Hoja ilitolewa na mchangiaji mmoja kuwa "Maalim hana mpya bora agombee ubunge..." Lakini mchangiaji kashindwa kuona kuwa kipindi anachokizungumzia cha Maalim akiwa kama kiongozi wa chama cha Upinzani ni muda wa miaka kama 15 tu, utawezaje kumhukumu kwa kipindi kifupi cha siasa za upinzani zenye mashaka na vitimbi chungu nzima, katika serikali inayoongozwa na chama chenye historia ya mateso, vitisho na mauwaji dhidi ya wapinzani wake, na licha ya mfumo wa vyama vingi mambo hayajabadlika sana vitimbi hivyo(mifano ipo ukitaka). Licha ya hayo muda mfupi tu wa Maalimu kuongoza upinzani Zanzibar mafanikio ya msingi mengi yamepatikana kwa mfano:
1. Mabadiliko ya Katiba kutokana na Muafaka(1999) yaliyopelekea kuanzishwa kwa taasisi kadhaa za kutoa haki kwa wananchi kama vile Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP) ambayo inaendesha kesi zote za jinai ambazo awali zilikuwa zikiendeshwa na Polisi, waliokuwa wakibambikia watu kesi ovyo ovyo tu,
2. Kubwa zaidi kurejeshwa kazini wafanyakazi waliofukuzwa kwa sababu za kisiasa ama kulipwa haki zao,
3.Uanzishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,
4.Uthubutu wa Maalimu kusema waziwazi uozo wa serikali na chama tawala umeamsha ari na mwamko mpya wa kimageuzi kwa wazanzibari na hasa vijana ambao awali walidanganywa kuwa " vyama vya upinzani vimekuja kuvuruga amani na utulivu na kumrejesha Sultani" kitu ambacho ni uongo.
Mambo ni mengi na sitaki kuchukuwa nafasi na muda wako lakini kwa ufupi tu nikuwa kama haya kayafanya kwa kipindi kifupi tu kama mpinzani "imagine" akipata serikali umbali gani atafika kuleta mabadiliko ya kiuchumi kisiasa na kijamii kwa ujumla, na pengine hata hiyo miaka 40 isifike.
Ukitizama kwa mizania kama hiyo utaona kuwa miaka 40 ya CCM madarakani tofauti na 15 ya CUF kama chama cha upinzani kwa mengi tu.