Ndugu zangu watawala, hali ilivyo sasa katika Nchi yetu si nzuri sana kimahusiano.
Umoja,upendo na amani vinaweza kupotea kutokana na uzembe mdogo mdogo wa watu wachache.
Juzi katika harakati za kuzima maandamano ya CHADEMA askari polisi wametumia nguvu kubwa mno kana kwamba Nchi yetu imevamiwa na Nchi nyingine.
Hali kama ile ikiendelea inaweza kujenga chuki kubwa sana kati ya Raia na Polisi na Viongozi wanaoamuru hayo yafanyike.
Kukishakuwa na uadui kati ya Raia na Polisi, Amani itapotea kabisa kwa sababu kutakuwa na kuwindana kati ya Raia Polisi. Hali ikishafika hapo, mpaka kuja kutengemaa inaweza kuchukua muda mrefu sana.
Rai yangu ni kwamba:-
1. Viongozi wa serikali waache kuwatumikisha Polisi kwa maslahi yao binafsi.
2. Polisi wajitahidi kutumia zaidi AKILI kuliko kutumia MABAVU dhidi ya Raia.