Ujumbe kwa Waziri wa Madini, Anthony Mavunde

Ujumbe kwa Waziri wa Madini, Anthony Mavunde

TrueVoter

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2008
Posts
3,034
Reaction score
3,032
Salaam Ndugu Waziri,

Mwishoni mwaka jana Tume ya Madini ofisi ya Madini Mbogwe Geita ilitangaza kukaribisha maombi ya leseni kwa wachimbaji wadogo kwenye eneo lililokuwa hifadhi ya Kigosi, lakini baada ya ugawaji wa mwanzo kufanyika, walitangaza tena maombi kwa block B eneo hilo hilo. Kutokana na matokeo ya ugawaji vitalu Block A, kwa niaba ya waombaji wengine na wachimbaji wadogo na wananchi wanaoitakia nchi yetu mema, nimeona vyema kukujulisha mambo machache uyafanyie kazi.

1. Pamoja na kuwa kila mtu ambae ni raia wa Tanzania ana haki ya kuomba, kwa nini majina ya watu maarufu wengi walipewa vitalu zaidi ya 3 na si kitalu kimoja kama wengine? majina kama Magufuli, Kikwete, Rosemary senyamule, Anna Makakala nk..

2. Kwa kutizama majina kuna baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya waliomba na kupewa vitalu, akiwemo Mkuu wa wilaya ya Mbogwe Grace Kingalame, je, hakuna mgongano wa masilahi wao kuomba vitalu kushindana na watu wengine ambao kupitia uchimbaji madini, kpato wanachopata kinakatwa kodi ambayo wao viongozi wanalipwa mishahara, hata kama ni haki yao kuomba lakini kimaadili si sawa! wao ni wasimamizi, sasa huo usimamizi unaufanya kwa namna ipi kama yeye tena anakuwa mchimbaji mdogo? hiyoni tamaa na ubinafsi, ambao kiongozi hapaswi kuwa nao!

3. Itafaa sana kama maombi ni mengi bora kugawa kitalu kimoja kwa kila aliyeomba, watakaopata wapate watakaokosa wakose lakini si sawa kugawa wengine vitalu 6 wengine 1 na wengine kukosa kabisa, kigezo gani kinatumika kumpa mmoja vitalu 6 mwingine kitalu 1, na kwa nini watu mashuhuri na viongozi tu ndio wanapewa vitalu zaidi ya kimoja?

4. Kwenye orodha ya majina block A kuna majina hayana TIN wala NIDA na kuna taarifa watu wa usalama wamepatiwa vitalu, je, ni sawa kufanya hivyo?

Mwisho, Mh. waziri ishauri serikali kwamba rasilimali ya madini hairudishiki, baada ya uzoefu wa kuchimba almasi, dhahabu na madini mengine kwa muda sasa ktk maeneo tofauti ya nchi, ni vyema sasa uchimbaji madini ufanyike pale tu thamani ya shilingi yetu inapoanza kupungua, madini yatumike kurudisha na kustabilize thamani ya shilingi,hilo ndio liwe lengo. Hakuna maana yeyote kuchimba madini yakaisha pasina na badiliko kwenye hali na ustawi wa watu, umaskini uko pale pale.

Eneo hili la Kigosi ni hifadhi, kumekuwa na ulazima gani kugawa vitalu watu wachimbe dhahabu sasa..mbona Mwalimu na viongozi wengine waliacha eneo hili liendelee kuwa hifadhi? isije kuwa ni tamaa ya baadhi ya viongozi kutaka kuchukua eneo hili kwa maslahi yao na kutumia kutangaza kugawia wengine kama kivuli tu, wakati eneo kubwa wanamiliki wao..kama ni hivyo, si sawa.

Hakuna mahali popote mali iliyopatikana kwa kudhulumu watu imekuwa baraka kwa mtu, familia au taifa! Tuache maeneo ya Hifadhi yaendelee kuwa hifadhi! Asante.
 
Back
Top Bottom