Ujumbe kwa Mh. Job Ndugai: Ujasiriamali una principles zake

Ujumbe kwa Mh. Job Ndugai: Ujasiriamali una principles zake

Manelezu

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
1,908
Reaction score
2,774
Mh. Speaker, ningependa kufikisha ujumbe huu kwa ufupi sana. Nimeamua kuandika baada ya kukusikia kwa mara ya pili ukiongelea ugumu wa ajira kwa vijana.

Sitaki kujikita sana kwa wajibu wa serikali duniani kote kutengeneza ajira na kuhakikisha sekta binafsi inakuwa kwa kasi ili kutoa fursa za ajira kwa vijana. Nchi hizo zipo, unazijua, kinachohitajika ni POWER OF THE BRAIN, kitu ambacho kwa kiasi kikubwa Waafrika hatuna. It's like we are programmed for failures, our political leaders.

Ngoja nijikite kwenye hoja yangu. Vijana kwa maelfu hawana ajira hilo liko wazi na wala sio debate tena, unashauri vijana wajiajiri, JAMBO ZURI SANA. Ila Mh. Ulishatumia tumia ubongo wako kufikiri vijana watajiajiri vipi? Naongelea mitaji. Wewe ni mtu mkubwa sana ndani ya serikali hii ulishajaribu kujiuliza and probably advice the government vijana watapata wapi mitaji ya kufanya huo ujasiriamali?

Ningekuona ni mwanasiasa makini kama ungeshauri vijana wajiajiri huku kuna Bank ya vijana inayotoa mikopo nafuu kwa riba esp kwa vijana wa vyuo vikuu. Your argument and comparison is poorly understood, unasema darasa la 7, unataka kijana wa chuo kikuu akaendeshe mkokoteni? Ili apate mtaji? Alisoma ili iweje? Mbona Waafrika tunakuwa a scum of the earth?

Hebu fanya hivi Mh. Sana, mtukufu. Ushauri toa kwa serikali vijana wapate mitaji then uendelee kutoa unsound political statements. Pia shauri Serikali hata kwa wale vijana waliobahatika kupata mitaji toka kwa ndugu wa kaamua kufanya ujasiriamali serikali yako iangalie suala la kodi. Leo naanza biashara kwa mtaji ambao hamkunipa wala hamjui nimetoa wapi siku ya kwanza hata sijapata faida natozwa mikodi.

Toeni basi incentives hata hiyo reli vijana waliomaliza chuo kikuu wanafanya biashara muwape unafuu wa kusafirisha mazao yao wanaolima muwaache wauze wanakotaka. Mahindi nilime mimi pembejeo haukunipa, na kuuza unipangie niuze wapi? Au unasahau serikali yako baada ya mavuno tu ndio mnaanza kupanga watu wauze wapi mazao?

Na mengi ila naomba kuishia hapa.
 
Ushauri muruaaa. Najua anapitapita humu atauona. Kwenye upande wa Kodi sio tatizo,tatizo kubwa ni mitaji kwa vijana. Serikali inatakiwa iwekeze kwa vijana kwa kuwapa mitaji. Nakubaliana na wazo la kuanzishe bank ya maendeleo ya vijana. Hizi asilimia kumi zinatolewa na halmashauri hazitoshi.
 
Hii sasa ndi inaitwa kutaalam decreasing in decreasing rate.
 
Ningekuona ni mwanasiasa makini kama ungeshauri vijana wajiajiri huku kuna Bank ya vijana inayotoa mikopo nafuu kwa riba esp kwa vijana wa vyuo vikuu..
Tanzania huhitaji mtaji ili kujiajiri. Hapo ulipo una laptop ama simu ambayo bei yake ni mtaji tosha.

Ardhi nchi hii ipo tele tena ni ya bure (nenda Tanga, Katavi, Tabora, n.k). Unataka mtaji wa nn? Bibi na babu yako walioko huko Nanyamba, Namanyele, Lyamba lya mbiti, n.k walipewa mtaji na nani?

Yaani wewe ulienda chuo kikuu kupoteza maarifa badala ya kuongeza maarifa?

Ama kweli vyuo vikuu Tanzania na Afrika ni sehemu za kupiga umbea, kufanya ngono na kujifunza utapeli tu.
 
Ushauri muruaaa. Najua anapitapita humu atauona. Kwenye upande wa Kodi sio tatizo,tatizo kubwa ni mitaji kwa vijana. Serikali inatakiwa iwekeze kwa vijana kwa kuwapa mitaji. Nakubaliana na wazo la kuanzishe bank ya maendeleo ya vijana. Hizi asilimia kumi zinatolewa na halmashauri hazitoshi.
Halmashauri ipi ilishatoa na kwa vijana gani, na vipi maendeleo ya biashara walizoanzisha.
 
Ushauri muruaaa. Najua anapitapita humu atauona. Kwenye upande wa Kodi sio tatizo,tatizo kubwa ni mitaji kwa vijana. Serikali inatakiwa iwekeze kwa vijana kwa kuwapa mitaji. Nakubaliana na wazo la kuanzishe bank ya maendeleo ya vijana. Hizi asilimia kumi zinatolewa na halmashauri hazitoshi.
Wanaongea tu sababu wana platforms just to score some political points ila hawana solutions zozote zile za kisiasa. Wanaongea as if wapo pale sio kutatua matatizo ya wananchi wao. Asia wamewezaje kutoa watu kwenye umasikini? Kama siasa hawaiwezi waache watu wenye akili waingie wabadili maisha ya watu.
 
Vijana wana nguvu kubwa sana, hawajaamua tu kubadilisha hali walionayo. Wamechagua kulalamika mitandaoni.
 
Wanaongea tu sababu wana platforms just to score some political points ila hawana solutions zozote zile za kisiasa...wanaongea as if wapo pale sio kutatua matatizo ya wananchi wao..Asia wamewezaje kutoa watu kwenye umasikini? Kama siasa hawaiwezi waache watu wenye akili waingie wabadili maisha ya watu.
Wanaiweza sabu inawapa kula ambayo ndio priority yao
 
Back
Top Bottom