Mudawote
JF-Expert Member
- Jul 10, 2013
- 11,612
- 16,189
GTs
Walioko karibu na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tafadhali mfikishieni ujumbe huu kwa unyenyekevu na mapenzi mema: Hotuba yake ya leo kuhusu Mpina pamoja na zingine zenye mwelekeo wa malalamiko zinamharibu zaidi kuliko zinavyomjenga. Mwambieni kuwa yeye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – siyo mlalamikaji.
Hotuba yake ya jana pale Simiyu ilikuwa bora sana – yenye matumaini, busara, na iliwagusa wananchi kwa kina. Watanzania wanahitaji kusikia lugha ya matumaini, siyo kauli za kuonesha nani hafai au nani anafaa. Tunahitaji Rais anayetupa dira na sio kuhukumu kila tone la upinzani au maoni tofauti.
Mwambieni kuwa yeye ni mti wenye matunda – na hakuna mtu anayetarajia kuchuma chungwa chungu kutoka kwenye mti wa matunda. Hata ikitokea chungwa moja chungu, mti hauwezi kusema nani achume au asichume – maana mti wenye tunda halali huwa haubagui.
Kwa kifupi, Dkt. Samia atambue kuwa Watanzania tunampenda sana. Akiamua kutumia lugha fasaha yenye faraja na matumaini, kila Mtanzania hujisikia fahari, hujawa na matumaini mapya, na wengine hata hulia machozi ya furaha kwa kuwa na Rais mwenye hekima na utu.
Tumsihi Rais aendelee kuwa kiongozi wa matumaini, siyo wa malalamiko. Aendelee kuhubiri mshikamano, maono, na mwelekeo wa taifa – kama alivyofanya Simiyu. Sauti yake inapotia moyo, taifa zima huinuka.