Chifu mkuu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2025
- 422
- 489
Huu ni Uzi maalumu kwa waislamu katika siku za ijumaa kupeana taarifa umeswali ijumaa msikiti gani, khatibu wa ijumaa alikuwa sheikh au Ustaadh gani na mada ya khutba ya ijumaa ilizungumzia nini.
Kwa kuanzia , Leo mimi nimeswali swala ya ijumaa katika msikiti wa Abuu Dharri Jundub bin Junada unaopatikana kwenye makutano ya Kawawa road na Mafuta street manispaa ya Moshi.
Khutba ya ijumaa imetolewa na sheikh Doctor Khamis Imamu toka Kariakoo Dar es salaam.
Ujumbe : Khutba ya ijumaa imetutaka waislamu kujiandaa kwa uchamungu tunapouelekea mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Pia sheikh kawakumbusha waislamu wanaodaiwa madeni ya swaumu ya mwezi wa Ramadhani iliyopita kulipa swaumu hizo kabla Ramadhani nyingine haijaingia.
Je wewe mwenzangu swala ya ijumaa umeiswalia wapi, msikiti gani, sheikh au Ustaadh gani katoa khutba , na khutba ya ijumaa ilikuwa na ujumbe gani?