Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Madam Spika, nimekusikiliza kwa makini ukitaja vifungu vya sheria & Kanuni ambazo unasema Luhaga Mpina (Mb) amevunja! Nakushauri rudi ukavisome vizuri maana baadhi ya vifungu UMEUPOTOSHA Umma. Umevitafsiri unavyotaka wewe ili lengo lako la kumwondoa Bungeni litimie, lakini sio tafsiri halisi ya kisheria.
Pia, kama Luhaga Mpina anasema alipewa adhabu pasipo KUSIKILIZWA, maana yake wewe kama Spika umeruhusu Katiba ya Nchi kuvunjwa; ibara ya 13(6)(a). Kwa hili, huna KINGA ya kutoshtakiwa na Mpina (mwathirika) anaweza kufungua kesi ya MADAI dhidi yako. Kama hii haitoshi, mtu anayevunja Katiba ya Nchi anatenda KOSA LA UGAIDI chini ya kifungu 4 cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi (2002).
Mwisho, wewe ni Mwanasheria na nikushauri tu unaposoma na kufafanua vifungu vya sheria, ufanye kwa WELEDI na kwa maslahi ya Umma na si yako binafsi au ya kikundi cha watu wachache! Tafadhali usichanganye SHERIA & SIASA. Hii sio mara ya kwanza, ulifanya hili pia wakati wa mkataba wa DP WORLD. Ulitoa pia tafsiri zako binafsi wakati wa kuhamisha Wamasai Ngorongoro!
Huku nje kuna wasomi wanaofuatilia. Usituharibie taaluma yetu tafadhali.
Pia soma Bunge lajadili juu ya adhabu ya Mbunge Luhaga Mpina. Laamua kumfungia vikao 15