Ujumbe wa kufungia mwaka 2021 na kuufungua mwaka 2022

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
UJUMBE WA KUFUNGIA 2021 NA KUFUNGUA MWAKA 2022; MHESHIMU MUNGU KWA MALI ZAKO.

Anaandika Robert Heriel.

Mungu humdharau mwenye Dharau, humheshimu mwenye kumuheshimu.
Tunapoelekea kuufunga mwaka 2021 na kuulaki Kwa furaha mwaka 2022 ujumbe huu utakuwa muhimu katika maisha yako. Ujumbe huu utasomwa na viumbe wote wenye utashi, na kila ausikiaye utamponya.

Niite Taikon wa Fasihi Kuhani katika Hekalu jeusi, mwana wa Nyota ya Tibeli yenye mbawa mbili irukayo.

Zipo Mali tulizonazo na zipo tunazozitafuta. Tunatumia Mali tulizonazo kuzipata tunazozitafuta.

Mali tulizonazo ni miili yetu yenye Afya, akili, na viungo vyetu vya Mwili. Mali hizi ndizo tunazozitumia kupata Mali zinazotuzunguka Kama vile ardhi, majumba, mifugo, viwanda, magari miongoni mwa Mali zingine.

Biblia inasema; Mheshimu Mungu Kwa Mali zako.

Kumheshimu Mungu ndio kufanyeje?

Kumheshimu Mungu katika Mali ni kuzitumia Mali zako ipaswavyo kwa kujinufaisha wewe na familia yako na jamii yako.
Kutomheshimu Mungu katika Mali ni kutumia Mali zako vibaya kujidhuru wewe mwenyewe au familia au jamii yako.

Kwa mfano, mtu anaweza akawa amejaliwa Mali ya maumbile mazuri ya Mwili. Labda ni mwanaume Handsome boy, kitendo cha kutotumia uzuri wake vizuri akautumia kuvunja ndoa za watu au kuharibu watoto wa watu tunasema hamuheshimu Mungu Kwa Mali zake ya uzuri.

Halikadhalika na Wanawake wazuri na wenye maumbo matata. Kutumia umbo lako kudhuru wengine ni kutomuheshimu Mungu.

Uongozi ni Mali isiyoonekana Kama vile Akili tuu. Unapokuwa kiongozi unapaswa umheshimu Mungu Kwa Mali yako hiyo. Sio utumie Mali yako kudharau watu wengine Kwa kuwaumiza, kuwatia jela na kuwasingizia kesi za hovyo hovyo, kuwanyima mishahara Yao, kuwadhulumu haki zao, hiyo tunasema ni kumdharau Mungu katika Mali zako.

Kazi ni Mali inayotokana na matumizi ya akili na nguvu. Unapofanya kazi yoyote lazima umheshimu Mungu katika Mali/kazi hiyo. Sio unamdharau Mungu Kwa kuwanyanyasa watu wake.

Ndugu zangu Askari acheni tabia za kumdharau MUNGU katika Kazi zenu. Unakuta Kaaskari labda kana kacheo Fulani kanadharau mbaya mno. Kanapokea rushwa, kanabambikizia watu kesi na kuwaweka ndani watu wasio na hatia hovyo. Acheni kumdharau MUNGU.
Acheni kuziingiza familia zenu katika laana.

Muheshimuni Mungu katika Mali zenu.

Kumheshimu Mungu ni pamoja na kuzitumia Mali zako vizuri.
Sio kuharibu mwili wako Kwa kunywa mapombe mengi mpaka ukapata madhara. Acha pombe na Kama ukishindwa kabisa basi kunywa Kwa kiasi maana sijasema kunywa pombe mi Dhambi.

Kumheshimu Mungu katika Mali zako ni pamoja na Kula vyakula Kwa kiasi. Sio unakuula mpaka unapata madhara. Unakuta mtu anakuwa Mlafi Kwa kila hovyo hovyo mpaka anapata magonjwa ya unene uliopitiliza au magonjwa mengine. Mheshimu Mungu.

Nafikiri nimeeleweka. Niwaachie Nukuu!

Mithali 3:9
Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.

Mithali 3:27
Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.

Mithali 3:34
Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema.

Kufikia hapo Sina la ziada.

Nawatakia Sikukuu maandalizi Mema ya Sabato, Heri ya sikukuu ya Christmas na Mwaka MPYA.

Ni yule Mtibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kobosho Road, Moshi
 
AMEN AMEN AMEN
 
Back
Top Bottom