Ujumbe kutoka kisiwa Juji "Tukishindwa kutofautisha maslahi ya Taifa, Tutakuwa waashi wa kugeuza mawe kuwa Malaika"

Ujumbe kutoka kisiwa Juji "Tukishindwa kutofautisha maslahi ya Taifa, Tutakuwa waashi wa kugeuza mawe kuwa Malaika"

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,291
Hii inaitwa Made in Kisiwa Juji.. Yaani mpaka leo mwaka 2019 nachelea kusema kwamba hatujafanikiwa kujuwa maslahi ya Taifa ni nini na najuwa kuna mahali tuliteleza.

Fuatilia haya maelezo yaliyonukuliwa mahali. Sauti kutoka kisiwa Juji.

" Kila aingiae madarakani anakuja na viroba vya vionjo na ghilba kuonesha kwamba yeye anaweza kuliko mwenzake. Utashangaa hata viongozi wanaotoka chama kile kile kilchoahidi maisha bora miaka mitano iliyopita na kikongwe kuliko vyote kinashindwa kuja na Falsafa inayoeleweka kuhusu kinachoitwa Maendeleo na Maslahi ya Taifa.

Leo Nchi inategemea mtazamo wa kiongozi wa juu na sio utaasisi. Hapo ndio tafsiri ya Uzalendo hugeuzwa kuwa mtazamo wa aliyeko madarakani na sio mitaala yetu ya mafunzo na ustaarabu wetu.

Unawezaje kuanzisha kikundi ndani ya system cha kuanza kunyanyasa watu wanaopinga mawazo yako na kumchukia kila anayetofautiana nawe kumpachika jina Beberu au sio mzalendo ili upate kuhalaLISHA KUMFANYIA MABAYA KAMA SIO UKENGEUFU. Zamani nilisikia watu hawa wakiitwa washamba sijui siku hizi.

Yaani makundi yote yanalazimishwa kuimba miluzi ya aliyeko juu utafikiri hawakuwepo hapa hapa mwaniona? Wazee wetu bila aibu na uzoefu wote walionao wanashindwa kujuwa nani anaharibu nchi hii ? Ina maana hakuna mahala pa kutazama kama tunakosea? Hakuna kioo chochote au kurunzi ya kumwirika yote yanayoendelea ili kujuwa kama haya yatendwayo sio Uzalendo lakini ni ghiliba?

Nadhani umefika wakati na sisi tubadilike kwa haraka ili tusije tukashindwa kutofautisha maslahi ya Taifa na kugeuka waashi tukaligeuza jiwe kuwa malaika
"

Huo ulikuwa ni ujumbe Kutoka KISIWA JUJI.


Nadhani kuna cha kujifunza hapo.


Kishada.
 
Kisiwa juji kisiwa juji nakutaja mara mbili,

Wahenga wamesema Ukimya wako ndio usalama wako.

Hata hivyo umenena vema na kwa hekima. Na hekima ni Maendeleo
 
Kisiwa juji kisiwa juji nakutaja mara mbili,

Wahenga wamesema Ukimya wako ndio usalama wako.

Hata hivyo umenena vema na kwa hekima. Na hekima ni Maendeleo
Daah. Hekima ni maendeleo
 
Tunaweza kukopa maneno hayo na kutufariji
 
Unamuua mtu kisa kahoji elimu yako. Unamminia risasi your fellow countryman utadhani mnyama unamuwinda kisa ametofautiana na wewe kimtazamo.

Irene Uwoya achukue fomu tututampisha
 
Back
Top Bottom