Ujumbe wa Henry Kileo mume wa Joyce Kiria

Ujumbe wa Henry Kileo mume wa Joyce Kiria

Mbona mnarudia rudia huo ujumbe. Au yeye ndiyo anarudia rudia kupost?
 
Ameandika Henry Kileo mume wa Joyce Kiria katika ukurasa wake wa Facebook.

Hakuna chochote katika maisha cha kupigania!

Nguo zako zile bora kabisa kuna mtu kwake ni matambara tu.

Akiba yako kwenye akaunti ya Benki ni sawa na mchango wa mtu katika sherehe tu.

Boyfriend au Girlfriend wako au mchumba ni Ex wa mtu!

Hivyo ni nini hasa cha kujivunia?

Maisha ni mafupi sana na madogo mno kujisikia kuwa mkubwa ama bora kuliko mtu wengine.

"Tupo sote uchi hadi kufa" aliwahi kusema Steve Jobs. Gwiji muanzilishi wa iPhone (ambaye kwa sasa kifo kimemchukua kwa maradhi ya Cancer)

"Hakuna kitu kinachoweza kutuokoa sote Kukabiliwa na kifo".

Naumia kuona watu ambao hujivunia utajiri, uzuri, akili, kiwango cha elimu, umaarufu na vitu vingine vya tamaa za kimwili, kwani hakuna jambo umefanya la mafanikio katika maisha yako ambamo halijafanywa na mtu mwingine ama kupitia

Cheo unachomiliki ofisini leo kilikuwa kinamilikiwa na mtu mwingine kabla na kitatwaliwa na mtu mwingine baadaye, wala hujui mtu huyo anaweza kuwa nani

Kuna jambo moja tu la thamani la kujivunia ambalo ni "MAISHA ndani ya Mwenyezi MUNGU Muumba".

HIVYO ni vema kuwa mwema kwa Jamaa zako na daima tengeneza Marafiki!

Daima kumbuka kwamba watu unaowakanyaga wakati ukiwa njiani kukwea ngazi kwenda juu huenda wakawa ni walewale utakaowakuta kwenye safari yako ya kuteremka ngazi

Hivyo jitahidi usiwe tatizo kwa watu wengine au kufanya maisha magumu kwa mwingine kwa kutumia nafasi yako, kwa sababu kwa wewe kufanya hivyo ipo siku watu hao hao wanaweza kuwa kikwazo kwako siku moja mbeleni.

Kumbuka,hata jani la mgomba wa ndizi kuna siku litanyauka na kuwa majani makavu yasiyo na ukijani tena!

Tafadhali usiwe na Ubinafsi, Wajulishe marafiki wengine kuwa sote tupo njia moja.

Kama siku moja utajisikia kulia, niite. Sina ahadi ya kukufanya ucheke lakini naweza kulia na wewe.

Kama siku moja unataka kukimbia kwenda mbali usiogope simu yangu.Niite nami nakuahidi kukimbia bega kwa bega na wewe!

Lakini, kama siku moja utapiga simu yangu na haina majibu basi njoo kwangu, Huenda nakuhitaji wewe.

Siku moja, mmoja wetu hatutakuwa naye hapa tena na utasikitika juu yake lakini ukiwa umechelewa kwani hutokuwa na nafasi hiyo tena!

Machozi yanaweza kukutoka!,lakini itakuwa umechelewa. Kwa hiyo, mkumbushe na kumwambia kila mtu kama vile ambavyo mimi nimefanya!
Jiwe gizani hilooooo
 
Wewe ndiyo huyo Kileo?

Naassume ni wewe, mbona una matusi sana mzee? Stress nini? Jaribu kupiga puchu au vipi kaka..

Jobs alikua ni co founder wa apple hiyo haimaanishi kua yeye ndiyo muanzisha iphone wewe kuandika tu kua jamaa ni mwanzilishi wa iphone ni komedi.

Jobs kilichomuua ni diet yake ya matunda tupu, hali ilikua mbaya mpaka ikafikia kipindi harufu ya mwili ikabadilika hiyo ilikua ni kabla organ zake hazijafeli.

Consult references zako upya.
sitaki kuendelea kukusemesha sana mzee baba
 
Poa, ila kwa yule demu ulibugi. Piga moyo konde songa mbele
Basi naombe nikurudie, hebu niambie inventor wa iphone ni nani maana kileo kasema no Jobs lakini wewe umekataa
 
Alizzoea kintonga sasa naamin anaanza kuelewa life ngoja maisha yamnyooshe. Atapata tabu saaaana
 
Nilipofika hapo kwenye Steve Jobs mwanzilishi wa iphone amekufa kwa kansa nimeacha kusoma.

Sipendi mtu anayeandika uongo halafu anaandika kama ana uhakika na hiko kitu
Nini kilimuua Steve Jobs?.,
 
Angeyasema haya kabla ya kuachwa tungemheshimu. Hii ni soni kubwa sana mwanamme kupewa talaka mchana kweupe.
Ungemweshimu Wewe na nani Mkuu!?
Usisemee nafsi za wenzako kuna watu si ajabu wataanzia hapo kumweshimu!
 
[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]
Mkuu, naona leo umenicheka kwasababu nimejaribu kuruka lugha ilio tuogopesha kwa kisingizio cha UMANDE... tehteehhh
 
Back
Top Bottom