Mada inahusika.
Wakati akitaja majina ya wateule wa nafasi ya kugombea uwakilishi kwa Zanzibar, Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM ndugu Polepole alisikika akitumia neno Mzee yule akimlenga Maalim Seif eti kuacha kuwataja viongozi wao na kufika hatua ya kusema ni onyo la mwisho na vyenginevyo atamshukhulikia kwa kumsema katika hali ya tofauti na kuibua mengine. Tunasubiri Ndugu Pole Pole aseme hayo mapya kuhusu Maalim Seif ambayo hayajasemwa.
Lakini analopaswa kutambua mwenezi huyu amjue vizuri Maalim Seif yanapoibuka mambo kuhusu maslahi ya Zanzibar.
Hii ni sauti na nembo ya Maslahi ya Zanzibar. Zanzibar kuna siasa zake na maalim Seif hazungumzii mambo madogo madogo.
Kule Zanzibar CCM ina wakati mgumu hili ndugu Pole Pole halisemi. Kule watu wanapigania SIASA na NCHI.
Kwenye Maslahi ya nchi ya Zanzibar Maalim Seif alishajipambanua zamani na hata wazalendo wachache waliomo CCM huyu ndio sauti yao hilo alitambue Mwenezi.
Alichokisema Maalim Seif ujumbe umefika tayari. Wazanzibari tokea enzi kwenye Muungano nafasi ya Naibu Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Zanzibar huwa ni mzanzibari bila kujali uhafidhina wake na ukada wake. Kitendo cha kubadilishwa na kuletwa mtu kutoka Bara linawakera hadi CCM na limekoleza kidonda cha kuletewa mgombea wa urais kutoka Bara asiyekubalika.
Mteuzi ni Rais Magufuli na ni lazima atajwe. Kwa nini asitajwe?
Kupelekwa wasimamizi wa uchaguzi wa NEC kutoka Bara wakiwa usalama wa Taifa huko Pemba na kuweka mapingamizi ya kihuni wanatekeleza maagizo ya CCM ambaye Rais Magufuli ndiye mwenyekiti wake.
KINACHOENDELEA ZANZIBAR
Kwanza ni ukweli kwamba ndani ya CCM Zanzibar kuna mgawanyiko wa wazi, kuna watu walipata nafasi ya kwanza kwenye ubunge na uwakilishi hawakuchaguliwa kwa sababu ya kutoaminiwa na wanadhaniwa wanatumika na upinzani. Ukweli ni kwamba wazalendo wa CCM Zanzibar wameshtukia mchezo wa kutaka kupotezwa Zanzibar na hawa watu wana jambo lao kwenye uchaguzi wa 2020. Kuna kila dalili ya kuwepo hatua za kimkakati za kuchaguliwa wabunge ambao ni mapandikizi kwa ajili ya kuunga mkono kila kinacholetwa.
Teuzi za wawakilishi na wabunge zimeegemea makambi, udugu na kupendeleana. CCM bara haiwaamini baadhi ya viongozi wenzao Zanzibar ndani ya CCM na serikalini huko Zanzibar. Hili linaleta ubushi wa kimaslahi. Zipo taarifa kwamba watu wanaodhaniwa kuunga Mkono upinzani (maslahi ya Zanzibar) wanawindwa na kulengwa.
Mgombea wa urais CCM Zanzibar hakubaliki na jitihada zinafanywa za kushawishi. Wazanzibari kwa umoja wao bila kujali itikadi za kisiasa wanamuona Rais Magufuli na utawala wake katika jicho la tatu. Hatma ya Zanzibar iko mashakani ukizingatia kauli za kutaka 2/3 ya wabunge kwa lazima na makovu ya Urais wa Zanzibar.
Zanzibar kuna CCM bara na Zanzibar. Kila kundi linaweka maslahi yake.
Ndugu Pole Pole Naomba umtambue Maalim seif vizuri huyu si mchovyo ni halisi.
Asubuhi Njema
Kishada.