Ujumbe kwa wale wote mnaoagiza magari kutoka nje. Usipite bila kusoma hapa

Ndugu habari za jion, Kuna jambo nimeona tuambiane ukweli ili tuelimishane kidogo.

Kuna watu watu wanaagiza magari nje kupitia agents au mawakala mbalimbali mbaya zaid kuna agents wengine sio waaminifu kabisa.

Mtu anakwenda kwa agent amchagulie gari, amsaidie malipo yaani kila kitu anafanya agent wewe unasubir gari tu ifike upewe tena unakuta gari umeiangalia juujuu kisa unamwamni agent wako acha ufala asee.

Sasa mambo yanayofanyika ni hatari mpaka huruma yani hawa jamaa wanabadili vitu vingi sana watu wanapigwa hela nje nje kama unavojua watu wengi hatuna elim ya magari. Inauma sana kwakweli.

Hawa jamaa wanawabadilishia taa [emoji362], fan na time belts, battery nk hivi ndo nashuhudia live. Mimi nimefungua ofisi yangu mitaa ya huku sokoine karibu na port view sasa huku ndo gari zilizotoka bandarin ndo zinazagaa sana unakuta gari inakaa mpaka wiki 2 kwa wakala unajiuliza ina maana mwenye gari hana taarifa? Kama ni ishu za tbs jamaa anashindwa kufix tatizo mapema?.

Hapa ofisn mimi nafanya polishing, painting, nauza lubricants nk sasa wengi huwa wanakuja kupata huduma, juzi kuna jamaa kaja na crown athelete kupiga ribiti sasa jamaa akampigia simu mwenye gari, maongezi yao yalikua hivi nanukuu “ tajir mambo vipi gari yako imefika toka juzi sasa nimeshamalizana na TRA bado TBS kwasababu gari betri imekufa na belts zote zimeisha tumeambiwa tuchange ili gari ipewe certificate ndo tukafanye usajili na gari ikiendelea kukaa hapa bandarin inachajiwa mkuu”

Jamaa akapaniki “ndomana nimekupa kazi betri sh. Ngap jama akamwambia chukua la mtumba la crown kama yako jamaa anauza achana naya dukani bei 250k na belts 270k za mtumba crown original, jamaa akasema nakutumia chap, jamaa anaongea ukituma mapema leo leo gari inatoka mpaka plate No. [emoji28]. Jamaa hakuchukua hta dk5 akatuma hio pesa walichofanya jamaa wakaisafisha ile betri wakabandika plate No. hao wakasepa boya kashaliwa[emoji28][emoji28][emoji119][emoji119]. Ikabandikwa pale DXM kumbe gari ilikua imesajiliwa tyr.

Mwingine huyu alikua dada amepigwa kama
Laki6 kweli kupiga ribiti, kuosha engine na kufanya service laki6??[emoji28][emoji28][emoji119][emoji119]. Jamaa anakuagizia gari imepauka hatari ikifika bongo anakupigia polish inanga’a fresh hizi gari kila siku tunapiga polishi na kurudia rangi ,au kama kuna michubuko anarudia rangi wewe huwezi jua. Ni matukio mengi siwez sema yote.

Sasa gari ambazo zinafanyiwa ma service ya ajabu ni hzi BMW na marcedes nyingi utakuta mara power window imekufa, sijui nn nilimuuliza jamaa akasema wengi wanaagza hizi gari kwa mihemuko anachukua ya bei rahs ilimradi na yeye awe na bmw matokeo yake gari inafika na matatizo lukuki.

Ushauri wangu agiza gari mwenyewe mpe agent kazi ya kufanya clearing tu, fatilia meli ilobeba gari yako mwanzo mwisho ikifika tu lazma agent anajua fatilia hatua zote anazofanya kama gari inashida mara nyingi tbs mtasumbuana kwenye tairi kama unachochote wape usipoteze muda kama una pesa mwambie atoke na gari wewe ichukue gari yako usimwachie kabadili tair hapo gari ushaichek angle zote.

Kama unatumia agent hakikisha anakupa picha za gari zote na malipo fanya wewe usimpe yeye afanye malipo hapa wengi wanalizwa, agent atakuagizia gari ya kawaida ili apate faida zile high quality hawezi sababu bei ni kubwa itamkata. Ogopa sana huu utapeli kuagza toyota ist ni 13.5m awamu ya kwanza utalipia 7m afu utamalizia 6.5m ogopa sana huu utapeli[emoji28][emoji28].

Kuna agent wengine ni waaminifu ila tatizo la wale wanaokwenda kule kufanya clearing bossy hawez kwenda bandarin atatuma vijana watu hawaaminiki asee watu wanajiongeza sana. Watu wana njaa nyie kuna jamaa tulimwambia tunataka taa za subaru OG akasema nipeni siku3 kuna gari inatoka soon kweli akaleta taa
Unafikiri katoa wapi?

Sema nini watu wanashusha mandinga makali sana asee daah [emoji119][emoji119].
Polishing ya gari mpya unafanya sh ngp
 
Ofisi yako ipo upande wa Port View au hapo karibu na kibanda Cha traffic. Mchana nitamleta raia mmoja hapo
 
kuna ile issue nyengine watu wana shusha gari bandarini wanajifanya gari may be ya zambia au congo, malawi n.k kumbe ni ya bongo bhn gari inakamilisha taratibu za bandarini ina toka ikifika kule mpakani ina geuzwa chaka kwa chaka kumbe mwenye gari anakuwa kaamda number plate kanunua kwa hizi gari zinazo piga mizinga au zimesha jichokea jamaa ana nunua number plate na chases number wanaenda wana i fix huwezi jua mzee tayari mtu anakuwa ame kwepa usajilj hapo nilisikia hizi fununu hivi ni kweli kuna undava huo au ni stori tu za vijana waendesha IT?
 
Hizi Story Mzee
 
Hizo Story hakuna Mtu mwenye uwezo wa kununua gari ya thamani,Kisha akwepe Kodi Ili aje asajiliwe kwa usajili wa namba ya Zamani
 
Huo mchezo upo hivi kama mtu anataka Fuso,Land Cruiser na Pick up double cabin kutoka Zambia Kwa Bei nafuu(Kitonga). Unanunua gari Zambia au Malawi iliyotumika kule Ili kupunguza gharama za kulipa Kodi pale border.

Kisha unatafuta Kadi ya gari kama hiyo hiyo ambayo gari ilipata ajali,imekufa. Hiyo gari utayoleta kutoka Zambia au Malawi itatumia Kadi, chasis no ya gari iliyokuwa huku baadae utaenda Polisi kutoa taarifa kuwa ulibadili injini au rangi.
Hiyo gari inaingiaje TZ? Kwa usajili wa Zambia?
 
Hii sio official ni shortcut na Watu ndio kazi zao. Hizo gari za Zambia zinaweza kuja kama scrap inachinjwa kule huku inakuja kama spare, Kuna njia za panya ikiingia inakatwa na kuvuliwa vifaa kwenye gereji za karibu na Tunduma kumbuka gari za Zambia huwa zinafika kufanya Service maeneo ya Tunduma upande wa Tanzania
 
Ndugu habari za jion, Kuna jambo nimeona tuambiane ukweli ili tuelimishane kidogo.

Kuna watu watu wanaagiza magari nje kupitia agents au mawakala mbalimbali mbaya zaid kuna agents wengine sio waaminifu kabisa.

Mtu anakwenda kwa agent amchagulie gari, amsaidie malipo yaani kila kitu anafanya agent wewe unasubir gari tu ifike upewe tena unakuta gari umeiangalia juujuu kisa unamwamni agent wako acha ufala asee.

Sasa mambo yanayofanyika ni hatari mpaka huruma yani hawa jamaa wanabadili vitu vingi sana watu wanapigwa hela nje nje kama unavojua watu wengi hatuna elim ya magari. Inauma sana kwakweli.

Hawa jamaa wanawabadilishia taa [emoji362], fan na time belts, battery nk hivi ndo nashuhudia live. Mimi nimefungua ofisi yangu mitaa ya huku sokoine karibu na port view sasa huku ndo gari zilizotoka bandarin ndo zinazagaa sana unakuta gari inakaa mpaka wiki 2 kwa wakala unajiuliza ina maana mwenye gari hana taarifa? Kama ni ishu za tbs jamaa anashindwa kufix tatizo mapema?.

Hapa ofisn mimi nafanya polishing, painting, nauza lubricants nk sasa wengi huwa wanakuja kupata huduma, juzi kuna jamaa kaja na crown athelete kupiga ribiti sasa jamaa akampigia simu mwenye gari, maongezi yao yalikua hivi nanukuu “ tajir mambo vipi gari yako imefika toka juzi sasa nimeshamalizana na TRA bado TBS kwasababu gari betri imekufa na belts zote zimeisha tumeambiwa tuchange ili gari ipewe certificate ndo tukafanye usajili na gari ikiendelea kukaa hapa bandarin inachajiwa mkuu”

Jamaa akapaniki “ndomana nimekupa kazi betri sh. Ngap jama akamwambia chukua la mtumba la crown kama yako jamaa anauza achana naya dukani bei 250k na belts 270k za mtumba crown original, jamaa akasema nakutumia chap, jamaa anaongea ukituma mapema leo leo gari inatoka mpaka plate No. [emoji28]. Jamaa hakuchukua hta dk5 akatuma hio pesa walichofanya jamaa wakaisafisha ile betri wakabandika plate No. hao wakasepa boya kashaliwa[emoji28][emoji28][emoji119][emoji119]. Ikabandikwa pale DXM kumbe gari ilikua imesajiliwa tyr.

Mwingine huyu alikua dada amepigwa kama
Laki6 kweli kupiga ribiti, kuosha engine na kufanya service laki6??[emoji28][emoji28][emoji119][emoji119]. Jamaa anakuagizia gari imepauka hatari ikifika bongo anakupigia polish inanga’a fresh hizi gari kila siku tunapiga polishi na kurudia rangi ,au kama kuna michubuko anarudia rangi wewe huwezi jua. Ni matukio mengi siwez sema yote.

Sasa gari ambazo zinafanyiwa ma service ya ajabu ni hzi BMW na marcedes nyingi utakuta mara power window imekufa, sijui nn nilimuuliza jamaa akasema wengi wanaagza hizi gari kwa mihemuko anachukua ya bei rahs ilimradi na yeye awe na bmw matokeo yake gari inafika na matatizo lukuki.

Ushauri wangu agiza gari mwenyewe mpe agent kazi ya kufanya clearing tu, fatilia meli ilobeba gari yako mwanzo mwisho ikifika tu lazma agent anajua fatilia hatua zote anazofanya kama gari inashida mara nyingi tbs mtasumbuana kwenye tairi kama unachochote wape usipoteze muda kama una pesa mwambie atoke na gari wewe ichukue gari yako usimwachie kabadili tair hapo gari ushaichek angle zote.

Kama unatumia agent hakikisha anakupa picha za gari zote na malipo fanya wewe usimpe yeye afanye malipo hapa wengi wanalizwa, agent atakuagizia gari ya kawaida ili apate faida zile high quality hawezi sababu bei ni kubwa itamkata. Ogopa sana huu utapeli kuagza toyota ist ni 13.5m awamu ya kwanza utalipia 7m afu utamalizia 6.5m ogopa sana huu utapeli[emoji28][emoji28].

Kuna agent wengine ni waaminifu ila tatizo la wale wanaokwenda kule kufanya clearing bossy hawez kwenda bandarin atatuma vijana watu hawaaminiki asee watu wanajiongeza sana. Watu wana njaa nyie kuna jamaa tulimwambia tunataka taa za subaru OG akasema nipeni siku3 kuna gari inatoka soon kweli akaleta taa
Unafikiri katoa wapi?

Sema nini watu wanashusha mandinga makali sana asee daah [emoji119][emoji119].
Hawa ma agent ni wezi tu.

Unaagiza gari ila wanakuletea mkweche.
 
Hivi kuna Gharama gani Kuagiza Mwenyewe!?

Je nikiingia Be forward siwezi Agiza Mwenyewe na Kufanya Clearance kila Kitu.

Hao ma Agent huwa wana Nini Ambacho Huwezi kukufanya?
Kuagiza mwenyewe unaweza ni vile watu wanaingiaga uvivu tu plus uzembe. Ila ukijaribu kuagiza kwa hawa madalali wa instagram ni umeliwa wamejaa matapeli wa kutupwa.

Ila kwenye clearance huwa lazima uwatumoe agents.
 
Watanzania wengi wamezoea spoon feeding..... kwenda tu website ya befoward kuchagua gari kwa hitaji lake, anamwachia agent na wengine wanamkabidhi cash eti agent ashughulike kila kitu tunayo safar ndefu sana
What do expect, utaambulia aina ya gari, habari ya Ubora na vingine ni juu yako.
Tatizo ni ushamba ndugu yangu yani mtu anajua kuagiza gari Japan ni rocket science kumbe ni kitu rahisi tu kipo straight
 
Usisahau pia odometer tampered unakuta gari imetembea klm laki mbili mtu anapigwa anashushiwa imetembea Km elfu 30 anaingia kichwa kichwa anauziwa bei mbaya, Dah ukiangalia ndani gari ya klm elfu 30 imechakaa kila kona. Hao ma agent ndio michezo yao wao wanakununulia gari lililotembea klm nyingi kwa bei ndogo halafu wao wanazishusha
 
Back
Top Bottom