Ujumbe wa Prof. Mwandosya: Gereza ni chuo cha uanasiasa, kutoka ni kuhitimu

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Katikati ya hofu, kuvunjika moyo na giza la kisiasa, wakati mwingine hutokea mtu anayethubutu kusema kile ambacho wengi wanaogopa kusema.

Mwaka 2018, Profesa Mark James Mwandosya alipomtembelea nyumbani kwake Joseph Mbilinyi (Sugu), baada ya kutoka gerezani, aliandika maneno haya:

“The ultimate college for politicians all over the world.”

Kwa maana nyingine, gereza ni chuo kikuu cha wanasiasa duniani.

Haya si maneno yangu. Ni maneno ya Profesa Mwandosya.

Lakini hakusimama hapo. Aliandika pia:

“Differences of opinion, outlook, political party affiliation or ideology should not be a basis for division, hatred or disunity.”

Kwa Kiswahili: Tofauti za maoni, mtazamo, chama au itikadi hazipaswi kuwa msingi wa mgawanyiko, chuki au kutengana.

Huu ndio utu ninaouzungumzia.

Unaweza kutofautiana na mtu kisiasa, lakini usimpotezee ubinadamu.

Profesa Mwandosya ni msomi wa uhandisi wa umeme, aliyewahi kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye kuwa Waziri katika wizara mbalimbali. Lakini heshima yake kwa watu wengi wa Mbeya na Rungwe haijajengwa na vyeo pekee.

Imejengwa na msimamo.

Mwaka 2018 alizungumza kuhusu misingi ya utawala bora na kukosoa baadhi ya mwenendo wa utawala wa Awamu ya Tano. Muda si mrefu akaondolewa kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, nafasi ambayo baadaye ilichukuliwa na Stephen Wassira.

Katika kipindi cha COVID-19, wakati wengi wakiwa na hofu ya kuzungumza, naye aliweka wazi uzoefu wake wa ugonjwa huo na watu aliowafahamu waliopoteza maisha. Alitibiwa Mbeya na baadaye Nairobi. The Washington Post pia iliwahi kumnukuu katika mjadala kuhusu COVID-19 Tanzania.

Na mwaka 2017, baada ya Tundu Lissu kupigwa risasi, Profesa Mwandosya alitoa pole.

Haya yote yanatuonyesha jambo moja:

Msimamo wa kisiasa haukulazimishi kupoteza utu.

Ndiyo maana nikikumbuka maneno yake kwa Sugu kuhusu gereza kuwa “chuo cha wanasiasa”, najiuliza:

Ikiwa gereza ni chuo, basi kutoka kwake ni nini?

Ni kuhitimu.

Na pengine somo kubwa zaidi ambalo mwanasiasa anaweza kuhitimu si kujua namna ya kushinda uchaguzi, bali kujua namna ya kubaki BINADAMU wakati wa tofauti za kisiasa.

Ninaamini siku moja Profesa Mwandosya akifika gerezani kumtembelea Tundu Lissu, hatakuwa amefanya jambo geni. Atakuwa amerudia ule ule msimamo aliouonyesha kwa Sugu mwaka 2018:

Mpinzani wako wa kisiasa si lazima awe adui yako wa kibinadamu.

Tabia njema, huruma, unyenyekevu na upendo ni vitu ambavyo si rahisi kufundishwa kwa kulazimishwa. Wapo watu wanaweza kuvuliwa madaraka, lakini hawawezi kuvuliwa utu.

Ndiyo maana heshima ya Profesa Mark James Mwandosya kwa watu wa Mbeya na Rungwe imeendelea kubaki.

Vyeo vinaweza kupewa na serikali.
Lakini heshima ya kweli hutolewa na watu.

Na historia inapokuja kuuliza:

“Ulipoona mwanadamu mwenzako akianguka, ulisimama upande gani?”

Jibu la mtu halitapimwa kwa cheo alichowahi kushika.

Litapimwa kwa ubinadamu aliouonyesha.

Credit: Emily Mwakilembe
 
Mbeya walipata msomi ambae aliwapigania sana hata ule uwanja wa ndege wa Songwe bila kuupigia kelele wahuni walikua wanapeleka hela Kilimanjaro kukarabati ule uwanja aliposhinda baadae akatengenezewa zengwe agombanie ujumbe wa NEC na mtoto wa Mwang'ondwa ili kumfifisha tu waliposhindwa na hapo wakashangaa kwenye kugombea nafasi ya Urais kupitia CCM alipata kura nyingi sana hawa ndio watu walifaa kuongoza Taifa hili kwa weredi..
 
Katikati ya hofu, kuvunjika moyo na giza la kisiasa, wakati mwingine hutokea mtu anayethubutu kusema kile ambacho wengi wanaogopa kusema.

Mwaka 2018, Profesa Mark James Mwandosya alipomtembelea nyumbani kwake Joseph Mbilinyi (Sugu), baada ya kutoka gerezani, aliandika maneno haya:

“The ultimate college for politicians all over the world.”

Kwa maana nyingine, gereza ni chuo kikuu cha wanasiasa duniani.

Haya si maneno yangu. Ni maneno ya Profesa Mwandosya.

Lakini hakusimama hapo. Aliandika pia:

“Differences of opinion, outlook, political party affiliation or ideology should not be a basis for division, hatred or disunity.”

Kwa Kiswahili: Tofauti za maoni, mtazamo, chama au itikadi hazipaswi kuwa msingi wa mgawanyiko, chuki au kutengana.

Huu ndio utu ninaouzungumzia.

Unaweza kutofautiana na mtu kisiasa, lakini usimpotezee ubinadamu.

Profesa Mwandosya ni msomi wa uhandisi wa umeme, aliyewahi kufundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye kuwa Waziri katika wizara mbalimbali. Lakini heshima yake kwa watu wengi wa Mbeya na Rungwe haijajengwa na vyeo pekee.

Imejengwa na msimamo.

Mwaka 2018 alizungumza kuhusu misingi ya utawala bora na kukosoa baadhi ya mwenendo wa utawala wa Awamu ya Tano. Muda si mrefu akaondolewa kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, nafasi ambayo baadaye ilichukuliwa na Stephen Wassira.

Katika kipindi cha COVID-19, wakati wengi wakiwa na hofu ya kuzungumza, naye aliweka wazi uzoefu wake wa ugonjwa huo na watu aliowafahamu waliopoteza maisha. Alitibiwa Mbeya na baadaye Nairobi. The Washington Post pia iliwahi kumnukuu katika mjadala kuhusu COVID-19 Tanzania.

Na mwaka 2017, baada ya Tundu Lissu kupigwa risasi, Profesa Mwandosya alitoa pole.

Haya yote yanatuonyesha jambo moja:

Msimamo wa kisiasa haukulazimishi kupoteza utu.

Ndiyo maana nikikumbuka maneno yake kwa Sugu kuhusu gereza kuwa “chuo cha wanasiasa”, najiuliza:

Ikiwa gereza ni chuo, basi kutoka kwake ni nini?

Ni kuhitimu.

Na pengine somo kubwa zaidi ambalo mwanasiasa anaweza kuhitimu si kujua namna ya kushinda uchaguzi, bali kujua namna ya kubaki BINADAMU wakati wa tofauti za kisiasa.

Ninaamini siku moja Profesa Mwandosya akifika gerezani kumtembelea Tundu Lissu, hatakuwa amefanya jambo geni. Atakuwa amerudia ule ule msimamo aliouonyesha kwa Sugu mwaka 2018:

Mpinzani wako wa kisiasa si lazima awe adui yako wa kibinadamu.

Tabia njema, huruma, unyenyekevu na upendo ni vitu ambavyo si rahisi kufundishwa kwa kulazimishwa. Wapo watu wanaweza kuvuliwa madaraka, lakini hawawezi kuvuliwa utu.

Ndiyo maana heshima ya Profesa Mark James Mwandosya kwa watu wa Mbeya na Rungwe imeendelea kubaki.

Vyeo vinaweza kupewa na serikali.
Lakini heshima ya kweli hutolewa na watu.

Na historia inapokuja kuuliza:

“Ulipoona mwanadamu mwenzako akianguka, ulisimama upande gani?”

Jibu la mtu halitapimwa kwa cheo alichowahi kushika.

Litapimwa kwa ubinadamu aliouonyesha.

Credit: Emily Mwakilembe
"Ujumbe wenye uzito. Tofauti za kisiasa hazipaswi kufuta utu. Historia mara nyingi huwakumbuka zaidi wale waliobaki na misingi ya ubinadamu, busara na heshima kwa wenzao hata walipotofautiana. Mwisho wa siku, madaraka hupita, lakini tabia na utu ndivyo vinavyoacha alama kwa vizazi."
 
Inasikitisha sana kwamba tishio la Prof. Mwandosya kuwa raisi baada ya JK kulisababisha awekewe sumu ile ile waliyopewa Nyerere na Mwakyembe. Bila shaka ni jambo lililopangwa na mtu yule yule kwa sababu modus operandi ni moja. Iliwachukua miezi kama sita madaktari wa India kuokoa uhai wake. Hata hivyo, athari za sumu ile zinampata sasa.

Utashangaa watu wale wale waliomtupa Prof. Mwandosya, kumfanyia hila na hata kudiriki kutaka kumuua na kuficha majina mfukoni, siku itokee anatutoka watampamba kwa kila aina ya maneno. Wanafiki wakubwa sana hawa.

Nchi hii, wee acha tu.

Ona pia: Watanzania wengi hawajui kwamba aliesimamia na kupanga mchakato wa ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2000 - 2025 ni Prof. Mark Mwandosya!
 
Bimkubwa mwanzoni alijitahidi kuificha sura yake halisi. Mwisho wa siku ameshindwa. Kiufupi ni zaidi ya katili.
 
Back
Top Bottom