Ujumbe kwa viongozi na mashabiki wa Simba SC

Wachezaji wazawa wakija Simba wanakuja kuua viwango vyao tu.

Mchezaji kijana mwenye kipaji kama Muhammadi Juma amepotea mazima.

Angeenda Yanga angekuwa wa moto sasa hivi.
Ona akina Bakari Mwamyeto, Faisal Salum. Muhammadi Baka, Mzinze wamepata muda wa kuonesha vipaji vyao na wameonekana.

Nashangaa Boko anacheza Muhammedi Mussa anaishia Benchi tu.
Mabeki wazuri kama Hussein Kazi na Israeli Mwenda wamebaki kuwa waokota mipira tu.
 
japo una hoja ila umepuyanga, kapombe sio mtanzania?? zimbwe ni mkongomani??? kibu?? mzamiru?? aishi?? wapambane waache kusubiria wapewe nafasi kwq ajili ya rotation
 
Tafadhali anayefahamu ku-download huu mlio anitumie niwe napokelea simu ni mlio mzuri sana kwa kupokelea simu.
 
Usilalamike bila kuwa na facts. Hao wachezaji wazawa wa Simba akina Kapama, Kyombo na huyo Mwenda wamewahi kupewa nafasi hata na makocha waliopita lakini performance zao ni DUNI saana.

Wakisajiliwa Simba wanajiona wamefika. Utaanzaje kumuweka bench Kapombe ili au Baleke au Phiri kwa ajili ya wachezaji wasiojituma?
 
Mechi Ijayo Ya Coastal Union Utashangaa Zimbwe Na Kapombe Wapo Badala Uwapumzishe Wajiandae Mechi Ingine Wape Chance Hawa Vijana Wengine Mwenda, Duchu
MNASEMAJE
Awapumzishe wakati ndio wanatakiwa wacheze ili wawe fit? Hii tabia imeanza kwa kasi, unakuta mtu anaweza kulogin basi anakimbilia kumkosoa mtaalamu aliyesomea kazi hiyo
 
Alokwambia kikos anapanga robertinho nani?. We huoni hata mbinu zake hazitokei?.

Kikosi Cha simba kinapagwa na uongozi flaniflan hivi. Kikishinda inaonekan kawaida na kikifungwa analaumiwa kocha
 
Si mambumbumbu ?
 
Kuhusu ubovu wa mashabiki jf Hilo nakuunga mkono [emoji817]. Humu siku hizi kuna vilaza kama kwenye siasa. Nachelea kusema wanasiasa wabovu ndo wamegeuka Wasemaji kuhusu soka Kwa ID tofauti.
 
Wachezaji Simba wanahitaji rotation, Manura ametumia kwenye mechi ambayo so lazima aanze, Peter Banda ameachwa wakati muda mwingi alikuwa anatumia bench. Mtoa mada yupo sahihi kocha ni Kama amekariri kikosi.
 
Kocha analaumiwa kwa matokeo mabaya na sio kwa kutompanga fulani. Simba sio timu ya taifa , unapolilia rotation iwe kwa wachezaji wote na sio eti wazawa. Kocha atafanya rotation atakapo ona yeye inafaa na sio kumpigia makelele wakati hutawajibika wewe endapo atapata matokeo mabaya akifanya hiyo rotation unayoitaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…