekea vijana wengi kufa vifo vya kifikra kabla hata ya kile cha kuingia kaburini.
Hoja anayoimudu mtoto wa darasa la nne huibuliwa bungeni na hujadiliwa kwa nusu saa, vizazi vyetu vinayaona haya, vizazi vyetu vinashuhudia kuwa kuna ajira mpya imezalishwa inaitwa “uchawa”, bado nawaza kama miaka kumi ijayo tunaweza kuwa na kizazi chenye uwezo wa kujenga hoja zenye mantiki na kujiamini kama tutaishi kulingana na mifumo hii ambayo huwezi kupata teuzi bila kumsifia kiongozi.
Ili tuweze kufika 2050 tukiwa jadidi na mithaki kimaendeleo katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii na kisiasa serikali inapaswa kuunda sera madhubuti itakayoambatana na kampeni mahsusi kwa ajili ya kukabiliana na janga hili la matatizo ya afya ya akili.
Kielelezo 3. Picha kwa hisani ya google.
Jopo la watalaamu wa masuala ya tiba ya afya ya akili liundwe, lifanye safari na kuweka kambi zitakazoambatana na semina za kitabibu kwenye kila kijiji nchini, matibabu na ushauri vifanywe bure ili kuruhusu watu wengi zaidi kufikiwa na huduma hii kwa ajili ya ustawi wa afya zao za akili.
Mitandao ya kijamii itumike ipasavyo katika hili, makala mbalimbali zitakazoielimisha jamii kuhusiana na tatizo hili zitengenezwe na kusambazwa mitandaoni, filamu zenye maudhui kuhusiana na tatizo husika pamoja na hadithi ziundwe na kusambazwa pasi na malipo kwa jamii,
View: https://youtu.be/OyQ8KaTbjnw?si=ujU0YGfsyYR1n0Xd
Kielelezo 4. Mfano wa filamu ihusuyo afya ya akili. Kwa hisani ya YouTube.
Pia watu waliofanikiwa kujinasua kutoka katika janga hili kwa namna moja ama nyingine watumike kama kiigizo na kuhamasisha jamii juu ya utimamu wa afya ya akili.
Tukifanikiwa kutibu akili zetu tutatengeneza kizazi bora chenye uthubutu wa kufanya maamuzi, kizazi kisichokua na uoga wa kukosoa chenye kukubali mabadiliko na kuruhusu muingiliano wa itikadi pasi na mifarakano wala chuki lakini tukifeli katika hili tutarudi tena kwenye jukwaa hili miaka hamsini mbele kuulizana ni namna gani tutakabiliana na janga hili.
Wasalaam.

Upvote
2